Wewe unaishi Dar, njoo mikoa Kanda ya ziwa ili useme umeme umeenea kila kijiji. Hapa bukombe Jimbo la mh. Doto biteko Kijiji Cha nampalahala tuko gizani tangu Uhuru, huko geita mjini Kijiji kinachopakana au kuelekea eneo la kukuruma wanakochimba dhahabu hata nguzo za umeme hawazijui.
Maeneo ya bisolwa Kona nyangwale wanaona nguzo zinapia na umeme Ila Hakuna transformer. Huku katavi na simiyu usiseme. Mallya unaishi dar kuwa mpole. Niulize waziri wa nishati kwao ni Geita Ila geita vijiji na maeneo mengi hayana umeme na Kama ipo umepita tu wananchi wanahesabu nguzo tu.