Wakati Uingereza wanashinikiza Waziri Mkuu wao ajiuzulu, sisi hapa Tanzani, Polisi anamchoma sindano mfanyabiashara na kumuua tumekaa kimya!

Wew hata jamaa yako jogoo akishindwa kupanda mtungi utamsingizia mwenda zake!

Utahira wenu unataka kumsingizia jiwe!

Mbona lisu alilalama sana kwamba andamaneni mkajificha uvunguni mwa vitanda vyenu?
 
Sisi tupo enzi za ujima !! Africa ni bara la hovyo kabisa.

Karne ya 21 tunafanya mambo ambayo Ulaya waliyafanya karne ya 13...same!!
Kwa sababu ya jiwe?
 
Katika wale 100, lazima yupo Tundu Lisu na Freeman Mbowe, na wengine wachache. Sisi wengine wote, ujasiri hakuna kabisa.

Kama Mungu angenipa nafasi kama aliyopewa Mfalme Suleiman, ningemwomba , Mungu atujalie ujasiri ili tuitetee nchi yetu ili kusiwepo na mtu wa kuiweka chini ya mamlaka ya Shetani.
 
Hakuna kiongozi wa kudai stimulate ubongo, MTKILA hayupo. LISU yupo mbali.
Jaribu kuimagine lile tukio la yule Askari wa US aliyemwua George Floyd, jinsi wamerekani walivyoshinikiza lile tukio Marekani nzima kwa maandamano.....

Hatimaye yule Askari akafungwa jela.

Hapa TZ yetu tunakuwa na taarifa kuwa kuna Polisi kamchoma sindano ya sumu mfanyibiashara wa madini hadi kumwuua na maiti yake imetupwa Baharini, tunaendelea kukaa kimya!
 
kwani ndugu wanasemaje? Si wameridhika mkuu .
 
Umasikini,, Ubinafsi, Ujinga na Uwoga...

Watanzania tumekuzwa hvo toka shule,,, ukihoji shule unaonekana umekaidi unafukuzwa,,,,, hata majumbani tunakuzwa kutohoji lolote... sisi ni ndio tu..

Bado tuna safari ndefu sana kama taifa.... Tunasukuma gari tukiwa tumepanda ndani yake..

-mwisho wa kunukuu-
 
kwani ndugu wanasemaje? Si wameridhika mkuu .
Hakuna cha kuridhika, ila mkwara unaopigwa na Jeshi la Polisi, kuwa ukiandamana, utakutwa na kipigo cha mbwa koko, ndiko kunakotufanya watanzania tuwe waoga kiasi hiki cha kupindukia
 
Sio kila kitu ni maandamano,haya tuandamane kwa lipi A. Askari kwa nn ameua? B. Kwa nn mtu amekufa kwa sindano. C. Kwa nn askari hajatiwa nguvuni?.
 
Wamarekani waliandamani kwa sababu kuu ni ubaguzi wa matukio ya aina ile. Tabia ya watu kama Trump ndio ilipelekea hata wahusika kutotaka kushughulikia kwa sababu tu black lad ndiye aliyeuwawa
 
Milioni 60 au 33?
 
Huu ni utamaduni wa nchi yoyote iliyokuwa ya kijamaa, na hata nchi za kidini. Katika nchi hizi, nchi huwa ya raisi na raia in wapangaji au wapita njia. Nchi zote zilizopitia siasa ya ujamaa RAIA wake ni waoga.
 
Your browser is not able to display this video.
 
Nasikia zamani wakubwa wetu waliwahi kula kitu inaitwa Bulga nadhani hii kitu ndio imeendelea kuathili kizaz hata kizazi
 
Watanzania hatujarogwa wala sio mazezeta ila nyerere alishatuweka wazi mapema sana, tuna maadui watatu tu
1. Umaskini
2. Ujinga
3. Maradhi

Tukifuta umaskini watu hawatauana kwa tamaa ya pesa (kama wapo wanaofanya hivyo)

Tukifuta ujinga ujinga watu watakuwa weledi katika nafasi zao kwa kila mmoja

Tukidhibiti maradhi watu watakuwa na afya nkema ya kuutumia weledi kufanya shughuli halali za kujenga taifa

Tatizo ni pale tunaposhindwa kupambana na hwa maadui badala yake maadui zetu tunadhni ni watanzania wenzetu, hapo ndipo tunachanganya mambo na kufikia hapa tulipo, kila kukicha kulalamika
 
Huu ni utamaduni wa nchi yoyote iliyokuwa ya kijamaa, na hata nchi za kidini. Katika nchi hizi, nchi huwa ya raisi na raia in wapangaji au wapita njia. Nchi zote zilizopitia siasa ya ujamaa RAIA wake ni waoga.
Ni kosa kubwa kuifanya nchi, kuwa ni mali ya Rais🥺
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…