Mukulu wa Bakulu
JF-Expert Member
- Aug 12, 2014
- 4,051
- 12,954
Wakati mwingine unajiuliza kama kiongozi wetu anaelewa anachokifanya ama haelewi chochote kabisa.
Juzi rais akiwa Kagera akasema kodi inayopaswa kukusanywa ni ya mwaka mmoja nyuma tu, miaka ya nyuma mamlaka zilikua wapi. Hapo ndio palinifanya kujiuliza kama rais wetu ana ufahamu hata wa sawa na punje ya haradani kuhusu masuala ya kodi ama hana kabisa.
Leo kampuni kubwa ya Mcdonald, imelipishwa zaidi Tsh Trilioni 2.5 za Kitanzania huko Ufaransa baada ya kugundulika imekua ikikwepa kulipa kodi kwa miaka 14 iliyopita. Mcdonald walikua wanachakachua hesabu na kuonyesha faida kidogo ili kukwepa kodi kwa miaka yote hiyo.
Sasa unajiuliza, iwapo Ufaransa wenye mifumo iliyoendelea bado makampuni yanatumia ujanja kukwepa kulipa kodi ila yakigundulika yanapelekwa mahakamani ana yanakubali kulipa bila kupelekwa mahakamani, kwa Tanzania watu wanakwepa kulipa kodi kisha wanaenda kuomba kwa rais wasilipe na rais anasema wasilipe.
Taifa ambalo haliko thabiti kwenye kukusanya kodi na mfumo wa kodi inaingiliwa na wanasiasa haliwezi kwenda popote.
Hii ndio matokeo yake tunayoyaona sasa, Rais wetu kwa kua hataki watu walipe kodi basi mbadala wake ni mikopo tu, kukopa tu. Tumeona kwenye bajeti yeye anawaza kukopa tuu.
Ndugai alisema ipo siku hii nchi itapigwa mnada na huo ndio ukweli.