Wakati Ulaya wakikusanya kodi ya miaka 20 iliyopita, Tanzania Samia anauliza miaka iliyopita mlikuwa wapi, msikusanye

nimepambana sana kuelewa ulichoandika sijakupata fresh sana but poa tu mkuu haina kwere ngoja masela walete kijiti na big G OG Chuga boy
 
Macdonald imelipishwa baada ya kuwa ktk mgogoro wa kutokulipa kodi.
Sidhani kama wameenda kukusanya kodi ya miaka ya nyuma kwa mackdonald ila alikuwa anadaiwa tayari ni tofauti na leo unamfuata mfanyabiashara na kumkadiria kodi ya mwaka 2015, ulikuwa wapi hukumfikia wakati huo?
 


Ulaya gani hiyo unayoongelea ?? au ya Magufuli Kuzimu ??

Ulaya kila mwaka unaletewa forms za ku declare na pia pesa ya kulipa au kulipwa kulingana na mapato yako uliyopata na kodi uliyolipa .

Kile ambacho utalipwa hutegemea ume declare muda gani lakini haifiki miezi 3 uatakuwa umelipwa , na kama unahitaji kuwalipa watu wa kodi wanakupa muda mpaka december uwe umelipa vinginevyo deni lako linaanza na riba kuanzia mwezi wa Januari na hapa wanakupa muda kama hujawalipa mahakamani unapelekwa
 
Kodi ya miaka ya nyuma ikidaiwa tunalalamika! Ikisamehewa tunalalamika! Ili mradi lazima tulalamike! Loh
 
Soma vizuri article mapato ya licence fees yatokanayo na baadhi ya franchise restaurants zilizopo france wao walikuwa wanayaweka kama mapato wanayopokea Liechtenstein kwenye kodi ndogo.

So kosa lao ni udanganyifu wa kodi through material misstatements toka 2009-2022 ndio kodi wanayolipishwa hiyo kama fidia.
 
Rais hakutakiwa kutoa amri kuwa sheria za kodi zisitekelezwea, angetoa amri kuwa maafisa wa kodi wasifanye kazi kwa kukomoa raia, lazima wasimamie sheria tu.
Hiyo hata Magufuli alihasema lakini ilikua ni kung'ata na kupuliza.

Mh. Rais Samia Suluhu Hassan yuko sahihi kabisa kufuta kodi za miaka zaidi ya miwili iliyopita.

Mimi baba yangu alikua analipa kodi na risiti zilikuwepo kilichotokea mwaka juzi akaletewa deni la mil 90 la miaka 5 ilopita

Tukaenda kupambana nao wakasema wameona imelipwa mil 70 kwa hiyo watadai mil 20
By then tukawa bado hatukubali kwa sababu tulitumia mhasibu anayejua sheria za kodi deni la kubumba likaletwa mpaka mil 9.

Hapo unatarajia kama huna risiti za miaka 5 iliyopita si unaingizwa choo cha kike

Mzee wangu alipata presha iliyoondoa maisha yake.

Hawa jamaa wanabambika, na wana tabia ya kukulazimisha kuwa wewe kwa biashara hii unapaswa kulipa kiasi fulani ambacho wewe mwenyewe ukiangalia tija ya unachokifanya havilingani.
 
Shida ni kwamba mkuu huku kwetu haya yalifanyika kwa ushahidi wenye mashaka sana

Lengo halikuwa kukusanya kodi bali kuwakomoa baadhi ya watu
Kwakua hatupendi kufuata sheria.

Hivyo mtu akiifuata sheria basi yatakuja maneno mengi kama hayo kukomoana udikteta , roho mbaya, katili, dhalimu kumbe ni kwamba watu hawataki sheria ifuatwe kwani hawapati super profit waliyozoea kupata.
 
Mheshimiwa Hangaya anataka kuwa rafiki na wafanyabiashara kwa namna ambayo wao wanataka anasahau kuwa hawa jamaa hawana huruma. Acha watu walambishwe asali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…