Wakati USAID Ikipotea, Tutegemee Vifo na Maambukizi Mapya ya HIV makubwa haijawahi tokea, Tusipochukua hatua ;it is really a timing Bomb!

USAID ilikuwa inapunguzaje maambukizi?

Maambukizi yanatokana na mtu asiye na maambukizi kushiriki tendo la ndoa na mtu mwenye maambukizi bila kinga.

Sasa hapo USAID inahusikaje?
kutoa hela za kununua dawa, kutoa elimu ya kujikinga na magonjwa hayo, mambo ni mengi mpaka msosi hutoa
 
kivipi wakati dawa hizo zinasaidia kuongeza siku?
 
kutoa hela za kununua dawa, kutoa elimu ya kujikinga na magonjwa hayo, mambo ni mengi mpaka msosi hutoa
Elimu gani ambayo sisi hatuijui kuhusu maambukizi ya vvu leo inayotegemea pesa za USAID, dawa gani wanatoa za kuzuia maambukizi ya vvu, na chakula kipi kinazuia vvu?

Labda kama unawatetea watawala, hakuna pesa ya USAID inafanya hizo kazi unazosema wewe, labda uende wazara husika wakupe mgawanyo wa matumizi ya pesa za USAID utuletee upya hapa.
 
Hakuna lolote litatokea wala hakutakua na mass deaths.
Propaganda tu, na dawa zitapatikana kama kawaida.
bora tu ziendelee kupatikana bure, tramp asilete taharuki afrika. Kwa habari ya msaaea wa msosi tutalima na kusaidiana chakula wenyewe waafrika ikitoke muafrika mwenzetu nchi yake imekumbwa na ukame tutampa chakula akalishe watu wake
 
THE BEST THREAD EVER AT JAMII FORUM.. Kama Mods Cookie Moderator Paw tafadharini wekeni STICKY hii thread. Ni ya muhimu kuliko umuhimu wenyewe...

Kudoz mleta thread, Kudoz JF... Hapa tusijadili mada kwa upande wa CCM au CHADEMA au SIMBA na YANGA. Tujadili kwa mustakabali wa taifa letu la leo na kesho..
 
Nice topic mkuu..nimependa insight nimejifunza kitu
 
Twende taratibu,hapo mwisho kabisa unasema ARvs ipo kunusuru ukimwi,na sio binadamu.
Ni kwamba ARvs zilitengenezwa kwa ajili yakufubaza virusi vinavyopelekea mtu kupata ukimwi,(upungufu wa kinga mwilini),,sasa ARvs zikisitishwa na ukimwi ukawa ujanusurika kipi kifuatacho!!,kumbuka ukimwi uko ndani ya binadamu aloathirika,je huyu mwathirika atanusurikaje?!!kifuatacho si ni kifo??au ulikuwa unamaanisha nini mkuu!!,,
 
kivipi wakati dawa hizo zinasaidia kuongeza siku?
HIV hana uwezo wa kusababisha ukimwi. Kama tutamwangamiza kifua kikuu keshokutwa basi ukimwi utakuwa umeangamia leo usiku. Najua hapo hutonielewa. Yaani kama kifua kikuu tutakipoteza miaka miwili ijayo basi ukimwi utakuwa umepotea mwaka mumoja nyuma yake
 
Ngoja kwanza. Ukipima ukimwi leo ukakutwa -ve utaambiwa uje baada ya miezi mitatu. Ukipima tena baada miezi mi3 ukakutwa ni -ve utaambiwa tena njoo baada ya miezi 3. Nini huwa ni hitima ya upimaji huo. ARVs inaweza ikazibwa pengo lake na vitu vingine kabisa kama elimu itatolewa kwa usahihi. HIV ni kitu kingine kabisa wala hakisababishi ukimwi kama tunavyofundishana. Ugonjwa uliouwa watu miaka ya 80_90 huko kagera ya kaskazini mashariki ulikuwa ni kifua kikuu ila akatwishwa HIV hiyo kesi na ndo anapambana nayo mpaka leo. Tukifanikiwa kumuangamiza kifua kikuu kesho basi ukimwi anajizika leo usiku
 
kama kuna ukweli fulani hivi!
 
Tuko twingi tu humu na huwa tunadanganyana sana. Kuna uzi alianzisha FRANCIS DA DON kuhusu hii mada ya HIV/AIDS aliyoandika na wenzake wanavyom-support utasikitika.
Dawa zikipigwa pin, mataifa yatajaa majonzi kila uchwao, na vituo vya afya vinaweza kuelemewa, nguvu kazi zitapukutika sana. Wao wanatazama kwa taswira ya juu tu may be hawakuwahi kuwa mashuhuda enzi zile Ukimwi ni Ukimwi haswa..

Isitoshe enzi hizi namba imeongezeka kupita kiasi
 
tramp aseme tu USAID/PEPFAR itaendelea kusaidia magonjwa ila si miradi mingine aeleweke
Zitanunuliwa sio kutoka bure. Serikali zinazowajari wananchi wao wale wacheza rafu maungoni, zijipange, Trump ni mfanya biashara mzuri sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…