Wakati USAID Ikipotea, Tutegemee Vifo na Maambukizi Mapya ya HIV makubwa haijawahi tokea, Tusipochukua hatua ;it is really a timing Bomb!

Wakati USAID Ikipotea, Tutegemee Vifo na Maambukizi Mapya ya HIV makubwa haijawahi tokea, Tusipochukua hatua ;it is really a timing Bomb!

USAID ilikuwa inapunguzaje maambukizi?

Maambukizi yanatokana na mtu asiye na maambukizi kushiriki tendo la ndoa na mtu mwenye maambukizi bila kinga.

Sasa hapo USAID inahusikaje?
kutoa hela za kununua dawa, kutoa elimu ya kujikinga na magonjwa hayo, mambo ni mengi mpaka msosi hutoa
 
Hakuna atakayefanya kosa kuzuia arvs. Maana hasara ya marekani ni kubwa kuliko afrika. Kuzuia kwa misaada ya ARVs ni kuizika AIDs Afrika. Huu ndo mwisho wa ukimwi. Wachague wao sasa. Wasitishe misaada wa kuusaidia ukimwi uendeleww kuishi ama wautelekeze ukimwi ufie huku afrika. Kumbuka ARVs ipo kwa kuunusuru ukimwi. Siyo kunusuru binadamu
kivipi wakati dawa hizo zinasaidia kuongeza siku?
 
kutoa hela za kununua dawa, kutoa elimu ya kujikinga na magonjwa hayo, mambo ni mengi mpaka msosi hutoa
Elimu gani ambayo sisi hatuijui kuhusu maambukizi ya vvu leo inayotegemea pesa za USAID, dawa gani wanatoa za kuzuia maambukizi ya vvu, na chakula kipi kinazuia vvu?

Labda kama unawatetea watawala, hakuna pesa ya USAID inafanya hizo kazi unazosema wewe, labda uende wazara husika wakupe mgawanyo wa matumizi ya pesa za USAID utuletee upya hapa.
 
Hakuna lolote litatokea wala hakutakua na mass deaths.
Propaganda tu, na dawa zitapatikana kama kawaida.
bora tu ziendelee kupatikana bure, tramp asilete taharuki afrika. Kwa habari ya msaaea wa msosi tutalima na kusaidiana chakula wenyewe waafrika ikitoke muafrika mwenzetu nchi yake imekumbwa na ukame tutampa chakula akalishe watu wake
 
Leo nitajikita kwenye kupotea kwa misaada ya HIV/AIDS tu , tuna watanzania zaidi ya millioni na nusu wanachukua na kupata dawa za HIV/IADS bure kutoka kwenye shirika la USAID, hawa watanzania wanapata vipimo vya serostatus na viral loads kila mwezi kupima maendeleo yao bure kutoka kwenye shirika la USAID, wale wenye maambukizI mapya wanagundulika mapema na wanapata vipimo na kuanza kutumia dawa bure kutoka kenye shirika la USAID, Wagonjwa wa HIV/AIDS wanapata cancelling na usaidizi wa lishe bora pamoja na njia za uzazi salama na za kujikinga kuambukiza wengine bure kutoka katika shirika la USAID. Condom za bei rahisi, virahinishi vyote vinapatika kwa bei subsdized kutoka shirika la USAID.

Sasa sayansi ya tiba inasema seroconvergence inakuwa kubwa mara zaidi ya hamsini (50-80%) mtu akiacha kutumia dawa za chronic illness mfano Kansa au za HIV/AIDS. Ebu tujikite kwenye HIV/AIDS; maana yake wale wadudu waliokuwa wamebakia kwenye sanctuary places wanaibuka kwa nguvu mpya na kasi ya ajabu, sio tu kwenye kuzaliana bali kumutate na kushambulia sehemu zote muhimu za mwili, maini, figo,damu moyo, mapafu, ngozi kwa speed ya ajabu, Mara nyingi hawa wagonjwa hawachukui muda kufariki ni bora wasingeanza dawa, it is non stopable battle of new serocovergence.

Kibaya zaidi, mbali ya virulence potential ya hawa virus wa hawa wagonjwa kuwa kubwa bali infectivity potential yao ni balaa, hapo nyuma uliweza kujamiiana na mtu wa HIV mara zaidi ya 10 bila maambukizi kwa sababu alikuwa yuko kwenye tiba (undetectable viral load); viral load yake ilikuwa very low, na infectivity power ya virus ilikuwa almost negligible.Sasa tutegemee infection rate (incidence) ya HIV kupanda zaidi ya mara 50, unategemea nini kuhusu maambukizi mapya;kumbuka jamii yetu tunaendelea kula bata bila kinga kama kawa, hatujui hawa watu wako kwenye seroconvergence tena wengi wao wamenawili kuliko sisi kajamba nani kutokana na protein za kwenye dawa hizo. Nakuambia hatujawahi kuencounter kitu kama hiki tangia ugonjwa wa HIV ugundulike.

Sasa cha ajabu watunga sera wanasubili disaster itokee, vifo vipangane mahospitalini , new infection rate ifikie zaidi ya 30 % ina maana ratio iwe 1.3 kati ya wagonjwa na wazima, it will be too late my friend na ndipo tushtuke, nakuambia itakua too late. Juzi nilikuwa najiuliza hivi hawa wazungu walipangakwa makusudi yaani "tuwadekeze kwa dawa za bure hawa waafrika, then tu- stop ghafla bila wao kujiandaa, wapukutike na kuambukizana kwa kasi ya ajabu ,hapo tutakuwa tumefikia lengo letu la depopulizing afrika" . Kama ndivyo ilivyokuwa basi watakuwa wamefanikiwa kwa asilima zaidi ya 110%. Na kwa sababu sisi tunaendekeza ngono sana sana tena sana sana na hatuko serious kenye kujikinga na hatujui kuchukua hatua haraka za kulinda jamii yetu, mfano si unaona mpaka sasa ni hatua gani imechukuliwa zaidi ya maneno ya kisiasa.

Nilitegemea nini sasa kwa watunga sera wetu kwenye hili Janga la kitaifa?

1) Kwanza wangefunds na kutoa new emergence strategic plan ya upatikanaji wa dawa na vipimo vya HIV/AIDS kwa uhakika na urahisi kwa wagonjwa wote.

2) Pili nilitegemea wangefund na kutoa new emergence strategic plans za uwezeshaji wa upimaji wa HIV/AIDS kwa uhakika na uharaka.

3) Tatu, tena muhimu zaidi nilitegemea kwa sababu tajwa paragrahy ya 1 na 2 hapo juu kuhusu uwezekano wa maambukizi mapya ya kasi ya umeme tulitegemea watenge fedha na kutengeneza new emergence HIV/AIDS health education , health promotion and prevention strategic plan ambayo iko tailored to the emerging situation

Kwangu mimi hii ya emergence HIV/AIDS health education ,health promotion and prevention strategic plan ambayo iko tailored to the emerging unique situation should be the first priority na ingeanza kuanzia January 2025,it is an emergence because it touches the corner stone of public health initiaves (emergence preparedness & prevention is better than cure). Kwa nini nasema hivyo? nitakueleza? kaa mkao wa kula tu husiwe mbishi, kwani humu jamii forum kila mtu ana PhD ya kila fani, mimi sielewagi comments zetu, kumbuka hii ni sayansi ya public health & health management. Jamani situation tunayoenda kukabiliana nayo hahijawahi kutokea duniani kote ,watu wengi , nchi nyingi kustop ghafla dawa za HIV/AIDS (mass stoppage of medication) na kusababisha mass viral load multiplication, viral mutation na infectivity rate (incidence) kuongezeka. Hii inahitaji another approaches of health education and health promotion ikitarget hizo arms tatu unique zinazotokea baada ya mtu kuacha dawa. It should not be business as usual.

Itabidi turudi kule kama mwanzo kutumia multiple media (news letters, radios, TVs, community dilogies, targeted health education mostly to patients themselves na hawa ni muhimu kwani ndio yatakuwa mbomb ya kulipulia watu. SBS targetting ku-raise community education and awareness, hasa ya nini kimetokea na kinachotokea, nini kifanyike wakati wa sex na mtu aliyeacha dawa, nini kifanyike kwa aliyeacha dawa, nini kifanyike ukijikuta umejichanganya na mtu aliyeach dawa, ni vitu gani muhimu vya kuzingatia wakati unadeal na hawa watu walioacha dawa. Lakini provision ya public assurance, serikali yao inafanya nini kukabiliana na hili janga ili kutoleta mshtuko wa kijamii, ni bora upate mshtuko wa mtu mmoja mmoja na si mshtuko wa jamii.hiyo ni hatari. Je wewe unasemaje kuhusu hatari iliyo mbele yetu.toa maoni yako.....
THE BEST THREAD EVER AT JAMII FORUM.. Kama Mods Cookie Moderator Paw tafadharini wekeni STICKY hii thread. Ni ya muhimu kuliko umuhimu wenyewe...

Kudoz mleta thread, Kudoz JF... Hapa tusijadili mada kwa upande wa CCM au CHADEMA au SIMBA na YANGA. Tujadili kwa mustakabali wa taifa letu la leo na kesho..
 
Nice topic mkuu..nimependa insight nimejifunza kitu
 
Hakuna atakayefanya kosa kuzuia arvs. Maana hasara ya marekani ni kubwa kuliko afrika. Kuzuia kwa misaada ya ARVs ni kuizika AIDs Afrika. Huu ndo mwisho wa ukimwi. Wachague wao sasa. Wasitishe misaada wa kuusaidia ukimwi uendeleww kuishi ama wautelekeze ukimwi ufie huku afrika. Kumbuka ARVs ipo kwa kuunusuru ukimwi. Siyo kunusuru binadam
Twende taratibu,hapo mwisho kabisa unasema ARvs ipo kunusuru ukimwi,na sio binadamu.
Ni kwamba ARvs zilitengenezwa kwa ajili yakufubaza virusi vinavyopelekea mtu kupata ukimwi,(upungufu wa kinga mwilini),,sasa ARvs zikisitishwa na ukimwi ukawa ujanusurika kipi kifuatacho!!,kumbuka ukimwi uko ndani ya binadamu aloathirika,je huyu mwathirika atanusurikaje?!!kifuatacho si ni kifo??au ulikuwa unamaanisha nini mkuu!!,,
 
kivipi wakati dawa hizo zinasaidia kuongeza siku?
HIV hana uwezo wa kusababisha ukimwi. Kama tutamwangamiza kifua kikuu keshokutwa basi ukimwi utakuwa umeangamia leo usiku. Najua hapo hutonielewa. Yaani kama kifua kikuu tutakipoteza miaka miwili ijayo basi ukimwi utakuwa umepotea mwaka mumoja nyuma yake
 
Twende taratibu,hapo mwisho kabisa unasema ARvs ipo kunusuru ukimwi,na sio binadamu.
Ni kwamba ARvs zilitengenezwa kwa ajili yakufubaza virusi vinavyopelekea mtu kupata ukimwi,(upungufu wa kinga mwilini),,sasa ARvs zikisitishwa na ukimwi ukawa ujanusurika kipi kifuatacho!!,kumbuka ukimwi uko ndani ya binadamu aloathirika,je huyu mwathirika atanusurikaje?!!kifuatacho si ni kifo??au ulikuwa unamaanisha nini mkuu!!,,
Ngoja kwanza. Ukipima ukimwi leo ukakutwa -ve utaambiwa uje baada ya miezi mitatu. Ukipima tena baada miezi mi3 ukakutwa ni -ve utaambiwa tena njoo baada ya miezi 3. Nini huwa ni hitima ya upimaji huo. ARVs inaweza ikazibwa pengo lake na vitu vingine kabisa kama elimu itatolewa kwa usahihi. HIV ni kitu kingine kabisa wala hakisababishi ukimwi kama tunavyofundishana. Ugonjwa uliouwa watu miaka ya 80_90 huko kagera ya kaskazini mashariki ulikuwa ni kifua kikuu ila akatwishwa HIV hiyo kesi na ndo anapambana nayo mpaka leo. Tukifanikiwa kumuangamiza kifua kikuu kesho basi ukimwi anajizika leo usiku
 
Tupo hapa tunakula bia kufurahia mwisho wa janga la the so called Ukimwi

In short hizo dawa na vipimo ndo zilikuwa zinaua watu maana ukipima ukiambiwa+ve lazima upanick /fear afya itatetereka then ukishaanza kuzitumia dawa it means utazitumia maisha Yako yote siku ukiacha lazima wasafirishe

Hilo ndio janga tulilokuwa nalo yaani dawa na vipimo sio Ukimwi hakuna ugonjwa unaoitwa Ukimwi duniani hivyo kusitisha dawa indirectly ni sawa na kusitisha Ukimwi Africa,

Eeh Mungu mjalie maisha marefu Trump naamini hili kafanya maksudi kwa kuwa anajua kilichopo nyuma ya pazia, Trump ni nabii
Tunaendelea kufurahia tukigonga glass za bia
kama kuna ukweli fulani hivi!
 
Tuko twingi tu humu na huwa tunadanganyana sana. Kuna uzi alianzisha FRANCIS DA DON kuhusu hii mada ya HIV/AIDS aliyoandika na wenzake wanavyom-support utasikitika.
Dawa zikipigwa pin, mataifa yatajaa majonzi kila uchwao, na vituo vya afya vinaweza kuelemewa, nguvu kazi zitapukutika sana. Wao wanatazama kwa taswira ya juu tu may be hawakuwahi kuwa mashuhuda enzi zile Ukimwi ni Ukimwi haswa..

Isitoshe enzi hizi namba imeongezeka kupita kiasi
 
tramp aseme tu USAID/PEPFAR itaendelea kusaidia magonjwa ila si miradi mingine aeleweke
Zitanunuliwa sio kutoka bure. Serikali zinazowajari wananchi wao wale wacheza rafu maungoni, zijipange, Trump ni mfanya biashara mzuri sana.
 
Back
Top Bottom