HIMARS
JF-Expert Member
- Jan 23, 2012
- 70,791
- 98,334
Hakuna kipaji cha kukata mauno au kucheza muziki.Tupe mfano basi wa wakata viuno walioishia kua mashoga, heshimu vipaji
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hakuna kipaji cha kukata mauno au kucheza muziki.Tupe mfano basi wa wakata viuno walioishia kua mashoga, heshimu vipaji
Uchezaji wa kawaida,video ndio imefanya upate emotions.Big up sana watoto wazuri, hadi machozi yamenitoka
Ufreemason tuuKundi la Ghetto Kids la Uganda laweka HISTORIA na Golden Buzzer kwenye British's Got Talent: Britain’s Got Talent ilirejea kwa msimu wake wa 16 siku ya Jumamosi ambapo kundi la densi la Uganda - GhettoKids - lilipata tuzo ya Golden Buzzer.
View attachment 2591136
BritainsGotTalent ni shindano la vipaji linaloonyeshwa kwenye televisheni nchini wingereza ambapo watu binafsi au vikundi huonyesha vipaji mbalimbali kama vile kuimba, kucheza, uchawi, vichekesho na zaidi. Maranyingi onyesho hutunikiwa Golden Buzzer mwishoni mwa usaili, na kupata nafasi ya kushiriki nusu fainali.
Jaji wa Italia Bruno Tonioli, aligonga Golden Buzzer katikati ya onyesho la Ghetto Kids.
"Lazima niifanye sasa," Tonioli alisema kabla ya kupiga kelele.
Watoto hao, walio na umri wa miaka mitano hadi 13, walicheza nyimbo mbalimbali ambazo zilifurahisha umati, kiasi kwamba Tonioli, hakuweza kungoja hadi mwisho mwa usaili wao, jambo ambalo halijawahi kufanywa hata mara moja.
Ghetto Kids wamepata umahiri wa kimataifa kwa ustadi wao wa kucheza na wametumbuiza hadhira mbalimbali, akiwemo mwimbaji Eddy Kenzo na rapa wa Marekani French Montana. Pia wametumia jukwaa lao kuhamasisha kuhusu umaskini na changamoto zinazowakabili watoto wanaoishi katika vitongoji duni.
Pia wametumbuiza katika matukio mbalimbali duniani, ikiwa ni pamoja na Tuzo za BET na Tuzo za Chaguo za Watoto za Nickelodeon.
Hao watoto ni wa eddy kenzo? I mean yeye ndio mwenye kituo?Safi sana kwao👏🏻👏🏻👏🏻. It is amazing. Sijawahi pinga ubora wa hawa watoto toka nimeanza kuona ushiriki wao kwenye hizi vitu.
Hongera ziende kwa eddie kenzo. Kaibeba sana uganda na hawa vijana.
Hapana. Ila anawatumia sana kwenye nyimbo zake na nyimbo za vijana wake.Hao watoto ni wa eddy kenzo? I mean yeye ndio mwenye kituo?
Halafu wengine yatima masikiniI'm so happy, especially baada ya kusikia comment ya Simon.
Go kids. [emoji1319]
Kweli kabisa ndugu, wanastahili kupata furaha, na wamefurahi kweli na watazamaji wamefurahi.Halafu wengine yatima masikini
Kweli wanastahili furaha
SanaKweli kabisa ndugu, wanastahili kupata furaha, na wamefurahi kweli na watazamaji wamefurahi.