Hii ya Kenya kukata mishahara 3% ya wafanyakazi sikubaliani nayo. Lakini idea ya kuwajengea nyumba masikini nakubaliana nalo 100%. Hapa Tanzania akitokea rais akaamua kuanza na masikini nchi nzima kujenga makao yao na kuwapa huduma zote muhimu matibabu, chakula, ulinzi na upendo hakika nitamsifu sana. Kila wilaya iwe na nyumba za kuwaweka masikini na wazee wasiokuwa na ndugu na hawajiwezi wawekewe huduma zote. Nilibahatika kutembelea nyumba moja ya wazee huko ulaya hakika niliwaonea wivu wale wazee wanahudumiwa kama wapo nyumbani wana kila kitu, wahudumu, dining room, dispensary full equipped, ambulance, na madaktari wao, michezo, library, vitabu na magazeti ya kila siku, sehemu ya kuendesha ibada (chapel), Tv, bustani, vyumba self contained na basi la kuwatembeza mjini nk alafu wanapewa posho ya kujikimu mahitaji binafsi na kila Ijumaa wanapewa free ticket ya kupanda usafiri wa serikali kwenda popote mjini hadi jioni saa 12. Nyumba hizo zinatunzwa na ni safi sana. Viongozi wa juu wa serikali wana ratiba maalum ya kuwatembelea. Tanzania tunaweza kama tukiamua mfano haya madini tunayochimba tukichukua zile fedha za makanikia tu zinaweza kujenga hizi nyumba. Wenzetu kule Zanzibar Marehemu Karume 1 alijenga hizo nyumba na aliweka baadhi ya huduma muhimu, baada ya kuondoka kila kitu kikafa ukienda kuwatembelea unaweza kulia ukiwaona wale wazee. Mimi mara ya mwisho kwenda kwenye hizo nyumba ilikuwa miaka mitano iliyopita sina uhakika kama kuna maboresho yoyote yaliyofanyika. Rais pia ajitahidi kulipa posho au pension kwa wazee wote wastaafu bila ya kujali kama aliajiriwa serikalini au alikuwa mkulima wazee wote wanastahili pension kutoka serikalini. Baada ya hapo tuhamie kwa vijana wasiopata ajira mradi wawe na umri unaokubalika nao walipwe posho ya kujikimu. Wakati umeshafika sasa kila raia alambishwe asali sio hao wachache mzee rope na wenziwe tu.