Wakati Wa Tanzania Wakipinga Tozo ya Barabara za TARURA, Wafanyakazi wa Umma Kenya Kukatwa Asilimia 3% ya Mishahara Kujengea Nyumba za Watu Maskini

Kenya sgain😔 Mnapenda kutuletea mambo ya kenya akili zenu zinamakenya? si mhamie huko kama mnawapenda sn?
Kenya haituhusu, sisi tuna namna yetu ya kufanya mambo na wao pia acheni kuwashobokea wakati wao huwa wanawadharau!!
 
Hii ya Kenya kukata mishahara 3% ya wafanyakazi sikubaliani nayo. Lakini idea ya kuwajengea nyumba masikini nakubaliana nalo 100%. Hapa Tanzania akitokea rais akaamua kuanza na masikini nchi nzima kujenga makao yao na kuwapa huduma zote muhimu matibabu, chakula, ulinzi na upendo hakika nitamsifu sana. Kila wilaya iwe na nyumba za kuwaweka masikini na wazee wasiokuwa na ndugu na hawajiwezi wawekewe huduma zote. Nilibahatika kutembelea nyumba moja ya wazee huko ulaya hakika niliwaonea wivu wale wazee wanahudumiwa kama wapo nyumbani wana kila kitu, wahudumu, dining room, dispensary full equipped, ambulance, na madaktari wao, michezo, library, vitabu na magazeti ya kila siku, sehemu ya kuendesha ibada (chapel), Tv, bustani, vyumba self contained na basi la kuwatembeza mjini nk alafu wanapewa posho ya kujikimu mahitaji binafsi na kila Ijumaa wanapewa free ticket ya kupanda usafiri wa serikali kwenda popote mjini hadi jioni saa 12. Nyumba hizo zinatunzwa na ni safi sana. Viongozi wa juu wa serikali wana ratiba maalum ya kuwatembelea. Tanzania tunaweza kama tukiamua mfano haya madini tunayochimba tukichukua zile fedha za makanikia tu zinaweza kujenga hizi nyumba. Wenzetu kule Zanzibar Marehemu Karume 1 alijenga hizo nyumba na aliweka baadhi ya huduma muhimu, baada ya kuondoka kila kitu kikafa ukienda kuwatembelea unaweza kulia ukiwaona wale wazee. Mimi mara ya mwisho kwenda kwenye hizo nyumba ilikuwa miaka mitano iliyopita sina uhakika kama kuna maboresho yoyote yaliyofanyika. Rais pia ajitahidi kulipa posho au pension kwa wazee wote wastaafu bila ya kujali kama aliajiriwa serikalini au alikuwa mkulima wazee wote wanastahili pension kutoka serikalini. Baada ya hapo tuhamie kwa vijana wasiopata ajira mradi wawe na umri unaokubalika nao walipwe posho ya kujikimu. Wakati umeshafika sasa kila raia alambishwe asali sio hao wachache mzee rope na wenziwe tu.
 
Huwa nasema mara nyingi sana kwamba Tanzania hii Serikali inadekeza sana Watu hasa wa Mijini..

Imagine mtu anakataa tozo ya mafuta Shilingi 100 ambayo inatakiwa Kujengea Barabara ila Barabara anazitaka.

Kama Mfanyakazi wa Umma anakatwa Asilimia 3% Kila Mwezi hiyo ni zaidi ya 10,000 Kila Mwezi eti Kwa Ajili ya Kujengea Watu Nyumba kana kwamba huyo Mfanyakazi ndio amesababisha watu kuwa Maskini na kukosa makazi..

Watu hatupingi Tozo shida ni matumizi ya Tozo mfano mfano kunahii Tozo yamiamala Nitajie manufaa yake napia uniambie Tozo imefanya nini nanini?
 
rais akaamua kuanza na masikini nchi nzima kujenga makao yao na kuwapa huduma zote muhimu matibabu, chakula, ulinzi na upendo hakika nitamsifu sana. Kila wilaya iwe na nyumba za kuwaweka masikini na wazee wasiokuwa na ndugu na hawajiwezi wawekewe huduma zote.
Hilo sio suluhisho wakati mijitu haina mbele wala nyuma inatotoa tu vifangara kama kuku halafu wanapotea
Ndio utaongeza jamii ya masiikini wakidhani maisha ni mdebwedo
Unatakiwa kuwatakaza kuzaliana kama kuku, yule mpuuzi aliturudisha nyuma sana
Mabeberu wamefanikiwa kuhakikisha kila mwananchi ana makazi yake, kwa kuhamasisha kuacha kuzaliana kama nzige, na wananchi wao wakafuata hayo baada ya vita kuu ya pili ya dunia, zamani na wao walikuwa kama sisi tu.
 
Hii ya Kenya kukata mishahara 3% ya wafanyakazi sikubaliani nayo. Lakini idea ya kuwajengea nyumba masikini nakubaliana nalo 100%. Hapa Tanzania akitokea rais akaamua kuanza na masikini nchi nzima kujenga makao yao na kuwapa huduma zote muhimu matibabu, chakula, ulinzi na upendo hakika nitamsifu sana. Kila wilaya iwe na nyumba za kuwaweka masikini na wazee wasiokuwa na ndugu na hawajiwezi wawekewe huduma zote. Nilibahatika kutembelea nyumba moja ya wazee huko ulaya hakika niliwaonea wivu wale wazee wanahudumiwa kama wapo nyumbani wana kila kitu, wahudumu, dining room, dispensary full equipped, ambulance, na madaktari wao, michezo, library, vitabu na magazeti ya kila siku, sehemu ya kuendesha ibada (chapel), Tv, bustani, vyumba self contained na basi la kuwatembeza mjini nk alafu wanapewa posho ya kujikimu mahitaji binafsi na kila Ijumaa wanapewa free ticket ya kupanda usafiri wa serikali kwenda popote mjini hadi jioni saa 12. Nyumba hizo zinatunzwa na ni safi sana. Viongozi wa juu wa serikali wana ratiba maalum ya kuwatembelea. Tanzania tunaweza kama tukiamua mfano haya madini tunayochimba tukichukua zile fedha za makanikia tu zinaweza kujenga hizi nyumba. Wenzetu kule Zanzibar Marehemu Karume 1 alijenga hizo nyumba na aliweka baadhi ya huduma muhimu, baada ya kuondoka kila kitu kikafa ukienda kuwatembelea unaweza kulia ukiwaona wale wazee. Mimi mara ya mwisho kwenda kwenye hizo nyumba ilikuwa miaka mitano iliyopita sina uhakika kama kuna maboresho yoyote yaliyofanyika. Rais pia ajitahidi kulipa posho au pension kwa wazee wote wastaafu bila ya kujali kama aliajiriwa serikalini au alikuwa mkulima wazee wote wanastahili pension kutoka serikalini. Baada ya hapo tuhamie kwa vijana wasiopata ajira mradi wawe na umri unaokubalika nao walipwe posho ya kujikimu. Wakati umeshafika sasa kila raia alambishwe asali sio hao wachache mzee rope na wenziwe tu.

So mkuu ulitembelea na kuuliza maswali au uliona Tu kwa macho ukajua nyumba za wazee ni bure? Ulaya cha bure pumzi tu.
 
Wazo LA kijinga sana.
Kenya hawana tozo za kwenye miamala.
Kenya hawana tozo za luku na mita za umeme.

Ukisoma report ya CAG utaona namna hela inavyoliwa na hao waweka tozo.
So, tozo ya sh 100 sio mbadala Bali ni wanasiasa kujiongezea wigo wa kula tuu.
Hayo mambo hayakuwepo na bado nchi ilipiga hatua. Awamu za tozo zimeanza baada ya Magufuli kufa.
 
Ni roho ya wivu tuu na si kingine.
Wivu wakati nalipa Kodi za kutosha kuwalipa mishahara nyie watumishi hewa. Kutwa mnatusumbua na njaa zenu kuomba kickbacks, no wonder mkistaafu mnarudi nyuma kimaendeleo.
 
Ruto anataka kutoza walio na mshahara aslimia tatu kwa lazima ili kujenga manyumba.Watu hawataki kukatwa pesa hizo kwani wamechukua mkopo kujenga nyumba wengine washajenga nyumba na hawaoni maana ya kulipia nyumba ambazo hatuna hakika .Alafu pia hii serikali inajulikana kwa wizi kuna uwezekano hizi pesa zitaibwa
 
Back
Top Bottom