Wakati wa ujenzi wa Reli ya TAZARA (1968 – 1975) zaidi ya Wafanyakazi 160 walifariki kwa ajali na magonjwa

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Wakati wa Ujenzi wa Reli ya TAZARA zaidi ya Wafanyakazi 160 walifariki kwa ajali na magonjwa, kati yao Wachina walikuwa 64. Ujenzi ulihusisha Vibarua na Wahandisi 38,000 kutoka Tanzania na Zambia, pia timu ya Wataalam na Wahandisi 13,500 kutoka China.

Reli hiyo iliyojengwa kati ya Mwaka 1968 hadi 1975 kutoka Kapiri Mposhi (Zambia) hadi Dar es Salaam (Tanzania) ina urefu wa Kilometa 1860.

Siku ya kuwakumbuka watendaji mbalimbali walipopoteza maisha katika ujenzi wa reli hiyo huadhimishwa Aprili 1 ya kila mwaka.

Picha: Mtandao
 
Walikuwa na wakati mgumu sana na machine zilikuwa bado sana kila kitu kilikuwa ni kutumia nguvu tu

Ni huzuni sana kwa watu waliojitolea na kupoteza maisha
Poleni ndugu wa wafiwa

Kuna nyingine ile ya Kenya / Uganda railway
Wale Simba wala watu wa Tsavo 1898
Walikula watu 135
Nimeongezea tu wakuu
 
Hii reli kila nchi ingejitegemea tu. Maana Zambia imekuwa ni mzigo kwa Tanzania mpaka basi.
 
Hi reli upande wa Zambia umekuwa tegemezi na mzigo kwa Tanzania heri tungejitenga nao tu kuliko hivi sasa ...biashara iko upande mmoja tu
 
Aprili 1 siku ya wajinga anyway! By the way, ni kawaida sana kwa idadi hiyo isingewezekana kwa miaka 7 ya ujenzi watu wasife. Unadhani SGR hawafi? Ikiwekwa idadi hapa hutoamini.

Ujenzi wa Mombasa - Nairobi enzi za ukoloni mkongwe wajenzi wa kutosha waligeuka mboga ya simba hapo Tsavo usiombe! Simba waliwala kweli kweli hadi huruma ila ndio hivyo punda afe mzigo ufike achana na mkoloni aliyekuwa na malengo yake.
 
Ni Halali maana syo Kwa Yale mahandaki??

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…