Wakati Waafrika wakiuzwa kama watumwa, Mashehe, Mapadre, wachungaji wa Ulaya, Amerika na Uarabuni walikuwa wapi?

Ndivyo ulivyoambiwa kanisani ?? Yaani muuzaji kajizuia kuuza 😝😝😝 Mkunazini hapajapata kuuzwa mtumwa hata mmoja. Kile kiwanja walipewa kanisa na Muingereza akaona ajenge kanisa na kuweka propaganda yake kuwa pale waliuzwa watumwa
 
Biashara ya Utumwa nchini Tanganyika iliendeshwa na Waarabu.
Sio Waarabu tu hata wazungu jiulize swali Kilimo cha Katani katk mikoa kama Morogoro Tanga kilianzishwa na akina nani na wale watumwa waliokuwa wakilima huko walikuwa wakitumikishwa na akina Nan? na walipatikana vipi?
 
Hii propaganda ya kuonekana mwarabu kafanya biashara ya utumwa na wazungu wanaonekana watetezi wa utumwa kupitia kanisa itaisha lini?? Mbona ni old way sanaaa watu wanashtuka kaka
 
Kama unasema kwamba "Mungu hajawahi kuonekana"
Mungu ni roho tunayoiona kupitia matokeo ya nguvu zake,haiwezekani kumwona ktk macho au vipimo vya maabara.
Walio sema Mungu yupo, walifanya uchunguzi gani na utafiti upi waka gundua kwamba huyo Mungu hawezi kuonekana?
Mungu ni roho,inabidi ufahamu roho ni nini ipi uwe na msingi mzuri wa kuuliza maswali yako.
Walifahamu vipi kwanza huyo Mungu yupo?
kwa kupitia matokeo ya kazi zake,ambazo ni kama shamba zuri lililopaliliwa na kupandwa mazao kwa ustadi.
Kisha wakaja na hitimisho kwamba huyo Mungu yupo ila hajawahi kuonekana?
Mungu ni roho tunamjua na tunamuona kupitia kazi zake si kwa macho.
Yaani wajue Mungu yupo, Halafu hapohapo waseme hajawahi kuonekana!!!
Mungu sio charger yako ya simu kwamba unapoiweka itakaa hapo na kama unajua ipo basi ni kwa kuiona.
Huoni , Hoja ya uwepo wa huyo Mungu ni ndoto za kufikirika?
kufikirika ndio point yenyewe ya uwepo wa Mungu,inafaa uwe na fikra kubwa zaidi kuona uwepo wake,vinginevyo utaanza kuuliza ameonekana wapi kama ufanyavyo wewe hapa
 
Mleta mada nimesoma kichwa cha habari nikachoka kabisa na kuona mada yako ni ya hovyo na isiyo na akili.
Bora ungekaa tu kimya kuficha ujinga!
 
Unaweza kuwa sawa...ila sasa kumbe huwa tunasoma history ya uongo kwamba wamissionari walikuwa agents of colonialism? Hii u turn kutoka kuwa agents mpk wakombozi ndio haieleweki nini ilisababishwa na nini? Au ni baada ya kuona wamenufaika vya kutosha?
 
Sio historia ya uongo, missionaries were agents of colonialism and letter agents of abolition of the slave trade.
P
 
Sio historia ya uongo, missionaries were agents of colonialism and letter agents of abolition of the slave trade.
P
Hii sawa sawa.. basi waombe radhi kwa kutesa watu na si kutaka wawe praised kwa kuondoa tatizo waliloleta wao. Kama tu issue ya pesa za bureau de Change ambayo serikali iliziteka na leo wanatangaza kuzirudisha. Kuna habari hapo?
 
Hii sawa sawa.. basi waombe radhi kwa kutesa watu na si kutaka wawe praised kwa kuondoa tatizo waliloleta wao. Kama tu issue ya pesa za bureau de Change ambayo serikali iliziteka na leo wanatangaza kuzirudisha. Kuna habari hapo?
1. Kanisa Katoliki waliisha omba radhi kuunyamazia utumwa.
2. Tunafundishwa kuwa watu wa shukrani, ukitendewa mabaya shukuru, ukitendewa mema shukuru.
3. Tulipo piga marufuku mikutano, tulinyamaza, mikutano ilipo ruhusiwa tukashukuru Mungu!.
4. Waliopora fedha bureau tulinyamaza, wanaporudisha, tunashukuru!.
5. Agents of colonialism anapozuia utumwa tunamshukuru.
P
 
Waarabu waliwafanya nini enyi wafuasi wa paulo? Mbona kila kitu waarabu waarabu!! Huko mashuleni hadi kwenye vitabu waarabu waarabu sijui kama bado yapo hayo madudu mliyo aminishwa!!
Shule tulizofundishwa ni zile za elimu ya propaganda (ni story ya uongo ambayo itaelezwa kizazi kwa kizazi mpaka iamini hii ni kweli) nchi hii kabla ya koloni ilikuwa chini ya dola ya kiislamu na moja ya fitina walianza kwa kutumia michoro mpaka leo kkkt wanapiga kelele et bandari anapewa mwarabu ataleta utumwa wao wamefanya nn zaidi ya kuzidisha umaskitin
 
Sawa mkuu tushukuru kwa Kila jambo.
Hivi tunawezaje wasaidia West Africa kutoka mikononi mwa Mfaransa?
Sisi angalau tumetoka kiasi chake mkoloni wetu hakuwa king'ang'anizi wao je?
Tanzania tulikuwa kiongozi enzi za ukombozi kupigania uhuru kusini mwa Africa vipi Leo hatuna la kufanya kabisa kusaidia huko West Africa?
 
Kwahiyo, Kwasababu wakati mtume anaeneza UISLAMU hukuwepo basi taarifa hiyo siyo ya KWELI?, Hiyo itakuwa akili ya ajabu sana.
KIFUPI: Historia inatuwezesha kupata taarifa kupitia wale waliokuwepo wakati huo ambao walishuhudia tukio likitokea( eye witness).
 
Basi Mungu huyo Hayupo katika uhalisia ni dhana ya kufikirika tu isiyo kuwepo inayo dhaniwa ipo.

Imaginations just an illusion.
 
Mjerumani alimpeleka nani utumwani?
 
Sio Waarabu tu hata wazungu jiulize swali Kilimo cha Katani katk mikoa kama Morogoro Tanga kilianzishwa na akina nani na wale watumwa waliokuwa wakilima huko walikuwa wakitumikishwa na akina Nan? na walipatikana vipi?
Hata babu yangu alishawahi fanya kibarua kwenye mashamba hayo.Kwa mujibu wa babu yangu walikuwa wanatembea kwa miguu kwa hiari yao wenyewe kutoka Sumbawanga kwenda Morogoro na Tanga kutafuta hela kwenye mashamba ya Katani na hizo hela zilitumika kununulia ng'ombe kwa wakati huo.Kwa hiyo utumwa wa Mzungu na Mwarabu ni vitu viwili tofauti,kwa Mzungu ulikuwa ni sehemu ya kutafutia utajiri lakini kwa Mwarabu ulikuwa ni sehemu ya kufukarisha watu weusi na kuwafanya omba omba.
 
Nao

Babu Yako alikudanganya sana kwaiyo unataka uniambie hata wakati inajengwa Reli ya kati na mjeruman Babu zetu walifanya kazi kama vibarua kwa hiyari yao?
 
Uliza kwanza watemi walikuwa wapi?sababu watemi ndio walihusika sehemu kubwa kuwauza vijana kwa waarabu na waarabu kuuza kwa wazungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…