"Wakati watu wanalia kuhusu kikokotoo nilikuwa naona kawaida, sasa nimeona ukali wake" Mtumishi aliyeambulia 10M baada ya kustaafu miaka 33 Magereza

Mkombozi ni shamba tu! Maana yake shamba la bei poa, kinyumba cha gharama nafuu sana wenyewe wanaita SLOPE , weka solar .

Fuga kuku wa kienyeji, kipindi cha kilimo Lima kwa utaalam, mambo mengine muombe Mungu.
 
Acha hao mapolisi waijue CCM LIVE. tukiandamana bandari isiuzwe wako mstari wa mbele kuitetea CCM. Tukidai katiba mpya wanasema tunaleta vurugu.
Wacha wazisome namba.
Mapolisi wakumbuke kwamba mbunge akustaafu baada ya miaka mitano ya bila kusema chochote bungeni analipwa milioni Mia mbili sabini. (Kwa miaka mitano) polisi miaka 33 milioni ishirini.
Kudumu chama Cha mapunduzi.
 
Mm najuta sana, mkataba umeisha toka mwaka jana May, nafutalia pesa zangu lakin bilabila unaambiwa mpk miaka 55-60 wakati hata 40 sijafika mamaeeeeh
Ila mbunge anapata stahiki zake siku ya kuvunja bunge.

Tena haambiwi akalete cheti cha ushindi wake wala kitambulisho cha ubunge.

Ajabu mtumishi mnyonge baada ya kutumika miaka 30+ siku ya kufuatilia mafao uchwara anaambiwa apeleke barua ya ajira, barua ya kuidhinishwa kazini, kitambulisho cha NIDA na makaratasi lukuki kisha anasugua benchi kusubiria mafao kiduchu ya kikokotoo cha CCM.
 
Mkombozi ni shamba tu! Maana yake shamba la bei poa, kinyumba cha gharama nafuu sana wenyewe wanaita SLOPE , weka solar .

Fuga kuku wa kienyeji, kipindi cha kilimo Lima kwa utaalam, mambo mengine muombe Mungu.
Tatizo letu watanzania wengi tunadhani KILIMO ni rahisi, eti mtu umezeeka umestaafu ndio unatafuta shamba, kimsingi unatafuta kifo, hapa jf ukiigia jukwaa la kilimo ndio utaona baadhi changamoto za kilimo, ukitaka kulima anza kabla hujastaafu
 
Tatizo letu watanzania wengi tunadhani KILIMO ni rahisi, eti mtu umezeeka umestaafu ndio unatafuta shamba, kimsingi unatafuta kifo, hapa jf ukiigia jukwaa la kilimo ndio utaona baadhi changamoto za kilimo, ukitaka kulima anza kabla hujastaafu
Unajua, kikokotoo ni PIGO la ghafla toka serikalini, kutoka kutegemea 55,000,000/= halafu unakuja pata 10,000,000/= . Usipotuliza akili, usipopata faraja toka watu wako wa karibu haswa familia !! UTACHIZIKA/ STROKE itakunyemelea.

Ushauri wangu huo, eneo dogo nimefanya na naendelea kufanya!. Kilimo ninachokizungumzia hapo ni kile cha kukufanya uwe na chakula.

Mfano - mm mwaka jana nimelima eneo dogo sana hapa ninapoishi kama robo heka au pungufu ya hapo nimepata kama gunia 1, mwaka huu nategemea kulima kama heka 5 maana tayari nimepata uzoefu mkubwa. Maana nililima kwa kufuata ushauri mtandaoni nilipanda kwa mbolea tatizo nilisafiri hivyo mbolea ya kukuzia sikuweka yaani nilitakiwa DAP /UREA/CAN .

Hivi sasa nafuga kuku na ninao kuku wa kienyeji , pamoja na kanga, ifikapo mwezi wa Dec 2024 Kwa uwezo wa Mungu ntakuwa nimepiga hatua kubwa na kusahau kabisa mambo ya KIKOKOTOO maana kimeniumiza sana.

Pension yangu imebidi nimpe kadi binti yangu aliyeko CHUO KIKUU maana kanyimwa mkopo, ukizingatia nikiwa kazini nilimsomesha shule za kulipia.
 
hali ni tete wacha watumishi wakomeshwe wanaikumbatia sana ccm,juzi mwalimu wa secondary mwandamizi kastaafu kaambulia milion 33 alitegemea 80,huku wakimuahidi kalaki 4 kila mwezi
 
Tatizo letu watanzania wengi tunadhani KILIMO ni rahisi, eti mtu umezeeka umestaafu ndio unatafuta shamba, kimsingi unatafuta kifo, hapa jf ukiigia jukwaa la kilimo ndio utaona baadhi changamoto za kilimo, ukitaka kulima anza kabla hujastaafu
Anza immediately ndani ya miaka miwili baada ya kuajiriwa
Baada ya miaka 5 huwazi hata mshahara
 
Maisha ya askari walio chini ya wizara ya mambo ya ndani ni magumu haswa. Huyu Ssgt amewawakilisha wengi ambao wengi wao hawawezi kuongea kutokana na utumishi wao.
 
Pension ya kila mwezi ndio kitu gani mkuu?
Baada ya kustaafu kuna ile hela mkupuo, siju niite ya kikokotoo inayolalamikiwa, lakini kuna pesa unapata kila mwezi, wanadai ni robo ya mshahara wako wa mwisho, nimewahi kusikia kuwa Askari Wana utaratibu tofauti, sasa ndio maana nikauliza, kuna wadau wakanishambulia, ndo nikawa mpole!!!
 
Ni vyema kuuliza kwanza kabla ya kutoa maelezo kama vile Jambo unalifahamu vizuri. Hapa ukumbuni wapo watu wenye uwelewa na kada mbalimbali mkuu. Usijari lakini utaelezewa na kuelewa hapahapa
 
Hao wa majeshi ni wapuuzi sana....hata watumishi wa kawaida sisi wanatudharau.....hata mkilalamika katika vikao tu vya gambe ndio wanaenda kutuchoma hovyo sana hao.....
 
Hiyo milioni 10 anunue pikipiki 2 ambazo ni almost 6m awe analetewa hesabu hiyo nne ndiyo akahangaike kutafuta shamba ambalo halitazidi 1m aanze kilimo mdogomdogo ataweza kuwa na uzee mwema kidogo
Boda hawahawa!?? Au Kuna wengine wa kutengeneza kama roboti Eunice!?? ....
 
Naskia Kuna pension ya Kila mwezi je pia nayo hapati?
Kwa KUMBUKUMBU zangu ..... Pensheni ya kila mwezi ni 67% ya mshahara aliostaafia AMBAPO pia Kwa awali alikuwa apokee 75% ya mshahara aliostaafia ..Sasa unajua mshahara wa sajent wa Magereza !??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…