"Wakati watu wanalia kuhusu kikokotoo nilikuwa naona kawaida, sasa nimeona ukali wake" Mtumishi aliyeambulia 10M baada ya kustaafu miaka 33 Magereza

"Wakati watu wanalia kuhusu kikokotoo nilikuwa naona kawaida, sasa nimeona ukali wake" Mtumishi aliyeambulia 10M baada ya kustaafu miaka 33 Magereza

analia kwa Furaha baada ya kukunja 21m at once ambayo haijawahi kuishika, analia kwasabb kachelewa kuzipata hizo 21m kwa sababu mbalimbali au analia kwa sababu fedha alizopata ni kidogo kutokana na kiasi kingine kulipa deni alilokopa na kumsaidia mwenye? au analia kwa Furaha kwasabb kiasi kilichobaki kitamsadia kwa muda marefu pole pole kidogo kidogo 🐒

na umejuaje analia kwa miongoni mwa sababu hizo hapo juu? wewe ni nani wake kwanza 🐒

aulizwe vizuri, huenda ana matatizo mengine binafsi makubwa zaidi, lakini Sheria hii haibagui cheo au nafasi ulioko. Sheria ni msumeno yeyote atakaestaafu atafuata sheria ya kikokotoo iliyopo 🐒
Na wabunge!?? Walipitisha inawahusu!?? Uchawa ukizidi unakuwa fwalaaa
 
Mkombozi ni shamba tu! Maana yake shamba la bei poa, kinyumba cha gharama nafuu sana wenyewe wanaita SLOPE , weka solar .

Fuga kuku wa kienyeji, kipindi cha kilimo Lima kwa utaalam, mambo mengine muombe Mungu.
Mungu anaombwa na wengi ...mpaka foleni yake ya maombi kumfikia Mungu anaweza kuwa ameshadanja.....
 
Hivi bro.. ukiona mtu mzima anatoa machozi usifikiri masihala, je unajua huyu jamaa alikuwa akipokea mshahara wa shilingi ngapi? je unajua ana watoto na wategemezi wangapi? umemsikia akisema alitegemea hela hii ya mkupuo anunue ka-shamba na kuanza kulima, kwa hiyo inawezekana hana nyumba hata kasehemu ka kujihifadhi.....je hako kaposho ka asilimia ngapi sijui ya average ya mishahara yake ya nyuma kila mwezi katatosha. kumbuka hata hako ka 10 millioni anasema kuna msururu wa wadai wanakasubilia na kenyewe.


Hata hivyo pia hiyo 55m angeipata ilikuwa ni big risk kuingiza kwenye kilimo unless ni kuongezea mtaji sio ndo aanze na biashara ya kilimo baada ya kustaafu

Pesa ya kustaafu haitakiwi iwekweze kwenye yafuatayo hasa ikiwa ndio pia unaitegemea kukupa mkate wa kila siku

1 kuanza nayo biashara unless tayar una biashara iliosimama unaongezea mtaji

2. Kilimo

Hiyo kumi achukue nusu iwekwe kwenye biashara ya. Mobile money angekuwa amepata yote ningemshauri anunue nyumba za uswahilini azikarabati apangishe pia awekeze kwenye mobile money

Uswazi nyumba ya 5m had 15m unakarabati inakupa wapangaji utapata had laki na nusu kwa mwez au laki 2 inategemea na quality na eneo
 
Back
Top Bottom