Unachanganya madesa na unapotosha ,huo unabii wa ufunuo 12 umetafsiri kwa akili yako ,biblia inajitafsiri yenyewe
Ufunuo 12:1 “Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili.”
Mwanamke: katika unabii hutumika kuwakilisha “kanisa”, na kanisa la kweli linawakilishwa na mwanamke ambaye ni bibi arusi, ambaye ni bikira safi, na amevikwa jua, mwezi, na taji ya nyota kumi na mbili. Wakati kanisa la uongo linawakilishwa na mwanamke ambaye ni kahaba na mwasherati. Paulo anaandika: “Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi.” (2 Wakorinto 11:2). Alikuwa akiwafundisha Injili ya kweli ili wasipokee uongo na kujichafua wenyewe, bali wakae katika kweli; maana kanisa ni msingi wa kweli (angalia 1 Timotheo 3:15), na hatimaye waweze kuwa kanisa la kweli ambalo ni bikira na liko safi bila doa wala waa lolote (Waefeso 5:27). Katika Ufunuo 14:4 tunaambiwa kwamba: “Hawa ndio wasiotiwa unajisi pamoja na wanawake [makanisa], kwa maana ni bikira. Hawa ndio wamfuatao Mwana-Kondoo kila aendako. Hawa wamenunuliwa katika wanadamu, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo.” Sababu kwanini ni bikira na wasafi ni kwa kuwa waliifuata kweli ya Kristo wakatakasika (Yohana 17:17), na walikataa kukubali mafundisho ya uongo yaliyotungwa na shetani katika makanisa makahaba yanayoungana na dunia ili kufanya uzinzi. Na siku ya kukamilika kwa ukombozi wote tunaona wanaitwa kama “mke wa Yesu” au “bibi arusi wa Yesu”, ikimaanisha kuwa walimtii Kristo na kukataa kufanya uasherati kwa kumtii shetani.