Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sema kweli!!!?Bikra Maria alipalizwa mbinguni akiwa mzima bila kufa.
Kule kana walimtumia akiwa hai. Sasa hivi wanamtumiaje wakati tayari ameishakufa mkuu?Katika harusi ya Kana, waalikwa walivyoishiwa na mvinyo, hawakwenda kwa Yesu moja kwa moja bali walipitia kwa bikira Maria, mama mtu. Kwa hiyo, wakatoliki wameiga kilichofanyika siku ile maana walifanikiwa kwa Yesu kubadili maji kuwa divai bora zaidi.
Kwa hiyo kupaishwa mbinguni kwa Eliya na Musa na bikra Maria (kama inavyodhabiwa), moja kwa moja waumini wanaweza kupitishia maombi yao kwa watu hawa badala ya kumuomba Yesu moja kwa moja mkuu?Wazee mbona hamsomi maandiko , mtatapeliwa sana na kina mwamposa kwa mtindo huu ,
Musa na Eliya hawakuwa wafu, Eliya alipaa mbinguni anawakilisha ambao hawataonja mauti, Musa ALIKUFA ,baadae akaja kufufuliwa na malaika ,anawakilisha watakaokufa na kufufuliwa
Ushahidi wa maandiko
Biblia inaonyesha kwamba Eliya hakufa bali alichukuliwa mbinguni akiwa hai. Hili liko wazi katika:
2 Wafalme 2:11
Hii inaonyesha kwamba Eliya hakuonja mauti, bali alichukuliwa moja kwa moja na Mungu.
Musa Alikufa na Akafufuka - Maandiko Husika
Biblia inasema wazi kwamba Musa alikufa, lakini kuna ushahidi wa kihisia kwamba alifufuliwa, na hili linatokana na tafsiri ya baadhi ya maandiko:
Kifo cha Musa:
Kumbukumbu la Torati 34:5-6
Musa Akifufuka (Hili linafahamika kupitia Yuda 1:9):
Yuda 1:9
Hakuna maandiko yanayosema mariamu alipaishwaKwa hiyo kupaishwa mbinguni kwa Eliya na Musa na bikra Maria (kama inavyodhabiwa), moja kwa moja waumini wanaweza kupitishia maombi yao kwa watu hawa badala ya kumuomba Yesu moja kwa moja mkuu?
Hapo ndio kunashida ya dini hii,ukianza kuhoji unaonekana we ni mpotevu.Kwa hiyo mkuu hapa inabidi tuamini tu bila kuhoji kama vile wapagani wanavyoamini tunguli za sangoma?
Sawa mkuu. Sasa naanza kupata mwanga kwamba maombi ya wakatoliki kupitia kwa bikra Maria ni ya kudhania tu.Hakuna maandiko yanayosema mariamu alipaishwa
Pia maandiko yanasisitiza hakuna jina WALILOPEWA WANADAMU ISIPOKUWA JINA LA YESU Tu
Wanatumia mapokeo ya WANADAMUSawa mkuu. Sasa naanza kupata mwanga kwamba maombi ya wakatoliki kupitia kwa bikra Maria ni ya kudhania tu.
Siku zote nimekuwa nikiwasikia wakatoliki katika sara zao wakimuomba bikra Maria, mama yake Yesu, awaombee. Hata katika nyimbo nyingi wanazotunga, wanamtaja bikra Maria na kumsihi awaombee kwa Yesu. Je, kwani huyu mama bado yu hai? Je, imani ya dini yao haihuruhusu muumini kumuomba Yesu moja kwa moja bila kupitia kwa mama yake?
View: https://www.youtube.com/watch?v=V9C1rqOJfxc
Hili ni swali ambalo nimekuwa nikijiuliza kwa muda mrefu bila majibu lakini nikaona leo nilete hili swali mbele ya wanazuoni wa masuala ya dini mliojaa hapa JF mnisaidie kutegua hiki kitendawili. Mtu yeyote anayefahamu hili suala kinagaubaga naomba anifahamishe nipate kuelewa.
Kwa uelewa wangu mdogo, nafahamu kuwa mtu pekee aliyekufa na kufufuka ni Yesu tu. Sasa huyu bikra Maria ina maana yeye hakufa? Kama bado yu hai yupo wapi? Tunaambiwa Yesu baada ya kufufuka alipaa mbinguni na ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Je, Maria yeye yu wapi? Au yeye ndiye ameketi mkono wa kushoto?
Maswali ni mengi lakini kwa kuwa humu JF kuna watu wenye uelewa mkubwa wa masuala ya dini, wakiwemo mapdre na maaskofu wa kanisa Katoliki mliomo humu, naomba mnifafanulie kuhusu hili jambo nipate kufunguka macho.
Asanteni sana.
Unaona jinsi mnavyosoma Biblia kama hadithi! Hivi hujawahi kuona msitari ambao Yesu anaagiza chochote tutakachomwomba baba yake kupitia yeye tutakipata? Kazi kweli kweli!Una swali la msingi na mimi naomba kuuliza kwa kujazia nyama,
Kwani wakristo hawawezi kumuomba Muumba wao (Baba yake Yesu) moja kwa moja bila kupitia kwa Yesu kama alivyosema Yesu wamwabudu baba yake tu?
Yohana 4:23
Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.
Yohana 17:3
Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma(mtume).
1korintho 15:28
Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe (Yesu) naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote.
Akiweka kifungu mnitagHebu tupe kifungu kwenye biblia mkuu.