Wakatoliki: Bikra Maria utuombee kwa mwanao Yesu. Je, bado yu hai?

Sanaaaa..... Inakuhusu nini...... Wewe si una Imani yako Baki nayo ikuponye ...waache wakatoliki na Imani Yao wapotee shida yako nini.... Au unataka Mudi akubusu kama alivyombusu swahaba wake.
Sisi tunaomba ufafanuzi tu mkuu. Kama huna jibu unaona ugumu gani kusubiri wenyewe waje kutufahamisha?
 
Iko hivi aliyekuwa anaabudiwa na ulimwengu wote wachache kwakujua ila wengi kwa kutokujua ni Mungu mke au malkia wa mbinguni,

Yeremia 44:17
Lakini tulipoacha kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, tumepungukiwa na vitu vyote; na kuangamizwa kwa upanga, na kwa njaa.

Matendo 19:27
Si kwamba kazi hii yetu ina hatari ya kudharauliwa tu; bali na hekalu la mungu mke aliye mkuu, Artemi, kuhesabiwa si kitu, na kuondolewa utukufu wake, ambaye Asia yote pia na walimwengu wote humwabudu.

Na ndo huyo pia ameandikwa katika ufunuo 12:1-9,hapa kuna miduara mitatu iliyokuwa itawala ulimwengu ya kwanza ndo huyo Mungu mke mataifa waliokuwa wanamuabudu walimuita Mungu na wapili ni joka na kuna mataifa ndo mungu wao na wengine wakaita dragon au dagon na wanasikukuu yake wanapitisha nyoka mitaani,

Mduara wa tatu ni vita kuna mataifa ndo Mungu wao kwao vita ni ibada.
 
Unachanganya madesa na unapotosha ,huo unabii wa ufunuo 12 umetafsiri kwa akili yako ,biblia inajitafsiri yenyewe

Ufunuo 12:1 “Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili.”
Mwanamke: katika unabii hutumika kuwakilisha “kanisa”, na kanisa la kweli linawakilishwa na mwanamke ambaye ni bibi arusi, ambaye ni bikira safi, na amevikwa jua, mwezi, na taji ya nyota kumi na mbili. Wakati kanisa la uongo linawakilishwa na mwanamke ambaye ni kahaba na mwasherati. Paulo anaandika: “Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi.” (2 Wakorinto 11:2). Alikuwa akiwafundisha Injili ya kweli ili wasipokee uongo na kujichafua wenyewe, bali wakae katika kweli; maana kanisa ni msingi wa kweli (angalia 1 Timotheo 3:15), na hatimaye waweze kuwa kanisa la kweli ambalo ni bikira na liko safi bila doa wala waa lolote (Waefeso 5:27). Katika Ufunuo 14:4 tunaambiwa kwamba: “Hawa ndio wasiotiwa unajisi pamoja na wanawake [makanisa], kwa maana ni bikira. Hawa ndio wamfuatao Mwana-Kondoo kila aendako. Hawa wamenunuliwa katika wanadamu, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo.” Sababu kwanini ni bikira na wasafi ni kwa kuwa waliifuata kweli ya Kristo wakatakasika (Yohana 17:17), na walikataa kukubali mafundisho ya uongo yaliyotungwa na shetani katika makanisa makahaba yanayoungana na dunia ili kufanya uzinzi. Na siku ya kukamilika kwa ukombozi wote tunaona wanaitwa kama “mke wa Yesu” au “bibi arusi wa Yesu”, ikimaanisha kuwa walimtii Kristo na kukataa kufanya uasherati kwa kumtii shetani.
 
Mkuu umemaliza kila kitu. Akikubishia nitag.
 
Kumbe hata nilichoandika hujakisoma, sasa unaniuliza nini?
Wewe uliandika hivi mkuu: Ujue kwamba Mungu alipenda kuukomboa ulimwengu kupitia kwa Maria, mama wa Yesu. Huu haukuwa mchezo wa kuigiza. It's the 'economy of salvation' (mpango wa Mungu wa kuwakomboa wanadamu).
2. Mungu hafungwi na muda. Kila jambo mbele ya Mungu linatenda sasa (Zaburi 90:4 na 2 Petro 3:8). Hakuna wakati uliopita au ujao.
3. Harusi ya Kana (Yohane 2:1-25) na pia Yesu alipobaki Jerusalem (Luka 2:41-52) na kutafuta na wazazi wake, 1) kule Kana waliokuwa harusini walimwendea Maria ili amwambie mwanae kwamba wsmeishiwa divai, na Maria akamwambia, na kisha akawaambia wale watu "atakachowaambia fanyeni". 2) Kule Jerusalem pia Maria na Yosefu walikuwa wakimtafuta Yesu, kisha wakamkuta hekaluni na mama yake akamuuliza "mbona umetufanya hivi...?" Katika masimulizi yote mawili Yesu alifuata au alitimiza aliyoambiwa na mama yake. Kanisa Katoliki linatambua umuhimu wa Maria katika maisha ya Yesu na katika ukombozi wa wanadamu. Haiwezekani Maria akabaki pembeni wakati Mungu mwenyewe alipenda kumshirikisha katika kumzaa Yesu na katika ukombozi wa wanadamu. Hivyo, Maria ana hadhi ya kuwa mama yetu kiroho/mama wa Kanisa na tunaweza kumwomba, kama walivyomwomba kwenye harusi ya Kana, amwambie mwanae kwamba wageni harusini wameishiwa divai na Yesu alitimiza alichoambiwa. Tunapomwomba Maria, tunamwomba atuombee kwa mwanae. Tunataka kuonyesha muunganiko uliopo/uhusiano ulioko kati ya yeye na mwanae na sisi pia. Kumbuka pale msalabani Yesu alimwambia Yohane (mmoja wa wale wanafunzi wake aliyempenda zaidi) "huyu ni mama yako" na kwa Maria "huyu ni mwanao" na kuanzia siku hiyo Maria alikwenda kukaa kwa Yohanne. Pia katika Luka 1:48 baada ya kujazwa na Roho Mtakatifu Maria alisema: "kuanzia sasa vizazi vyote vitaniita mbarikiwa/mwenyeheri."
4. Kwa hiyo, tukimwomba Maria (kama nilivyosema kwamba mbele ya Mungu kila kitu ni sasa) hakuna cha wakati uliopita, yote yanatendeka sasa. Na Yesu alisema "anayemwamini hata kama amekufa, ataishi milele" (Yohanne 11:25). Je, Maria alimwamini Yesu? Je, Maria anaishi? Ndiyo.


Ndipo nikakuuliza huyo Maria unayesema yu hai anaishi nchi gani?

Sasa nionyeshe kwenye hilo andiko lako reeeefu ni wapi umetaja kuhusu alipo bikra Maria unayesema ANAISHI. Anaishi wapi?
 
Bisha ubishavyo ila ndivyo ilivyokuwa.
 
Shida yako ni kumwomba Maria au kutaka kujua anaishi nchi gani? Maana naweza kuwa najibu swali ambalo hujaniuliza.
 
Watu walioandika biblia kuna makosa mengi sana ya kiufundi walifanya.

Mfano: Huwezi kusema Mungu ni roho, halafu wakati huo huo ana MKONO WA KUUME na wa kushoto. Huo mkono unatokea wapi tena? Roho zina mikono?
Hii ni kushindwa kuelewa literal na figurative translations. Kazi kweli kweli
 
Kama sio Mkatoliki hata ukieleweshwa utaelewa?
 
Hapa tunadanganyana. Bikra Maria. Alikuwa mwanadamu kama mwanadamu mwingine tu.
 
Yesu hakuwahi sema maombi kwenda kwake yapitie sehemu nyingine. Hakuwahi. Na utaona hata kuna sehemu alisema mama na ndugu zake ni wale wanaosikiliza na kufuata neno la Mungu. Bikra Maria tuna mheshimu kama mama ambaye alipitishiwa Yesu kisha kazi yake ikaisha hapo. Alibaki kuwa mama wa Yesu tu binadamu kama binadamu mwingine.
 
Cha msingi tuoneshwe kaburi lake tulifukue tuone kama hajaoza kweli?
 
Sielewi ugunu Huwa unatoka wapi Kwa Hawa wenzetu kuelewa hili
 
Yote uliyosema sio sababu ya watu kutokuhoji ili kuujua ukweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…