Yaan kwamba hamsomi kabisa kabisa maandiko ?.
Mwanadamu Dunia amepewa jina Moja tu la kuombea chochote , nalo ni JINA LA YESU.
Unajiuliza , MTU aliyekufa, Kisha nyinyi wenyewe mliohai mkamuita "Mtakatifu", huyohuyo mnamuomba awaombee Kwa Mungu?.
Mbona ni wazi na suala la akili ndogo tu na huhitajiki kua na Uelewa mkubwa wa masuala ya kiroho ndo ujue kua Mfu Hana lolote alijualo Wala kulisikia wala Hana mawasiliano yoyote yale na Mungu .
Ukiristo wenu ni wa aina gan?
Fransisko wa Asizi (kwa
Kiitalia Francesco d'Assisi; tangu
utotoni jina la
ubatizo Giovanni, yaani Yohane (Mbatizaji), liliachwa kutumika; pia
ubini mwana wa Petro Bernardone ulikuja kuachwa baada ya wao kushindana;
Assisi,
Italia,
1181 au
1182 - Assisi,
3 Oktoba 1226) alikuwa
mtawa shemasi wa
Kanisa Katoliki.
Baada ya kuishi
ujana wenye raha,
aliongokea maisha ya
Kiinjili ili kumtumikia
Yesu Kristo aliyekutana naye hasa katika watu
maskini na walalahoi, akijifanya
fukara vilevile, na hatimaye alitaka kufa uchi ardhini.
Akizungukazunguka huko na huko, hadi
Nchi takatifu, aliwahubiria watu wa kila aina
upendo wa
Mungu akilenga kuiga kikamilifu kila
siku mfano wa Yesu kwa maneno na matendo
[1].
Alianzisha jumuiya ya
kitawa yenye
matawi mbalimbali ambayo leo ni
utawa wenye wafuasi wengi kuliko yote wakikadiriwa kukaribia
milioni moja
duniani kote.
Alitangazwa na
Papa Gregori IX kuwa
mtakatifu tarehe 16 Julai 1228.
Anaheshimiwa na wengi hata nje ya
Kanisa lake, ambalo limemtangaza [msimamizi]] wa wanaoshughulikia
hifadhi ya mazingira.
Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe
4 Oktoba[2].
Maisha na karama yake
[
hariri |
hariri chanzo]
Ulaya na Kanisa mwishoni mwa karne XII
[
hariri |
hariri chanzo]
Fransisko alipozaliwa,
Ulaya na
Kanisa vilikuwa na hali ya kutatanisha kuliko kawaida, kutokana na mvutano kati ya mapya na ya kale.
Mambo ya kale ni yale ya utawala wa ngazi mbalimbali ulioenea kutoka
Ufaransa kuanzia
karne IX: kila mtawala aliweza kugawa eneo lake na kuwakabidhi watawala wa chini akiwadai sehemu ya mapato na hasa msaada wakati wa vita, kufuatana na ahadi yao ya kuwa waaminifu kwake moja kwa moja. Utawala huo ulikuwa ukirithiwa na watoto ambao waliheshimiwa kama masharifu yaani watu wa ukoo bora na kutakiwa wawe hodari vitani. Ili watawale vizuri na kulinda maeneo yao walikuwa wakiishi katika
ngome pamoja na watumishi wao. Watu wa kawaida waliishi mashambani katika hali ngumu sana hata wakaitwa watumwa wa ardhi. Hivyo Ulaya ilikuwa na
askari na
wakulima tu, mbali ya viongozi wa Kanisa na
watawa.
Kwa hali ya maisha watawa, ambao walikuwa aina ya
wamonaki tu, na
makleri wa juu walilingana na masharifu, ila makleri wa chini hawakuwa na
elimu wala
mali nyingi. Utajiri wa Kanisa, ambalo lilifikia kumiliki karibu nusu ya ardhi ya Ulaya nzima, uliwapotosha wengi na kuvuta miito ya bandia. Wengi walitambua haja ya
urekebisho ndani ya Kanisa, na juhudi za pekee zilifanywa na wamonaki kama vile Hildebrando (ambaye akawa
Papa Gregori VII) na Mt.
Petro Damiani katika
karne XI, halafu na Mt.
Bernardo wa Clairvaux katika
karne XII akihimiza kupambana na maovu ya viongozi wa Kanisa hata kwa kutohudhuria
ibada za wale wanaoishi vibaya. Jitihada hizo zilifanikiwa kidogo tu, kwa sababu ni vigumu kurekebisha mitindo mibaya iliyoenea, hasa katika mazingira ya
dini.
Hali hiyo ilichangia uenezi wa
Waislamu na hasa wa
Wakatari (maana yake Watu Safi); wazushi hao, baada ya kupata wafuasi kwa kushambulia maovu ya viongozi wa Kanisa, walikuwa wakifundisha njia ya roho zao kukombolewa. Kwa kuwa eti, ulimwengu huu ni mbaya, si kazi ya
Mungu wetu, ni lazima kujitenga nao kwa kukataa vitendo na vyakula vinavyohusika na
uzazi. Viongozi wa Kanisa walichelewa kuona hatari hizo, mpaka zilipokwishaenea mno: ndipo walipoanza kuzikabili hata kwa
silaha wakishirikiana na baadhi ya watawala. Hata hivyo
uzushi ukaendelea kustawi, kwa kuwa wengi walipenda maisha magumu ya watu hao kuliko yale ya viongozi wa Kanisa; hivyo waliwasaidia wasikamatwe.
Uzushi wa aina nyingine ulianza muda mfupi baadaye (karne XI hiyohiyo) huko
Lyon (Ufaransa Kusini). Mchochezi wake ni
Valdo, ambaye alikuwa mfanyabiashara, akaguswa na
Injili, akawapeleka mabinti wake kuishi
monasterini, akauza mali zake, akawagawia
maskini, akaanza kuhubiri huko na huko kama walivyofanya wengine kabla yake wakisisitiza
ufukara kama njia bora ya
wokovu. Wengi waliguswa wakajitahidi kushika masharti ya Injili, hata baadhi yao wakaanza kuwashambulia makleri wabaya, kususia ibada zao na kuwapiga pia. Msimamo huo ulipingwa vikali kama
kiburi na
unafiki. Basi Valdo na wengine walipokatazwa na maaskofu wasihubiri tena wakafikia hatua ya kuwakataa.
Huko Italia Kaskazini walitokea wengine wakisisitiza kazi kuliko ufukara (
Mafukara wa Lombardia na
Wahumiliati, maana yake Walionyenyekea) ambao walikuwa wote watengenezaji wa vitambaa duni vya
sufu kwa ajili ya maskini na ambao walichanga mali na mapato wakiishi kishirika.
Mifumo hiyo yote ilionyesha uhai wa dini, na juhudi za
walei wengi kwa urekebisho wa Kanisa. Jambo hilo jipya lilitokana na udhaifu wa makleri, pia na umbali wa wamonaki na maisha ya
umati. Wamonaki pia walianza kushambuliwa kwa kufuata ufukara bandia na kula
jasho la wengine, tena kwa kutoshughulikia
uchungaji. Hivyo walei wakaaanza kujiongoza hata katika mambo ya kiroho.
Msingi wa matukio hayo ni miji kupanuka haraka sana. Baada ya
mwaka 1000, kitovu cha Ulaya si tena vijijini na mashambani. Waliomiminika mijini walianza kukataa utawala wa ngazi wa zamani na kujichagulia viongozi ambao wadumu muda fulani tu,
demokrasi ikaenea. Miji hiyo huru ikaanza kuvamia maeneo ya jirani ili kuyatawala, ukaweka watawala wa zamani chini yake. Mijini utengano wa
matabaka matatu ya zamani ukawa unapungua: watu wadogo waliojiimarisha ki
uchumi (hasa waliofanya
biashara ya
bidhaa kutoka nchi za mbali) wakazidi kupata nguvu hata kulingana na ma
sharifu. Pamoja na utajiri watu hao walipaswa kujipatia elimu walau kidogo (ndio mwanzo wa kazi ya walimu wa watoto), hata wakatamani walingane kabisa na masharifu kwa kuiga mitindo yao ya Cortesia (maana yake
Ustaarabu) ambayo ilidai kumheshimu
mwanamke fulani kama mtawala wa binafsi, na kwa ajili ya huyo kujifanya wakarimu, wapendevu, wachangamfu, na kutunga nyimbo na mashairi. Mitindo hiyo ilienea kutoka ngome za masharifu hadi
barabara na vichochoro vya mijini, ambapo vikosi vya wavulana vilikuwa vikiwaimbia wasichana.

Makazi ya Fransisko alipokuwa mdogo.
Asizi katika karne XII
[
hariri |
hariri chanzo]
Kwa asili Asizi ni
mji wa Kirumi ambao ulipata umuhimu kwa sababu unatawala barabara kuu ya mkoa wa Umbria kutoka
Spoleto (makao ya mfalme mdogo aliyekuwa chini ya mfalme mkuu wa
Ujerumani) hadi Perugia mji uliokuwa chini ya utawala wa
Papa. Wakati huo kulikuwa na ushindani mkubwa kati ya Asizi uliokuwa chini ya mfalme mkuu na jirani yake Perugia uliosimama upande wa Papa.
Mbali ya hayo ndani ya mji wenyewe yalianza mapigano kati ya mayores (wakubwa, yaani masharifu) na minores (wadogo) yaliyosababisha masharifu wengi kukimbilia Perugia na hivyo kuzidisha
chuki kati ya miji hiyo. Matokeo yake ni mapambano ya mwaka
1202 ambayo Fransisko pia aliyashiriki akashikwa mateka kwa mwaka mzima.
Mbali ya hao watu wadogo waliotajirika (hasa kwa biashara), Asizi ulikuwa na mafukara, lakini tofauti na wale wa zamani (
watumwa wa ardhi) ambao pamoja na kuwa na maisha magumu hawakukosa
chakula (pia kutokana na
mshikamano wao). Kumbe ufukara wa mijini haukuwa na dawa, uwe umetokana na kukosa
kazi au kulipwa kidogo au kuugua. Ngazi ya mwisho ilikuwa ya watu waliotengwa na jamaa kama vile wakoma.
Ili tuelewe mazingira hayo ni lazima tukumbuke kwamba “sifa ya kijamii” (yaani jinsi mtu au neno wanavyotazamwa na
jamii yote) ilikuwa na nguvu sana hata kuwabana wote waseme na kutenda ilivyotarajiwa. Hata hivyo mtu aliweza pia kuchangia au kubadilisha mitazamo ya umati, na Fransisko anajulikana kwa kipawa cha kuelewa, kugusa na kujivutia jamii nzima.
Mfanyabiashara
[
hariri |
hariri chanzo]
Maandishi yote yanayomhusu yanasisitiza utajiri mkubwa aliozaliwa nao. Hatuwezi kumuelewa tusipozingatia sana jambo hilo lililomfanya alelewe namna ambayo inatokana na utajiri, inasisitiza umuhimu wa utajiri na kulenga ongezeko la utajiri. Baba yake hakuwa na
kiwanda, ila aliweza kutajirika ajabu kwa kusafirisha vitambaa vya thamani kutoka
Ufaransa. Ingawa hatuna habari nyingi za hakika kuhusu wazazi na
malezi yake, hiyo inaweza kutosha.
Mwaka wake wa kuzaliwa umehesabiwa kuanzia tarehe ya kufa, kwa kupunguza miaka iliyosemekana aliishi. Habari nyingine kuhusu kuzaliwa kwake ziliweza zikatungwa ili kumfananisha na Kristo. Jina lake la
ubatizo Yohane lilibadilishwa na baba yake ili kukumbusha moja kwa moja nchi ya Ufaransa, asili ya utajiri wake (Fransisko = Mfaransa).
Elimu yake ilikuwa ya wastani: alijua kidogo
Kilatini,
Kifaransa, mashairi na
Biblia. Malezi yake yalimfanya hodari hasa katika
biashara ili aweze kuendesha shughuli zote za baba yake. Na kweli kabla hajaongoka aliiweza sana kazi hiyo. Kama kawaida ya zamani zile, akiwa na umri wa miaka 20 alianza kuhesabiwa mtu mzima na kujihusisha na
siasa na
vita pia ili kushika nafasi ya juu zaidi kama
sharifu. Ndicho kipeo alichojiwekea. Unakumbukwa
ukarimu wake kwa
maskini, lakini hata ukarimu huo aliuzingatia ili kutimiza wajibu wa
ustaarabu kuliko kwa kumpendeza
Mungu. Kwa lengo hilohilo la kujitafutia usharifu akawa
askari, na akiwa kifungoni Perugia akazidi kuwachangamkia wote, hata sharifu fulani mkorofi. Kuhusu hali iliyotangulia
uongofu wake hatujui zaidi, ila mwenyewe aliona kwamba kuishi kwa kufuata mitindo ya
ulimwengu kunamchukiza Mungu.
Uongofu
[
hariri |
hariri chanzo]
Giotto,
Fransisko anavua hadharani, Basilika la juu la Asizi
Jinsi gani
neema ya Mungu ilileta ndani ya mtu huyo mapinduzi yanayotushangaza hata leo? Hatujui vizuri mabadiliko hayo yalichukua muda gani, wala asili yake ni nini, ila kwamba Fransisko alianza kuguswa na
huruma halisi kwa maskini. Mwenyewe alipousimulia uongofu wake katika
wasia alisisitiza hatua ya kushinda
hofu ya wakoma aliyokuwa nayo sana. Basi baada ya kumbusu mmojawao, alichagua kuwa nao badala ya kuwa sharifu, yaani ashuke badala ya kupanda
daraja katika jamii. Baada ya uteuzi huo akasita bado kidogo kabla hajaacha ulimwengu na kujitoa kwa Mungu. Kutokana na hatua hiyo muhimu alianza kufurahia machungu badala ya matamu: ndiyo maisha ya
toba (
utawa).
Alipotambua kwamba
ukoma wa roho yake ulitisha kuliko ule wa ngozi ya wagonjwa alianza kuwakaribia kwa
upendo si tu kwa kuwagawia
mali, bali hata kwa kuhatarisha
afya yake: akiwa tayari kuambukizwa nao alikuwa pia tayari kutengwa na jamii moja kwa moja kama vile hao. Hivyo kwake neno kuu halikuwa ufukara kama juhudi za kujinyima, bali kama kushiriki kabisa hali ya watu wa mwisho, kwa kuwa hao ni wenzetu kwelikweli na kielelezo cha Kristo. Baadaye,
Utawa wa Ndugu Wadogo ulipoimarika kwa kupata miundo ya
shirika, ulisisitizwa ufukara wenyewe, kiasi kwamba kanuni ya kudumu haitaji wakoma wala
huduma kwa maskini. Basi, kwa wasia wake Mt. Fransisko kabla hajafa alisisitiza tena
karama halisi ya uongofu wake pamoja na mengine yaliyoanza kusahaulika, kama vile
kazi za mikono.
Jambo la kwanza linaloonyesha wazi neema ya Mungu ikimfanyia kazi ni ile
ndoto iliyomrudisha nyumbani wakati wa kwenda vitani akiwa na miaka 23. Tangu hapo hakuweza kuridhika tena na maisha ya zamani, akawa anafuata mawazo yake mapya badala ya kupiga kelele na wenzake baada ya kuwagharimia
karamu kama mfalme wao. Alijaribu kuishi pangoni na kusali tu, akishinda vishawishi vikali vya kiroho. Siku moja katika kanisa la Mt. Damiano akasikia sauti ya Msulubiwa ikimuagiza arekebishe
Kanisa lake. Ingawa alielewa maneno hayo kama kwamba yanahusu jengo, muhimu ni kwamba akawa amekutana na Msulubiwa ambaye
mateso yake yanajumlisha na kuyatia maana mateso yote ya
binadamu. Kuanzia hapo akaambatana na
Yesu moja kwa moja katika ukweli wa maisha yake duniani: ndivyo unavyoeleweka ugumu wote wa maisha ya Fransisko.
Matendo yake yakazidi kumchukiza baba yake aliyeweza kuvumilia
ubadhirifu wake ulipolenga usharifu, lakini si uliposaidia maskini tu. Hivyo baba akamshtaki
mahakamani, akimpatia hatimaye nafasi ya kujitambulisha mbele ya wote kama askari wa Kristo moja kwa moja: ni kwa sababu alikataa kuhukumiwa na serikali kwa kujidai ni mtumishi wa Mungu, na hivyo ni mtu anayeweza kuhukumiwa na
Askofu tu. Baba alipodai mali zake mbele ya huyo, Fransisko akakubali mara moja akimrudishia pamoja na
pesa,
nguo zote na hata jina, akitamka
hadhara ya watu kwamba kuanzia hapo atamuita Baba Mungu tu, si
Petro Bernardone tena. Uamuzi huo wa kishujaa uliowagusa sana wote ulimfanya asiweze kurudi nyuma: amejitoa kwa Mungu moja kwa moja na kuacha hakika ya
riziki. Kubaki
uchi mbele ya wote kulikuwa na maana nyingine pia, kwa sababu kulikuwa ni
malipizi ya hadharani yaliyoweza kutolewa na Kanisa kadiri ya
sheria. Hivyo Fransisko alionyesha nia yake ya kuanza na moja, akitubu
anasa za zamani alizozifuata kwa nguo maridadi. Tena wakati huo lilizingatiwa sana neno la Mt.
Jeromu la “kumfuata uchi Kristo uchi” kuwa ndiyo namna bora ya toba. Basi, kuanzia hapo alishiriki kabisa hali ya wasio na kitu, akisikitikia tu kutozaliwa katika hali hiyo, maana yake ufukara wake ulikuwa wa
hiari na wenye kustahili, hivyo ni utajiri fulani kwa Mungu.
Kufuata mtindo wa Injili
[
hariri |
hariri chanzo]
Porsyunkula huko Asizi
Baada ya Fransisko kujitangaza
mtawa ilimbidi atambue atakuwa wa namna gani. Alikataa
upadri, lakini si kwa sababu ya kuudharau kama walivyofanya wazushi; kinyume chake, toka mwanzo alijaliwa
imani ya pekee kwa
ekaristi na kwa wanaohusika nayo. Aliuona upadri kuwa ni cheo kikubwa mbele ya Mungu na hata mbele ya watu, naye hakupenda kuheshimiwa wala kuwa na hakika kuhusu riziki. Kwa sababu hiyohiyo hakupenda kuwa
mmonaki, ingawa aliwaheshimu
Wabenedikto na kushirikiana nao vizuri. Tena akitaka kuwa kweli mtu wa mwisho na kuwaheshimu wote, hakukubali kushambulia mapadri na wamonaki kwa maovu yao.
Baada ya kukataa hali hizo mbili ndani ya Kanisa, alianza kujitafutia maisha asiyoyajua bado na asiyoweza kuelekezwa na mtu yeyote. Basi, akavaa
kanzu ya
mkaapweke, lakini alikuwa akirudi mjini kila siku ili kuombaomba mawe ya kutengenezea makanisa na chakula pia. Kwa hiyo hakusogea mbali na watu, bali alizidi kuhusika na maisha ya Asizi, ingawa kwa namna yake, akipokea hasa
dharau alivyokusudia. Maisha yake yote hakuvunja uhusiano na jamii kama walivyofanya watawa wengi, bali akaendelea kuwa
ndugu wa wote na kushiriki maisha yao ya kila siku.
Miaka miwili aliyotumia kuyarekebisha makanisa ilikuwa migumu sana kimwili na kiroho tukizingatia pia mahangaiko yake kuhusu
wito. Lakini Mungu akapokea malipizi na
sala yake akamuangazia sehemu ya
Injili aliyoisikia wakati wa
Misa. Enzi hizo
walei wengi walivutiwa na maneno ya Injili ambayo waliyaelewa namna yao, bila ya ufafanuzi wa kitaalamu. Fransisko alifanya vilevile, ndiyo maana maisha yake yakaja kuwapendeza wengi na kuenea kasi ajabu. Dondoo ambalo lilimgusa na kumuangaza hasa ni lile la Yesu kuwatuma
mitume wake kwa mara ya kwanza. Tangu hapo alikusudia kufuata Injili hiyo, hata ufukara wake ukapata sura nyingine, yenye kulenga utume. Kutokana na mwanga huo akabadili kanzu yake na kutupa
viatu vyake na kujifungia
kamba, ambayo ilikuwa
ishara ya toba, tena haikuweza kuficha pesa (tofauti na
mshipi wa ngozi). Halafu akaanza kuhubiri toba kwa
unyofu uliowagusa wengi. Ndipo Waasizi walipoanza kumuelewa si
kichaa, na ndipo alipoanza kupata wafuasi. Wa kwanza alikuwa
Bernardo wa Quintavalle, mtu maarufu tena tajiri, wa pili
Petro Cattani, padri. Ndio mwanzo wa jamaa iliyokuja kumhangaisha sana, kwa sababu hakuwa na wazo la kuanzisha chochote wala hakupata mtu wa kumuelekeza. Tena wakati huo haikuwa rahisi kukubali padri aongozwe na
mlei.
Katika wasia wake Fransisko akikumbuka hatua hiyo muhimu alisisitiza kuwa ndipo Mungu mwenyewe alipomfunulia afuate mtindo wa Injili takatifu, yaani hasa madondoo yale aliyoyakuta katika kufungua mara tatu kitabu cha Misa kilichokuwa juu ya altare: 1) “Ukitaka kuwa mkamilifu, nenda ukauze…” 2) “Msichukue chochote kwa safari…” 3) “Anayetaka kunifuata, ajikane…” Baada ya kusoma hayo, aliwaambia wenzake ndiyo kanuni na maisha ya wale wote watakaowafuata. Ufukara wa Kifransisko ukifuata madondoo hayo ya Injili ni wa moja kwa moja kwa mtawa binafsi na kwa shirika zima. Kwa kuchagua mtindo huo wa Injili takatifu alitofautiana na watawa wale waliofuata tangu karne nyingi mtindo wa Kanisa la mwanzoni wa kuwa na mali zote shirika. Ndivyo walivyofanya wamonaki ambao hawakuwa na chochote chao binafsi, lakini
monasteri zao zilikuwa tajiri, kiasi kwamba wakaanza kushambuliwa kama wanafiki wanaokula
jasho la wengine na kukosa ufukara halisi.
Waamini wengi kama Bernardo na padri Petro walitamani mtindo mwingine, pamoja na
uadilifu wa makleri,
uchungaji wenye bidii na ujirani na watu, hasa wenye shida. Mungu aliwachagua watakatifu Fransisko na
Dominiko Guzman ili kuridhisha Wakristo hao. Wote wawili walishika ufukara wa kijumuia pia, ingawa Mt. Fransisko aliusisitiza zaidi akiudai pia kama msimamo katika jamii ili kupigania
ujamaa na
usawa wa binadamu. Hata baada ya wengine kujiunga naye hakushughulikia suala la
nyumba: waliishi kwenye
pagale za makanisa, huku wakizungumziwa sana mjini kwao. Halafu wakaanza kusafiri wakihubiri huko na huko, si kama kawaida ya mapadri, bali kwa kutoa mfano wa ufukara na
unyenyekevu, halafu kwa kujibu maswali ya watu waliowashangaa. Polepole waliweza pia kuhimiza toba na
msamaha ili kueneza
amani: muhtasari wa
mawaidha yao ni
salamu ile ambayo Fransisko alidai kufunuliwa na Mungu, “Bwana akujalie amani”.
Baada ya jaribio la kwanza la namna hiyo wakaongezeka, naye akawatuma tena wawiliwawili sehemu mbalimbali kisha kuwashirikisha
mang’amuzi yake, kwamba wasikate tamaa kwa kuona ugumu wa baadhi ya watu, wamtegemee Mungu, wahubiri toba kwa nguvu ili kuokoa watu, wadumu watulivu katika
dharau. Walipoulizwa waitwaje walijibu tu kuwa ni watu wa toba kutoka Asizi, yaani hawakujiona kuwa shirika maalumu, bali kundi mojawapo la wale wengi ambao toka zamani walijifunga kufanya toba kwa namna maalumu hadharani.
Mwaka huo
1209 walipofikia idadi ya 12 walichukua hatua ya kuelekea
Roma ili kuthibitishwa na Papa katika maisha yao na kuruhusiwa naye katika
utume wao, ili kushinda
upinzani uliojitokeza na hasa kujihakikishia njia yao ni njema. Kwa ajili hiyo walipaswa kupanga kikamilifu zaidi wanataka kufanya nini.
Kanuni ya awali
[
hariri |
hariri chanzo]
Kanzu iliyotumiwa na Fransisko mwaka
1215 hivi.
Kanuni hiyo ilihitajika ili kujipendekeza kwa Papa na kupata kibali chake. Fransisko katika
wasia akashuhudia kwamba aliandikisha “kwa maneno machache na kwa unyofu, naye bwana Papa akaniimarisha”. Leo hatuna tena kanuni hiyo kwa sababu iliendelea kurekebishwarekebishwa mpaka mwaka
1221 ilipotolewa kanuni ndefu ambayo tunayo, tena mpaka mwaka
1223 Papa alipothibitisha kwa maandishi toleo la kudumu linalofuatwa na Utawa wa Kwanza mpaka leo.
Ni kwamba miaka yote Fransisko alizidi kung’ang’ania azimio lake la kushika kikamilifu mtindo wa
Injili takatifu, lakini pia maisha yalimlazimisha kung’amua haja ya kuulinganisha na hali halisi mbalimbali. Ugumu mwingine wa kazi hiyo kwake ulitokana na kukosa utaalamu wa
sheria uliolitawala Kanisa la zamani zake kwa namna ya pekee. Hivyo hata alipomuachia mwingine uongozi akazidi kudai ndugu wamtii ingawa hana tena
mamlaka juu yao. Alitamani kuwa daima mtu wa mwisho hata shirikani, lakini hakuweza kuachana na wajibu wake kwa shirika lililoanza kwa njia yake. Hata katika safari ya kwenda Roma alimteua Bernardo kuwa kiongozi, lakini mbele ya Inosenti III aliyejitokeza ni Fransisko. Papa huyo alikuwa anakabiliana na matatizo mengi ya Kikanisa na ya kisiasa, lakini yeye, kwa kupitia ngazi mbalimbali (hasa
Askofu Guido wa Asizi na Kardinali
Yohane wa Mt. Paulo), alifaulu kuongea naye na kukubaliwa.
Viongozi hao walijitahidi kwanza kuelekeza mifumo mipya ya kiroho kwenye
umonaki, na pili iliposhindikana wakairuhusu mradi isifuate
uzushi bali ikubali kuongozwa na makleri kusudi isivuruge maisha ya Kanisa. Hivyo Mt. Fransisko na wenzake walipokataa kanuni za kitawa zilizokwishakubaliwa, wakaruhusiwa kwa sauti tu wafuate azimio lake na kuhubiri
toba.
Maisha ya Ndugu Wadogo huko Asizi
[
hariri |
hariri chanzo]
Kisha kurudi kwa furaha Asizi walibanana katika kibanda fulani huko
Rivotorto, halafu wakahamia Porsyunkula. Mahali penyewe panatusaidia sana kuelewa karama ya Kifransisko: si maisha ya kimonaki yanayohitaji kujitegemea kwa mashamba makubwa na
mifugo, wala ya
wakaapweke wanaohitaji kuishi mbali na watu, bali ni utawa unaohitaji
utulivu na upweke kwa ajili ya
sala, lakini pia unadai uhusiano mkubwa na watu wa nje ili kupata
riziki na hasa kuwajenga kwa mifano na maneno. Hivyo si kati ya watu, wala si mbali nao.
Mchana ndugu walikuwa wakienda mjini kufanya
kazi mbalimbali ndogondogo na kuwahimiza watu waishi kwa
uadilifu. Muda uliobaki, hasa
usiku, ulikuwa kwa ajili ya sala upwekeni. Maelezo mengine kuhusu maisha ya wakati huo tunayapata tena katika
wasia ambamo Fransisko ametuachia ukumbusho wa kudumu.
Jambo la kwanza ni
ufukara mkuu ambao uliwadai ndugu wote wawaachie
maskini mali zao. Hivyo jumuia haikuwa na kitu, ikaishi kwa shidashida pembeni mwa
jamii kama watu waliotupwa, wakiridhika na
kanzu moja tu, tena duni sana, wakiiongezea sanasana viraka ndani na nje ili kupunguza
baridi, halafu
kamba na
kaptura. Mavazi ya namna hiyo yalikusudiwa kudhihirisha hali ya chini ya ndugu wadogo katika Kanisa na jamii kwa hiyo yalitakiwa kusababisha
dharau, si
heshima.
Jambo la pili ni maisha ya sala, ambayo yalikuwa tofauti kwa ndugu
wakleri na kwa ma
bradha kutokana na
elimu yao: wa kwanza walijua
Kilatini,
lugha ya liturujia; wa pili kwa kawaida hawakujua hata kusoma. Hivyo Fransisko na wakleri wengine walitumia
Sala ya Kanisa, wakati mabradha walipangiwa kurudiarudia
Sala ya Bwana mara kadhaa. Kwa njia ya
liturujia Fransisko akazidi kupata
ujuzi wa kidini, ila aliendelea kuchukia jambo moja la elimu ya wakleri, yaani kwamba mara nyingi ujuzi wao waliutumia kuipotosha maana halisi ya maneno ya
sheria na hata ya ujumbe wa Mungu. Aliona kwamba elimu hiyo haitoshi kuwafanya watu watambue na kushika kama yeye uhusiano uliopo kati ya mateso ya walio wengi na yale ya Yesu. Ukweli huo unajulikana na watu wenye
upendo, si wenye elimu tu. Ndiyo sababu Fransisko katika
malezi hakusisitiza mafundisho na ujuzi kwa jumla, bali
mang’amuzi na mifano inayogusa mioyo.
Upande wao mabradha, kama vile katika mifumo mingine ya wakati huo, walitumia Sala ya Bwana ambayo kwao ilikuwa na uzito wa pekee, kutokana na jinsi Fransisko alivyoongoka kwa kumkataa mzazi wake na kumchagua Mungu tu kuwa baba yake: ndiye tegemeo pekee na ndiye anayewafanya watu wote kuwa ndugu.
Juu ya msingi huo wa
udugu, tofauti ya sala haikuleta
ubaguzi kazi ya wakleri na mabradha: wote walikuwa wakijiona wajinga na kujiweka chini ya yeyote, unavyosisitiza wasia baada ya kukumbuka namna yao ya kusali. Alipouandikisha ameshamruhusu Mt.
Antoni wa Padua awafundishe wanashirika mambo ya
dini, lakini anaendelea kuogopa elimu hiyo pia itawavimbisha na kuwasogeza mbali na
wito wao wa
udogo, kumbe
ujinga unaleta dharau aliyotamani daima.
Hivyo tena katika wasia akataja mara
kazi ya mikono, akieleza inavyowapasa wote, hata yeye mwenye
madonda ya Yesu! Katika kusisitiza kazi ndogondogo kama za mwanzoni alitoa sababu mbili: moja ni kufukuza
uvivu, kama ilivyofundishwa na
wamonaki toka zamani; lakini inayotajwa kwanza ni maalumu kwa kazi hizo za watu wadogo, yaani kutoa mfano mzuri kwa wanaowaona.
Wafransisko wa kwanza walifanya kazi hivyo, pasipo kulenga
malipo moja kwa moja. Ndiyo sababu mara nyingine hawakulipwa chochote kwa kazi waliyoifanya. Hapo wakaikimbilia “meza ya Bwana” kwa kuombaomba nyumbani kwa watu. Zamani hizo katika Kanisa ilieleweka wazi kuwa
fukara ana haki ya kuishi na kuwa Mungu anamkaribisha
chakula kwa njia ya watu wakarimu.
Hata hivyo daima kuombaomba kuna ugumu wake, hasa
aibu na dharau za watu. Lakini hizo zinachangia
ustawi wa
unyenyekevu na udogo kwa kuweka kweli katika ngazi ya mwisho ya jamii. Pamoja na malengo hayo, ni wazi kwamba kwa Fransisko njia ya kawaida ya kujipatia riziki ni kufanya kazi wenyewe, si kutegemea tu kazi ya wengine kama walivyotafsiri baadaye shirikani.
Jambo lingine la pekee ambalo Fransisko alilikumbuka katika wasia ni salamu ya
amani aliyofunuliwa na Bwana. Amani hiyo ilihitajika sana, hasa wakati huo wa vitavita, lakini yeye alilenga pia amani ya rohoni, yaani amani ya Kimungu inayoondoa
dhambi. Hivyo salamu yake ya Kiinjili ilikuwa kama
muhtasari wa mahubiri yake.
Baada ya kukumbusha hayo yote, wasia unasisitiza ufukara wa majengo (nyumba na vikanisa) ya wafuasi wake, pamoja na msimamo ambao wawe nao, yaani wa kuishi huko kama wageni na wasafiri tu, tayari kuondoka siku yoyote kama walivyofanya huko Rivotorto walipomuachia nafasi
punda wa
mkulima mkorofi.
Kwa msingi huohuo wa udogo wasia unaongeza katazo la kwamba watawa wasimkimbilie
Papa wala
ofisi zake ili kupewa
fadhili, yaani
idhini ya kutenda tofauti na watu wengine. Katazo hilo kali lilikusudiwa tena kulinda udogo wa jamaa yake. Fransisko toka mwanzo alijichagulia nafasi ya mwisho asipende kushindana wala kujilinda na mtu yeyote. Katika kufafanua katazo hilo alitamka wazi kuwa ndugu wadogo wasiombe fadhili hata kama ni kwa ajili ya kuhubiri. Aliutaka
utume, lakini hakupenda uharibu udogo: aliona ni afadhali kuacha utume sehemu fulani kuliko kuacha udogo.
Hivyo ni wazi tofauti iliyopo kati yake na
Mt. Dominiko.
Mwanzilishi huyo wa
Utawa wa Wahubiri alilenga uenezaji wa
ukweli, akatafuta njia za kufikia lengo hilo, yaani ubora wa mapadri wake kuhusu elimu na
utakatifu; kwake ufukara ulikusudiwa kuwafanya wahubiri wapokewe katika
mazingira yale tuliyoyaeleza. Ili kufikia lengo hilo alijipatia fadhili nyingi toka kwa Papa, uenezaji wa ukweli usije ukazuiwa na
mamlaka nyingine yoyote. Kumbe Fransisko alifanya tofauti, kadiri ya chaguo lake: alipotambua kuwa
Bwana amewaita yeye na wafuasi wake wakaokoe watu, alijitahidi kufanya hivyo lakini bila ya kuacha nafasi ya mwisho aliyojichagulia. Aliona si rahisi kubaki pembeni mwa jamii na mwa Kanisa (kama vile wakoma na wengineo), na papo hapo kujihusisha kikamilifu na maisha ya jamii (ili kuleta amani) na ya Kanisa (kama shirika kubwa ajabu), lakini kabla hajafa alisisitiza tena katika wasia chaguo la mwanzoni, ambalo ni la maana kwa
karne zote kwa vile daima watakuwepo watu wa mwisho wenye kudharauliwa.
Msanii wa Bwana
[
hariri |
hariri chanzo]
Hatuwezi kuelewa vizuri maisha hayo ya mwanzoni tusipozingatia jambo lake lingine ambalo ni la pekee katika
Kanisa la Magharibi, yaani tabia ya kupenda viigizo na kuchekesha watu ambayo ilichangia kwa kiasi kikubwa uenezi wa Ufransisko na mafanikio ya utume wake. Fransisko alikuwa mfurahivu si kwa
silika tu wala si kutokana na muungano wake na Mungu tu. Alipenda kufanya mambo ya ajabuajabu kwa makusudi mazima ili kuwashangaza watu na kuwafanya watafute majibu ya maswali yaliyojitokeza ndani mwao. Kwa maana hiyo alipenda kujiita “ioculator” (= mtu wa viigizo na vichekesho,
msanii) wa Bwana.
Zamani hizo “msanii” alikuwa mtu anayepata riziki kwa kuchekesha watu akitenda mambo ya ajabuajabu popote pale anapopita: tena haogopi kutoa ujumbe mzito katika vichekesho vyake, kwa kuwa amejiweka pembeni mwa jamii. Basi, Fransisko aliamua kuwa mtu wa namna hiyo kwa ajili ya Bwana, yaani kwa lengo la kuwavuta watu na kuwapasha ujumbe wa toba. Ndiyo njia yake ya kufanya utume.
Akiwa kwanza mfanyabiashara hodari alijua vizuri namna ya kuwavuta watu wanunue
bidhaa zake; baadaye akatumia
kipawa hicho ili watu wapokee ujumbe wake. Kwa namna za kuvaa na kutenda, pamoja na kuvumilia dharau, yeye na wenzake waliteka
roho za watu, hata walipoacha
utani na kuhimiza toba wakasikilizwa kuliko wahubiri wa kawaida makanisani. Hivyo walitangaza
Injili mitaani katika mazingira ya watu wa kawaida na kwa mitindo na
lugha vinavyotumika mitaani.
Basi, baada ya kumaliza kuikarabati Porsyunkula, walishughulika zaidi mjini wakitoa mfano wao na kuhimiza toba; halafu usiku hasa walikazania sala katika utulivu wa porini. Hivyo polepole Waasizi wakabadili mtazamo wao juu yao na kuanza kuwaheshimu. Ushindi huo ulipatikana kwa
gharama kubwa (dharau, mateso n.k.), lakini ushindi muhimu zaidi ni ule walioupata juu yao wenyewe wakijipatia hivyo
furaha na
uhuru wa wana wa Mungu.
Mt. Klara na Dada Wadogo
[
hariri |
hariri chanzo]
Kuanzia karne XI
wanawake wa
Ulaya walishika nafasi za maana kuliko kawaida katika jamii na Kanisa, wakijitokeza pia kwa wingi kufuata
tapo lolote la kiroho la Kikatoliki au la kizushi. Kumbe Fransisko hakupata mwanamke yeyote wa kumfuata kwa walau miaka sita tangu aongoke, na hata baada ya kumpata
Mt. Klara, hakuwapata tena wengi. Sababu ni kwamba hakuwa
mchungaji wa roho bali mtu mwenye kutafuta njia yake, wala hakuwa na mpango wa kuanzisha lolote, bali alitaka kushiriki tu hali ya watu wa mwisho. Basi, kwa wanawake nafasi ya mwisho haikuwa tu ile ya wakoma, bali pia ya ma
kahaba na ya
wachawi. Hivyo kwao chaguo la nafasi ya mwisho lilikuwa gumu zaidi, si tu upande wa mateso bali pia upande wa dharau, mbali ya kwamba lingesababisha masingizio juu ya uhusiano wao na ndugu wa kiume.
Klara alizaliwa mwaka
1193 au
1194, hivyo alikuwa na miaka 12-13 Fransisko alipovua
utu wa kale mbele ya mji mzima katika uwanda ule ambako iko nyumba ya Klara. Kwa hakika huyo akaendelea kusikia habari mbalimbali juu ya Fransisko: alivyopata wafuasi, mmojawao
Rufino binamu wa Klara; alivyokubaliwa na Papa n.k. Hatujui kama ni kwa sababu hizo kwamba alikataa
ndoa mbalimbali mpaka akafikia umri wa miaka 18, wala hatujui kama walikutana mara nyingi kwa mashauri ya kiroho. Ila tunajua kwa hakika kuwa baada ya Klara kukimbia nyumbani usiku na kujiunga na jamaa ya ndugu wadogo, akifuatwa na mdogo wake
Mt. Agnesi baada ya
wiki mbili tu, Fransisko alitimiza
wajibu wa kumlisha kiroho kwa mahubiri, mifano na hata maandishi.
Kwa
ushahidi wa Klara tunajua kwamba hata kwake himizo kuu la Fransisko lilikuwa kuambatana moja kwa moja na ufukara wa
Mwana wa Mungu. Mapema sana (kabla ya mwanzo wa mwaka
1213) Fransisko aliwaahidia akina Klara kuwashughulikia sawa na ndugu wa kiume, akafanya hivyo mpaka kufa, ingawa kipindi fulani alijizuia asiwatembelee kusudi ndugu wengine wasipate
kisingizio cha kufanya hivyo.
Klara aliitikia kwa namna bora ya upendo na
uaminifu, akamsaidia kuelewa vizuri zaidi wito wake wa kitume. Kufika kwake kwenyewe kulimfanya Fransisko afikirie sana na kushauriana naye juu ya maisha atakayoyashika. Mara wakatambua njia ya wanawake iwe tofauti na ile ya
wanaume: kwa hiyo Klara akawa
mmonaki na baadaye
abesi, ingawa kwa kushika kikamilifu ufukara mkuu na kuhusiana kidugu na wenzake.
Tofauti na ndugu wadogo, ambao Fransisko aliwaelekeza wafuate “
mtindo wa Injili takatifu”, yaani Yesu alivyowaagiza
mitume waende (
Math.10:5-15), aliwaelekeza Waklara kwenye “
ukamilifu wa Injili takatifu”, unaoonyeshwa hasa na
heri nane na
hotuba nzima ya mlimani (Math. 5:1-7:27), bila ya kuwabana kwa mtindo huo wenye vipengele vingi vya pekee. Tofauti inaonekana wazi katika ushahidi wa Askofu
Yakobo wa Vitry ulioandikwa mwaka
1216 ukieleza maisha ya Wafransisko yalivyokuwa bado mwanzoni: wote walikuwa wanakula
jasho lao, ila ndugu wa kiume kwa kufanya kazi hasa mjini au vijijini, kumbe akina
dada kwa kubaki katika makao yao.
Fransisko aliwahurumia daima wanawake hao waliokubali dharau na magumu ya kila aina. Yeye, ambaye hakusita hata kidogo kufuata tu mtindo wa Injili, katika kuwaongoza alizingatia sana
udhaifu wa
jinsia yao, na kama kwa kulazimishwa tu na Klara alimruhusu kushika magumu mengi: kila mara
huruma ya Fransisko na msimamo imara wa Klara vilikutana katika kumpendeza Mungu. Ni baada tu ya kung’amua msimamo huo, kwamba Fransisko alimuahidia atawatunza sawa na ndugu wa kiume. Mwongozo wake wa uso kwa uso ukawa muhimu kuliko kuwaandikia
kanuni fulani: badala yake mwenyewe alichukua
jukumu la kudumisha ufukara mkuu na udugu katika
monasteri ya kike.
Mkutano mkuu
[
hariri |
hariri chanzo]
Huyo Yakobo wa Vitry, pamoja na “
Ngano za Wenzi Watatu”, wanashuhudia jambo lingine muhimu katika Ufransisko, yaani
mkutano mkuu ambao ulikuwa ukifanyika kwanza mara mbili kwa mwaka kwenye
sikukuu ya
Pentekoste na ya
malaika Mikaeli, halafu kwenye Pentekoste tu ya kila mwaka, halafu tena kila baada ya miaka mitatu. Kuhusu wahudhuriaji, kwanza walikuwa ndugu wote, lakini walipoongezeka mno na kuenea mpaka mbali wakaruhusiwa kuhudhuria tu wahudumu wa jamaa. Mahali pa kukutana palikuwa Porsyunkula.
Kwa muundo huo Fransisko alitaka kudumisha
umoja kati ya wafuasi wake, kwa kuamua pamoja juu ya sheria na mipango ya shirika, lakini hasa kwa kustawisha upendo wao wa kidugu na kwa kuwarudisha pale walipoanzia, wasije wakasogea mbali mno na wito wao wa asili.
Mpaka alipoishi, mwenyewe alikuwa
moyo wa mikutano, awe anasikilizwa au kupingwa katika
juhudi zake za kuokoa mambo makuu ya karama yake mbele ya marekebisho yaliyodaiwa ili kulingana na viongozi wa Kanisa, na wingi wa ndugu wa kila aina na mazingira mapya. Marekebisho hayo yalikuwa yanabadilisha polepole sura ya jamaa, isiwe tena kundi dogo la marafiki wanaodharauliwa, bali shirika linaloeleweka na kuheshimika.
Fransisko alikubali marekebisho kadhaa ya lazima, lakini akikumbuka siku za nyuma alikuwa na
hamu ya kuzirudia: ndio
utatanishi ambao ulimfadhaisha mpaka mwisho ukaendelea kuvuruga umoja wa utawa wake. Upande mmoja ndugu mdogo anapaswa awe mtu wa mwisho katika Kanisa na jamii, kupenda adharauliwe na wote na kukabili magumu kama ya waliotupwa na wenzao. Upande mwingine anapaswa awe
mwanakanisa akishirikiana na wachungaji na kueneza toba kwa maneno yake pia, ambayo yapokewe kama muhimu kwa
wokovu wa watu. Kushika hayo mawili bila ya moja kumponyoka, ndilo
jaribio la Fransisko.
Zaidi ya hayo alikuwa akihimiza mkutano mkuu, ila pengine alikataza wasipite kiasi katika
malipizi, kama alivyomkataza Klara. Mwishoni, baada ya kuwabariki wote, alikuwa akichunguza na kuruhusu wahubiri wapya kwa kuzingatia walivyo katika ujuzi wa dini, uwezo wa kusema na hasa ubora wa maisha, kwa kuwa alitaka wafundishe kwa matendo kuliko kwa maneno.
Uenezi wa shirika na kujihusisha kwa Kanisa la Roma
[
hariri |
hariri chanzo]
Yakobo wa Vitry alieleza
furaha yake na
mshangao akiona
urahisi wa ndugu wadogo kupenya aina zote za watu, tofauti na wamonaki na wakleri. Ustawi wa shirika ulifanya lipate
nguvu katika Kanisa na kuenea kwa
kasi mahali pengi. Watawa hao wapya wakaja kuwavutia pia wanabaraza wa Papa, hata makardinali wakataka kuwa nao nyumbani mwao, na uhusiano na Papa ukawa mkubwa zaidi na zaidi.
Wakati huohuo nyumba za Kifransisko zikaanza kuwa za kudumu zaidi, ingawa si mali ya shirika, mpaka zikapata kila moja ndugu ambaye awe
mlinzi wa
wanajumuia wenzake.
Kwanza aliwashughulikia Kardinali
Yohane wa Mt. Paulo, lakini bila ya kujihusisha mno. Baada ya
kifo chake Fransisko akaona umuhimu wa kuwa na mwingine kama
mwakilishi wa Papa, akamuomba awe Hugolino, Kardinali askofu wa
Ostia, aliyemtabiria atakuwa Papa (akaja kuitwa Gregori IX). Huyo alikuwa na mang’amuzi mengi ya kisiasa na ya Kikanisa alipokutana naye huko
Florence; Fransisko vilevile alikuwa ameng’amua mengi kuhusu
uongozi wa shirika, tena kwa
uchungu, hasa kuwa hataweza kuliongoza peke yake. Ndiyo sababu ukaanzishwa
muundo wa
provinsya, yaani
kanda zilizokuwa kila moja chini ya ndugu fulani kama
mtumishi.
Ugawaji wa shirika kikanda ulihitajika hasa baada ya kuvuka milima ya Italia Kaskazini (
Alps) kati ya mwaka
1215 na
1217. Mwaka huo iliamuliwa pia kuvuka
Bahari ya Kati ili kuendea
Nchi Takatifu. Katika mkutano mkuu ulioamua hivyo, Fransisko aliwaeleza washiriki kuwa mwenyewe hawezi kubaki nyuma kisha kuwatuma ndugu zake wakabiliane na matatizo mengi, hivyo akajichagulia
Ufaransa akaondoka. Alipofika Florence ndipo alikutana na Hugolino, wakafunga
urafiki wa kudumu wakaheshimiana mpaka kufa. Mazungumzo yao ya awali ni kama picha ya yale yatakayofuata: Kardinali akimshauri Fransisko afuate
busara, Mt. Fransisko akieleza motomoto sababu za
imani zinazomuongoza, hatimaye Kardinali akinyamaza kwa kutambua Mt. Fransisko anaongozwa na
Roho Mtakatifu. Hugolino alifaulu kumzuia asiende Ufaransa, shirika lisije likashambuliwa mno na wapinzani wake mbalimbali, lakini Fransisko hakukubali kuacha mpango wa kutuma ndugu kwenye nchi nyingine za Kikristo na hata za
Kiislamu, akieleza kuwa Mungu aliyewatuma kwa wokovu wa watu wote atawatunza kokote alivyoahidi. Vivyo hivyo baadaye akakubali kiasi tu mashauri ya Hugolino, asiachane na mambo makuu ya wito wake.
Mbali na
dhana ya kwamba Kardinali alipotosha
mfumo wa Kifransisko kwa manufaa ya uongozi wa Kanisa, ukweli ni kwamba Fransisko alikubali marekebisho kadhaa akitambua madai yenye msingi ya ndugu wapya (hasa wa nchi za mbali na wasomi); zaidi tena
wema wake ulimfanya ayakubali ili kukwepa kikwazo kinachoweza kusababishwa na mabishano kati ya ndugu. Ndiyo mateso ya miaka kumi ya mwisho ya maisha yake: alizidi kuona
njia bora ya kuelekea utakatifu wa Kiinjili, kumbe wafuasi wake wengi wanashindwa kuikubali au wanakataa kuelekezwa, hata kwa kumpinga na kumdharau waziwazi.
Hivyo miaka ya ushindi na uenezi wa shirika, ndiyo miaka michungu zaidi kwake, kiasi kwamba akajaribiwa kukata tamaa na kujiona amedanganyika. Lakini akadumu kutegemea
maongozi ya Mungu kwa shirika lake, akapokea mateso hayo pamoja na ya
mwili kama namna nyingine ya kushiriki hali ya watu wa mwisho, na hasa ya Yesu msulubiwa aliyesalitiwa na wanafunzi wake.
Kuhusu uenezi wa shirika nje ya Italia tuna vitabu viwili muhimu kwa kuwa viliandikwa na wahusika,
Jordano wa Giano kuhusu
Ujerumani, na
Thomas wa Eccleston kuhusu
Uingereza. Hasa huyo wa pili bila ya kukusudia alionyesha wazi jinsi shirika lilivyozidi kusogea mbali na nia ya Fransisko kadiri mahali palipokuwa mbali na Italia na kadiri miaka ilivyozidi kupita.
Kwa vyovyote mwanzoni mwa uenezi huo hali ilikuwa ngumu, hasa kwa sababu hayakufanyika
maandalizi yoyote, tena Fransisko alikataa katakata kuwaombea waliotumwa hati ya
utambulisho toka kwa Papa. Hivyo sehemu nyingine walifukuzwa kama wachawi au wazushi, kwa sababu
Papa Inosenti III alikubali shirika na kanuni lakini kwa
sauti tu. Makubwa zaidi yaliwapata akina
Berardo waliouawa na Waislamu huko
Moroko (
1220): ndio
wafiadini wa kwanza wa shirika.
Matukio hayo yalichangia wazo la kuhitajika maandishi yenye kuthibitisha shirika, kwa kuwa Ndugu Wadogo walikuwa hawaeleweki: si wakaapweke, wala wamonaki, wala
wakanoniki, wala mapadri
wanajimbo, ila walidai kuwa shirika la kitawa bila ya kufuata mojawapo kati ya kanuni nne zilizokubalika kwa watawa.
Ni kwamba Fransisko aliogopa kanuni inayofuata mtindo wa kisheria badala ya mtindo wa Kiinjili: msimamo huo ulikuwa kinyume cha mazoea ya
Kanisa la Roma hasa wakati huo. Mt. Fransisko aliona Injili inazidi kutudai kadiri tunavyoendelea Kiroho, kumbe sheria zinaweza kutekelezwa na kumfanya mtu ajipongeze na kuridhika asijitahidi zaidi. Hasa alijua
ujanja wa
binadamu katika kufafanua sheria ili wakwepe mizigo yake. Hata hivyo Kanisa likamdai kanuni maalumu ili kuondoa wasiwasi juu ya shirika hilo jipya. Upinzani huo pia, uliochochewa na wamonaki na mapadri walioshikilia
mapokeo yao, ulionyesha haja ya kuthibitisha shirika kwa kanuni maalumu. Basi, kazi ilikuwa kuitunga: Fransisko aliziandika zaidi ya moja na kuzijaribu mpaka akatoa ile ya kudumu, akisisitiza hasa ufukara mkuu na kutaka
pesa iepukike.
Katika kazi hiyo alisaidiwa na ndugu wataalamu wa sheria, mbali ya mapendekezo ya mikutano mikuu na ya Kardinali Hugolino. Juhudi za Fransisko zililenga kuhakikisha kanuni haitazimisha roho, yaani hamu ya ukamilifu wa Kiinjili.
Lakini kabla hajakabili moja kwa moja kazi hiyo aliamua kwenda ng’ambo ya Bahari ya Kati kwa jaribio kuu la maisha yake: kumshuhudia Yesu mbele ya
sultani na ikiwezekana kuuawa kama ndugu mdogo halisi. Akaondoka fukara tena mpole,
silaha zake zikiwa ni imani na upendo tu, tofauti na
askari wa msalaba waliokuwa wakiuana na Waislamu.
Hamu ya kufia dini na ugonjwa wa Mt. Fransisko
[
hariri |
hariri chanzo]

Fransisko mbele ya Sultani
al-Kamil (
karne ya 15).
Hata kabla ya mwaka 1219 Fransisko alifunga
safari aende kumshuhudia Yesu kwa Waislamu: katika mwaka wa sita tangu aongoke (1211) alipanda
meli ambayo ikaishia
Korasya; halafu mwaka
1214 hivi akaelekea
Hispania ili kuvukia Moroko lakini akaugua ikambidi arudi nyuma.
Ni kwamba kuanzia karne XI, kama matokeo ya
vita vya msalaba, Wakristo walipata tena hamu kubwa ya kufia dini, wasiridhike na ile namna ya kumfia Yesu siku hadi siku kwa maisha ya kimonaki. Fransisko pia alitamani kumrudishia Yesu ule upendo mkuu wa kutoa
uhai kwa rafiki yake, lakini hakujitafutia mateso kwa kuwashambulia Waislamu kwa silaha wala kwa matusi, bali alijitahidi kuwaokoa kwa mahubiri yake motomoto lakini yenye
upole pia. Kama vile alivyokuwa mstaarabu kwa wote kabla hajaongoka, akaendelea kuwa hivyo hata kwa Waislamu wakati wa vita vikali kati yao na Wakristo, kwa kuwa alisema, “Mungu ni
ustaarabu”.
Alikwenda kwenye
kambi lao kama
mwanakondoo kati ya
mbwamwitu, bila ya
ulinzi wala hati ya kumtetea. Mbele ya sultani alibishana na
shehe wake, akaheshimiwa kwa
ujasiri wake wa kuhatarisha uhai wake ili kuokoa watu, na kwa ufukara wake uliomfanya akatae
zawadi yoyote. Ni wazi alikuwa na
karama ya kuvutia watu wowote, hata wasio Wakristo (mpaka leo anayo, ilivyoonekana siku ya kuombea amani iliyokusanya viongozi wa dini zote huko Asizi mwaka
1986). Fransisko alibaki
Mashariki ya Kati (
Siria,
Misri na
Israeli) zaidi ya mwaka mmoja.
Kabla hajaondoka Italia, akijitambua kuwa
mkuu wa shirika kubwa, aliacha ndugu wawili kama
makamu wake (
Mathayo wa Narni na
Gregori wa Napoli) akiwagawia
madaraka. Lakini kazi iliyokuwa ngumu kwa mwanzilishi mwenyewe ikawashinda, na juhudi zao hazikufaa: k.mf. walitunga sheria mpya kuhusu
mfungo ili zilingane na zile kali za mashirika mengine. Kumbe Fransisko hakuzipenda, akitaka zaidi kufuata Injili inayoruhusu kula vyovyote vilivyoandaliwa kwa watu wa Mungu. Kwake ilikuwa muhimu kuwa fukara kweli, na hivyo kukosa hakika ya kupata kila siku vyakula mbalimbali ambayo ingemdai mtu ajipangie mipaka asije akawa mlafi. Mfungo wa Kifransisko hasa si wa kujichagulia, bali unatokana na maisha yenyewe. Vilevile juhudi za ndugu wengine zilileta
vurugu zikienda kinyume cha nia ya Fransisko ya kutoomba hati za utetezi kutoka kwa Papa na kuhusu namna ya kuhudumia wakoma.
Hali ya shirika ikawa ngumu kiasi kwamba bradha Stefano akavuka
bahari bila ya
ruhusa akamuarifu Fransisko, ambaye, kisha kushauriana na
Petro Cattani, na kufunuliwa na Mungu la kufanya, akarudi haraka Italia akarudisha hali ya kwanza. Lakini aliona pia umuhimu wa kuwa na Kardinali mmojawapo ambaye alishughulikie shirika akamuomba kwa Papa kama tulivyokwishaeleza.
Ndipo pia alipokabili moja kwa moja kazi ya kutunga
kanuni ya kudumu. Kwa ajili hiyo alimuomba
msaada ndugu
Kaisari wa Speyer,
mtaalamu wa
Biblia, apambe maagizo ya Kanuni kwa maneno hasa ya Injili ili sheria zisizimishe hamu ya ukamilifu: madondoo hayo yanachukua thuluthi moja ya
Kanuni ya mwaka 1221.
Lakini tarehe
29 Septemba 1220 katika mkutano mkuu Fransisko akachukua hatua nyingine ya kushangaza, alijiuzulu katika wadhifa wa mkuu wa shirika. Sababu ni mbalimbali: hali mbaya ya
afya, matatizo ya shirika, hamu ya kurudi chini na kutii badala ya kuwa
kiongozi anayeheshimiwa na Kanisa lote. Pamoja na kuacha uongozi rasmi, hakuacha kuwajibika kama
kielelezo kwa wote na
mtungasheria mkuu.
Toka mwanzo waliomfuata hawakuzingatia sheria fulani, bali walikusudia kufanana naye; upande wake hakukubali kuwadanganya kwa kuwaonyesha utakatifu nusunusu au kuridhika na sifa yake bila ya kulingana nayo siku kwa siku. Hasa miaka ya mwisho akakazana asije akawa mtu wa kuheshimiwa badala ya mfano wa kufuatwa. Ndiyo sababu aliacha uongozi rasmi wa shirika ili aweze kuwa kielelezo wazi zaidi cha Ndugu Mdogo hasa katika kutii.
Ni vema tujiulize namna gani mfano wake uliweza kuwagusa watu wote. Upande mmoja ni kwamba wanahitajika watu wa Mungu, lakini hasa wasio mbali na jamii bali ni wenye kushiriki mang’amuzi ya watu wa kawaida, na wenye kupatwa na magumu ya maisha ya kila siku, hasa ya maskini. Upande wa pili
nafsi yenyewe ya Fransisko ilivutia wote hata kabla hajaongoka, na
mvuto huo wa ki
maumbile ukaja kuzidishwa na utakatifu aliojaliwa.
Uamuzi wake wa moja kwa moja wa kushika nafasi ya mwisho ulisababisha kwanza dharau, lakini baadaye heshima kwa kuwa unagusa mioyo ya wote, ukionyesha tena njia ya Mwana wa Mungu aliyeshiriki kabisa hali ya binadamu jinsi ilivyo kimaisha. Maneno yake mepesi, matendo yake ya kueleweka, mwenendo wake wa kupendeza, salamu yake ya amani,
kipawa chake cha kushirikisha furaha na uchungu, na mengineyo yalichangia ushindi wake. Lakini mwenyewe alilenga zaidi ushindi mwingine, yaani ule wa kuona
furaha kamili katika majaribu ya kila aina, hata kutoka kwa wafuasi wake.
Kati ya mateso yaliyomuathiri hatuwezi kusahau yale ya mwili. Wote wanashuhudia kwamba tangu
ujana wake alikuwa dhaifu, lakini baada ya kuongoka akatesa mwili wake kiasi cha kulazimika baadaye auombe umsamehe. Halafu alipokwenda ng’ambo ya bahari alipatwa na
maradhi mawili ya kudumu,
malaria (ambayo haikuwa na
tiba wakati huo) na
trakoma (inayosababisha
upofu wa
hatua kwa hatua).
Mbali ya mateso ya maradhi yenyewe, labda ni makali zaidi yale ya
matibabu ambayo aliagizwa na
ndugu Elia na Kardinali, akayavumilia kishujaa kabisa, k.mf. alipochomwa mishipa yote ya
damu kati ya
sikio na
jicho kwa kutumia
chuma cha
moto. Ili ashiriki zaidi mateso ya wakoma na wengineo, na hasa ya Mwana wa Mungu, hakujihurumia kama wagonjwa wengi, bali alizidi kuwahurumia wengine, kama vile ndugu waliomuuguza, wenyeji wake waliosumbuliwa na wageni waliomtembelea, na wagonjwa fukara. Tena hakuacha ukali wa malipizi yake kwa lengo la kuwa mfano bora kwa wanashirika. Nguvu zake za kiroho tu zilimfanya azidi kulishughulikia shirika na kulitungia kanuni katika hali hiyo ya
ugonjwa, pamoja na kuandika
barua kwa watu mbalimbali na kudai atembezwe juu ya punda ili atoe ujumbe wa Mungu walau hivyo akishindwa kuhubiri.
Uandishi wa Kanuni
[
hariri |
hariri chanzo]

Kanuni ya kudumu iliyothibitishwa na Papa Honori III tarehe 29 Novemba 1223.
Kama alivyokubali jamaa yake igeuke kuwa shirika, tena kubwa, Fransisko alipaswa kukubali linahitaji miundo ya kufaa, kama vile mwaka wa
unovisi (ulioagizwa na
Papa Honori III mwaka 1220) na hasa kanuni. Ni vigumu leo kutambua mabadiliko yote yaliyofanyika katika yale maneno machache ya Injili yaliyokubaliwa na Inosenti III kwa sauti tu (1209) mpaka ikathibitishwa kanuni ya kudumu (
1223). Miaka hiyo yote Fransisko alishughulikia
ufumbuzi wa
suala hilo zito, akisaidiwa au kupingwa na watu wengine, hasa wanashirika.
Kama kumbukumbu ya kazi hiyo inabaki sanasana
kanuni isiyothibitishwa, ambayo inashuhudia hatua iliyofikiwa mwaka 1221, na ambayo iliongoza utungaji wa kanuni ya kudumu. Kwa jumla katika ile isiyothibitishwa,
sura 17 za kwanza ni za zamani kuliko zile zinazofuata. Sura ya mwisho (24) ni sala tu ambayo ilitungwa na Fransisko na kubandikwa kama nyongeza.
Kwa nini kanuni hiyo haikuthibitishwa? Nani hakuridhika nayo? Mwenyewe au wafuasi wake au viongozi wa Kanisa? Hakika yeye alipendezwa nayo sana kwa jinsi inavyohimiza kuishi Kiinjili: ndiyo sababu mwishoni aliandika ndugu hawaruhusiwi kuongeza wala kupunguza wala kubadili hiyo kanuni.
Kumbe Kanisa lilidai kanuni iwe na sura ya kisheria zaidi. Hivyo kazi ya Fransisko ikaendelea, alivyoshuhudia hasa
ndugu Leo ambaye alikuwa
karani wake na kufuatana naye na
ndugu Bonisyo kwenye
mlima wa
Fonte Colombo ili kukamilisha kanuni majira ya baridi kali kati ya mwaka
1222 na 1223. Leo ametueleza upinzani wa akina Elia na uchungu wa Fransisko aliokuwa anautoa katika sala, hasa kutokana na hakika aliyokuwanayo juu ya matakwa ya Mungu kwa shirika lake: alikuwa akitulia tu katika nia yake ya kuzidi kuonyesha kwa matendo yake yale ambayo Yesu alimfunulia.
Hata hivyo, ndugu wengi hawakukubali kuyapokea kama sheria kwao. Ilimbidi akubali baadhi ya madai yao, pamoja na mashauri mbalimbali ya Kardinali na labda ya Papa mwenyewe. Lakini, pamoja na kutimiza hivyo udogo wake, hakukubali kuacha yaangushwe mambo makuu ya wito wake. Hivyo kanuni ya kudumu kwa jumla inafuata ile isiyothibitishwa, tena inaonyesha wazi kuwa mwandishi mkuu ni Fransisko, pia mengine yamesisitizwa naye hata kuliko alivyofanya katika kanuni ya muda. Pamoja na hayo, shida kubwa aliyoiona ni kwamba kanuni ya kudumu kwa mtindo wake wa kisheria inaeleweka zaidi, lakini pia inawaruhusu wanasheria kuitafsiri kwa namna inayoiondolea umotomoto wake.
Ingawa hakuweza kukwepa maendeleo hayo, mpaka mwisho wa maisha yake alitafuta
mbinu nyingine, kama vile kufanya Porsyunkula iwe kielelezo cha kudumu,
ndugu Bernardo awe mfano bora wa ndugu mdogo baada ya mwanzilishi kufa, na hasa wasia wake mfupi na mrefu ambao karne zilizofuata ukazidi kuchochea uaminifu wa wafuasi wake na kusababisha marekebisho mengi ya shirika.
Tarehe
29 Novemba 1223 kanuni ilithibitishwa na Honori III ikawa
sheria ya Kanisa ambayo Fransisko mwenyewe hakuweza kuibadilisha tena. Kwake na kwa Kanisa haukuwepo
wasiwasi kuhusu kanuni kuwa ileile ingawa imerekebishwarekebishwa. Kama vile tangu mwaka 1209 hadi 1223, hata baadaye alidai kuwa ndiyo Injili yenyewe, yaani
kiini chake.
Kwa njia ya kanuni hiyo Kanisa lilipokea aina mpya ya utawa isiyofuata sheria za kawaida. Katika kanuni zimeingia kwa pamoja karama ya Fransisko na mamlaka ya Kanisa linalopokea toka kwa Bwana wake zawadi ya
maisha yaliyowekwa wakfu likiifafanua na kuiratibu na kuipa miundo ya kudumu. Fransisko aliufurahia
uthibitisho wa Kanisa akazidi kuwahimiza ndugu zake waifuate hiyo kanuni akiwabariki kwa kila namna. Lakini katika kuielewa tunapaswa kuzingatia pia msimamo wa Kanisa lililoithibitisha. Lenyewe linadai mpaka leo ufafanuzi wake rasmi ubaki mikononi mwake, kama ulivyotolewa na Gregori IX (
1230),
Nikola III (
1279),
Klementi V (
1312) na
Inosenti XI (
1679).
Upande wa Fransisko tukumbuke hakika yake ya kuwa ameangazwa na Mungu aonyeshe upya mtindo wa Injili takatifu kama njia bora ya ukamilifu. Kwa msingi huo aliita kanuni
kitabu cha
uzima,
tumaini la wokovu,
uti wa Injili, njia ya ukamilifu,
ufunguo wa
paradiso,
sharti la
agano la milele. Kwa njia yake ndugu wanaweza kupata utulivu wa kweli na kuonja
utamu na wepesi wa
nira ya Kristo. Kwa wokovu wao alitaka wajifunze maneno ya kanuni na maana yake, na kuitafakari ili washinde
ulegevu na kutimiza
ahadi zao. Alitaka watumishi wajitahidi kufanya itekelezwe kikamilifu kama alivyojitahidi mwenyewe aliyeandika kuwa wanaoivunja hawahesabu tena kama Wakatoliki wala ndugu zake wala hataki kuwaona mpaka watubu. Mwishowe alitaka kila ndugu mdogo afe akishika kanuni mikononi.
Katika wasia aliwakataza pia ndugu wote wasifafanue kanuni wasije wakaipotosha katika
unyofu na
usafi wake. Bila ya shaka hakuweza kumkataza Papa asitoe
ufafanuzi, wala hakuwa na nia ya kuzuia maelezo manyofu yenye kulenga
utekelezaji wake mtakatifu.
Historia ya shirika ikaja kushuhudia kuwa unyofu huo mbele ya kanuni ndio uliostawisha utakatifu wa ndugu na utume wao: marekebisho ya mfululizo ya shirika ni kazi ya Roho Mtakatifu anayehuisha shirika la Ndugu Wadogo katika njia ya Injili wasipoachana na unyofu huo.
Maandishi mengine ya Mt. Fransisko
[
hariri |
hariri chanzo]

Baraka kwa ndugu Leo, iliyoandikwa na Fransisko kwa mkono wake mwaka 1224

Toleo la zamani kuliko yote yanayojulikana ya
Utenzi wa viumbe, linalotunzwa katika
maktaba ya
Konventi takatifu ya Mt. Fransisko, huko Asizi.
Kanuni ndiyo maandishi yaliyojenga zaidi utawa wa Ndugu Wadogo na Kanisa pia. Tunasema ni ya Fransisko ingawa alisaidiwa kuitunga: kwa kiasi fulani ni vilevile kuhusu maandishi yake mengine ya
Kilatini na ya Kiitalia. Kati yake tunaanza kuona mawili yanayotusaidia sana kuelewa historia ya shirika iliyofuata. Ya kwanza ni kanuni fupi kwa
makao ya upwekeni, ambayo ni muhimu ili kuelewa mwelekeo huo wa Fransisko na wenzake ambao ukawa mwelekeo wa wale wote waliotamani kurudia ufukara na
unyofu wa mwanzoni. Ya pili ni barua kwa Mt.
Antoni wa Padua, ambayo ni muhimu ili kuelewa msimamo wa mwisho wa Fransisko kuhusu masomo yaliyokuja kushika nafasi kubwa katika shirika na kuchangia tukio la ndugu wengi kuishi mijini katika
konventi kubwa (ndiyo asili ya jina “
Wakonventuali”).
Kanuni hiyo fupi iliandikwa kati ya mwaka
1217 na
1221, yaani wakati kanuni ya muda ilipokomaa kutokana na mang’amuzi ya shirika. Mtindo wa maisha ulikuwa umebadilika: ndugu wengi, badala ya kuishi karibu na miji au vijiji wakifanya kazi na watu
mchana na kukesha kwa Mungu
usiku, wamekuwa wanapendelea kuishi mbali na watu ili kusali tu. Kwa ajili hiyo yaliongezeka makao maalumu ya upwekeni ambamo ndugu wanaishi kwa muda fulani wakishika
desturi mbalimbali za
wamonaki. Fransisko aliona umuhimu wa kuuratibu mwelekeo huo ulingane na
karama ya Ndugu Wadogo, kama vile alivyofanya pamoja na Klara kwa wamonaki wake wa kike. Hivyo kanuni hiyo inasisitiza udugu na upendo kati ya
wakaapweke, pamoja na udogo. Katika roho hiyo ya Kifransisko zinakubalika desturi zifuatazo za kimonaki: kuwa na
ugo, chumba cha binafsi,
ratiba inayofuata vipindi vyote vya
Sala ya Kanisa, pamoja na kuamka usiku wa manane kwa
Kipindi cha Masomo, na
kimya kikuu hadi
Sala ya Kabla ya Adhuhuri.
Fransisko alivutiwa sana na maisha hayo, kwa sababu yalimwezesha kushika ufukara wa pekee, akiishi ma
pangoni kati ya miamba na katika vibanda vya
fito. Sababu nyingine ilikuwa kukwepa usumbufu wa watu waliomtafuta ili kumuona na kumheshimu. Hatujui kanuni hiyo fupi iliendelea kufuatwa mpaka lini, lakini mfumo wa upwekeni ukabaki na kuchochea
juhudi katika shirika hadi leo, mbali ya kwamba desturi hizo zilienea mapema katika konventi zote.
Barua kwa Mt. Antoni iliandikwa baada ya kanuni kuthibitishwa, yaani mwaka
1224 au
1225. Hiyo mistari michache yenye sura ya kisheria ilikuwa
jibu rasmi kwa
ombi la kuruhusiwa awafundishe
teolojia Ndugu Wadogo. Labda Antoni mwenyewe aliombwa afanye kazi hiyo akiwa
msomi wa kwanza katika shirika. Kwa vyovyote hakupenda kuleta jambo jipya utawani pasipo
ruhusa ya mzee wake. Huyo akimjibu aliheshimu
elimu yake kwa kumuita “Askofu wangu”, halafu akamkubalia akitambua ni hatua isiyoepukika, lakini akaweka sharti lilelile linalohusu kazi yoyote, yaani kwamba
roho ya sala na ibada isizimishwe nayo.
Ufupi wa barua, pamoja na utovu wa mapambo, unadokeza hali ya ndani ya mwandishi, kwamba aliamua kukubali kama kwa kulazimishwa na maendeleo ya shirika, ingawa anatambua hatari za kibali chake kwa siku za mbele. Basi, akamuachia Antoni jukumu la kuhakikisha masomo yasizimishe roho ya sala, akimuamini huyo mfuasi bora aliyeficha usomi wake kusudi awe ndugu mdogo halisi.
Hivyo ni wazi kwamba Fransisko hakuiogopa teolojia yenyewe: hivyo, ingawa alijiita
mjinga kwa kutokuwa na
elimu ya juu, alijiongezea mwaka hadi mwaka ujuzi wa Maandiko Matakatifu kwa njia ya
liturujia akajitafutia msaada wa ndugu
Kaisari wa Speyer ili kupamba kanuni ya muda kwa madondoo ya
Biblia. Aliyoyaogopa ni
kiburi cha wasomi,
majivuno ya
wahubiri, na hasa
ujanja wa
wanasheria, akijua kwamba hayo yote yanazuia
Neno la Mungu lisizae matunda. Alitaka neno lipokewe kwa unyofu jinsi lilivyo na kutekelezwa; basi, njia pekee ya kuweza kufanya hivyo ni sala ya kudumu.
Bila ya shaka, Antoni katika kufundisha alitimiza sharti alilowekewa, kama walivyokuja kufanya baada yake
walimu kadhaa, hasa Mt. Bonaventura. Lakini mwaka wa kifo cha Antoni (
1231) waliingia shirikani walimu wa
chuo kikuu cha
Paris, ambao wakaendelea kufuata mitindo walioizoea nje ya
Ufransisko. Hapo ndugu wadogo kama
mwenye heri Egidi wa Asizi walilaani mji huo wakisema umeharibu kabisa Asizi, yaani karama ya mwanzoni.
Basi, barua hiyo inathibitisha tena
busara ya Fransisko katika kukubali mabadiliko kadhaa asiache kupigania kiini cha karama yake, kuambatana na Yesu aliyeshika nafasi ya mwisho hapa duniani, akishikamana na watu wadogo, si kwa lengo la kuwapatia maendeleo ya kidunia tu, bali hasa kuwarudishia hakika ya kuwa ni wa maana kwa Mungu, kama si kwa watu wenye uwezo. Historia ya karne zilizofuata ikathibitisha ushindi wa Fransisko, yaani
uhai wa karama hiyo katika Kanisa.
Kuhusu maandishi mengine aliyotuachia, tukumbuke kwamba
maradhi yalikuja kumzuia kwa kiasi fulani asiendelee kusafiri sana kwa ajili ya
utume. Hasa baada ya kutiwa
madonda matakatifu akaja kuhitaji mfululizo ndugu
wauguzi ambao wakawa hivyo ma
shahidi wa mambo mengi waliyoyaandika hapo baadaye. Walishuhudia
mateso yaliyompata upande wa
mwili na wa
roho, yaliyomhusu binafsi na yaliyolihusu shirika na
upinzani ndani yake. Hata katika hali hiyo hakukubali kulegeza maisha yake, akitaka azidi kuwa kielelezo cha ndugu mdogo kwa wote. Vilevile alipopunguza utume wake, hakuacha kuwashughulikia watu walau kwa maandishi. Basi, tutayachambua kidogo kama njia bora ya kumfahamu mwenyewe na mang’amuzi yake.
Jambo ambalo linarudiarudia daima ni umuhimu mkuu wa
Mwili na Damu ya Kristo. Fransisko katika maandishi anaonekana
mwenezaji wa pekee wa
heshima kwa
sakramenti hiyo. Katika hilo alifuata maagizo ya
Mtaguso IV wa Laterano, lakini alipanga heshima hiyo katika ibada yake kwa Yesu. Kwake ni
ajabu upendo uliomfanya awe
mwanadamu hata akakubali kufa, na ni ajabu zaidi kwamba baada ya kurudi mbinguni anazidi kuitikia padri anapomuita katika
maumbo ya mkate na divai. Kutokana na hayo alidai padri aheshimiwe na kujiheshimu kwa kuishi kitakatifu pamoja na kuadhimisha na kutunza vema Mwili wa Kristo.
Kuhusu
barua halisi kwa mtu maalumu zimebaki chache sana; zilizo nyingi zilitumwa kwa viongozi wa shirika, kwa wakuu wa
serikali, kwa
wakleri na kwa
waamini wengine wote kwa jumla. Lengo lilikuwa kusisitiza mawazo yake makuu yashikwe na kufanyiwa kazi.
Barua kwa shirika lote ilikusudiwa kukumbusha
wajibu wa kila ndugu kama alivyokuja kufanya katika
wasia.
Kwa waamini jumla aliandika mapema barua nyingine ambayo wengi wanaamini kuwa ndio mtindo wa maisha ambayo aliwapendekezea watu wa toba ambao walivutiwa na mfano wake wakaja kuitwa
Utawa wa Tatu. Ndiyo sababu tunaikuta mwanzoni mwa kanuni ya
Papa Paulo VI kwa Wafransisko wa Ulimwenguni, na nusu yake ya kwanza imo pia mwanzoni mwa kanuni ya
Papa Yohane Paulo II kwa mashirika ya Utawa wa Tatu. Toleo la kwanza la barua hiyo lina sura mbili, kuhusu wanaofanya toba, halafu kuhusu wasiofanya toba. Kwa Fransisko toba ni kumpenda na kumuabudu Mungu kwa nguvu zote na kuzitii
amri zake. Toleo la pili likaongeza mambo mbalimbali, hasa ukurasa juu ya Neno wa Baba ambamo alijumlisha
fumbo la wokovu ili wote waishi kulingana nalo.
Tofauti na vijitabu hivyo vyenye sura ya barua ya wazi, kipo kingine cha pekee kilichosababisha wataalamu wabishane sana: ni
mawaidha ishirini na manne ambayo ni kama
muhtasari wa mafundisho ya Kibiblia ambayo Fransisko aliyasisitiza zaidi. Hatujui nani aliyakusanya wala lini. Si ajabu kwamba sura ya kwanza inahusu
ekaristi na kueleza kwa undani imani kutokana na
maisha ya sala hasa. Sura nyingine karibu zote zinahusu njia ya ufukara mkuu na unyenyekevu wa moyo. Kuanzia XIII mawaidha yana mtindo wa
Heri, yakichimba zile za
hotuba ya mlimani], isipokuwa XXVII inamchora
mtumishi wa Mungu ambaye maadili yake yamekomaa na kulingana yote, yakishinda vilema.
Aina ya mwisho ya maandishi ya Mt. Fransisko ni sala ambazo alizitunga na kuzitumia na ambazo zinatuwezesha kupenya
siri ya roho yake katika uhusiano na Mungu ambao ulifikia vilele visivyoelezeka. Katika maandishi ya aina hiyo hakulenga kuwaelekeza watu wafuate karama yake wala kuwahimiza wamtumikie Mungu, bali ni yeye na Mungu tu, hivyo tunafikia chanzo cha maandishi mengine na cha maisha yote ya Fransisko.
Kati ya sala hizo tunaweza kutia maanani
Sifa za Mungu alizoziandika kwa mikono yake kwa faida ya
ndugu Leo, huko mlimani
Alverna, mara baada ya kung’amua mateso na upendo wa Yesu msalabani. Ni tunda la moto la kumtazama Mungu na kumuitia kwa majina na sifa mbalimbali kutokana na Biblia, liturujia au moyo wenyewe wa Mt. Fransisko: ndivyo alivyozama ndani ya Mungu akirudia kumuelekea na kusema, “Wewe…”

Bonde la Umbria likiwa na
Mlima Subasio kwa nyuma: upande wa kushoto inaonekana
Assisi katikati ya mlima.
Sala nyingine ya pekee aliitunga si kwa Kilatini, bali kwa
lugha yake mwenyewe akiweza hivyo kutokeza kwa urahisi mkubwa zaidi yale aliyokuwanayo moyoni. Ni
Utenzi wa Viumbe Vyote,
shairi la kwanza la Kiitalia, ambalo alilitunga baada ya usiku wa mateso na majaribu ya kukatisha tamaa mnamo Aprili au Mei 1225, ambapo mwishoni aliahidiwa na Mungu
uzima wa milele. Katika
furaha isiyoelezeka ya kuwa na
hakika hiyo akiwa bado duniani, Fransisko alianza kumsifu Mungu kwa viumbe vyake ambavyo yeye kuliko watakatifu wote alijaliwa kuona vinavyohusiana na
Muumba. Tusisahau hali ya
afya yake wakati huo, ambapo hakuweza kuona kitu wala kuvumilia
mwanga, ila alikumbuka kwa
shukrani mazuri yote aliyoyaona hasa katika
bonde la
Spoleto, ambalo alisema hajaona mahali pazuri zaidi.
Katika utenzi huo hataji viumbe hai isipokuwa binadamu, ambaye anapaswa kumsifu Mungu hasa kwa njia ya
msamaha na
uvumilivu. Basi, alianza akimtukuza Mungu kama alivyozoea, kwa maneno mbalimbali, lakini mara tu akakiri kuwa binadamu hastahili hata kumtaja. Baada ya kutamka wazi jinsi Mungu alivyo Mkuu mno kuliko mtu, akaanza kumsifu kwa ndugu
jua: ndicho
kiumbe kilichomuuma zaidi kwa wakati huo, lakini linammaanisha Mungu kwa namna ya pekee. Halafu akamsifu kwa
mwezi,
nyota,
upepo,
majira,
maji,
moto na
ardhi inayotuzalia ma
tunda, ma
ua na ma
jani. Hatimaye akafunga utenzi akiwahimiza watu kumsifu, kumtukuza, kumshukuru na kumtumikia Mungu kwa unyenyekevu mkubwa.
Utenzi huo unapinga
uzushi ambao wakati huo uliambukiza wengi na kuwafanya waone
ulimwengu ni mbaya na unatawaliwa na
shetani. Fransisko hakubishana nao katika
mihadhara ya dini walivyofanya
Wadominiko, ila aliimba kwa lugha ya watu wadogo na kwa namna inayovutia juu ya uzuri na faida ya viumbe vinavyotangaza wema wa Muumba. Kwa kupokea ujumbe huo watu walikingiwa uzushi huo. Ndiyo njia ya Ndugu Wadogo katika utume: kuwaelekea watu wadogo kwa namna rahisi inayowasaidia kumgeukia Mungu kwa moyo wote. Usomi uliwazuia wengi wasione njia hiyo wala kuwafikia watu wa kawaida. Kumbe huyo mtu mnyofu, aliyejiita mjinga, aliwaelewa na kuwafikishia ujumbe wa imani.
Mtazamo mfurahivu uliomwezesha kuviona vyote kuwa ni ndugu zake, kwa kuwa vimeumbwa na Mungu yuleyule kwa faida ya mtu, ulimfanya asichoke kumshukuru na kuwaalika wote wafanye vilevile. Kuhusu mabaya yanayotokea pia hakuwalaumu mashetani, kwa kusema ndio walioharibu ulimwengu, bali aliwaona kama
askari wa Bwana waliopewa kazi ya kuadhibu makosa ya binadamu. Huyo ndiye mkuu wa viumbe vinavyoonekana, na ndiye aliyeharibu ulimwengu wote kuanzia
dhambi ya asili.
Katika maandishi yake Fransisko anatukumbusha kuwa yaliyotupata ni matokeo ya
dhambi zetu, na kuwa tunapaswa kutubu kwa kushiriki kazi ya Mkombozi. Mwenyewe alizingatia sana
fumbo la msalaba: toka mwanzo wa
uongofu wake alimzingatia Yesu katika ukweli wa mateso yake ambayo yalianza pangoni yakaendelea maisha yake yote kabla hayajafikia kilele chake huko
Kalivari. Kwa njia yake ukweli huo pia ukaja kuenea ukifuta uzushi uliomuona Yesu kama
malaika tu. Ukweli huo unadai si imani tu, bali upendo na
mshikamano naye. Kwa misingi hiyo Fransisko hakuweza kushindwa na
uchungu wote wa miaka ya mwisho ya maisha yake, bali aliugeuza kuwa
furaha kamili. Ndio ushindi wake pamoja na Kristo, uliothibitisha mafundisho yake. Ndivyo alivyoweza kuongeza baadaye mistari mingine katika utenzi huo ili kumsifu Mungu hata kwa ndugu kifo.
Miaka ya mwisho
[
hariri |
hariri chanzo]
Kaburi la Fransisko huko
Asizi.
Baada ya kanuni kuthibitishwa, Fransisko alikwenda
Greccio kujitafutia kimya na upweke. Ndipo alipopata wazo la kuadhimisha
Noeli kwa namna mpya ili kuitia maanani zaidi. Kwa msaada wa mtawala wa kijiji hicho, kwa ushirikiano wa wananchi na kwa mahudhurio ya ndugu wengi, liliandaliwa
pango lenye majani makavu,
ng’ombe na
punda, halafu ikaadhimishwa
Misa ambapo Fransisko, akiwa shemasi, alisoma Injili na kuhubiri kwa utamu mkubwa. Lengo lilikuwa kuwafanya Wakatoliki wote wakumbuke jinsi
Mwana wa Mungu alivyojishusha duniani, si tu kwa kujifanya mtu, bali pia kwa namna alivyozaliwa na alivyoishi. Chaguo lake la ufukara lilitegemea ukweli wa maisha ya Yesu kama mtu wa mwisho na mtu wa mateso. Baada ya miezi michache ufuasi huo wa moja kwa moja ukaja kuthibitishwa na madonda matano aliyotiwa juu ya
La Verna.
Kati ya Greccio na mlima huo, Fransisko alipitia maisha ya Yesu na kuyafanya yawe mang’amuzi yake matamu na ya kutisha pamoja. Ndivyo alivyozidi kutambua ubora wa mifano: kwa kuwa Yesu ametufundisha kwa matendo kuliko kwa maneno; upendo tu unaweza kupenya mafumbo yake na kupokea kikamilifu ujumbe uliofichika humo.
Kwa upendo wa namna hiyo Fransisko alipanda mlimani ili kuishi na ndugu wachache msituni. Katikati ya mwezi Septemba
1224 alifikiwa na
njozi ya pekee ambayo ilimuachia mwilini
madonda ya Yesu. Kwa kuwa yeye aliyaficha akaagiza wenzake pia watunze
siri; baada ya kufa tu watu wengi wakaja kujionea katika
maiti yake ajabu hilo, ambalo liligusa zaidi mioyo kwa sababu ilikuwa mara ya kwanza kutukia duniani.
Mbali ya mateso hayo aliyojaliwa Kimungu, miaka ya mwisho ya Fransisko iliendelea kujaa yale ya kibinadamu pia. Kwanza
maradhi ambayo
matibabu aliyoagizwa kuyapata hayakuleta
nafuu, bali yalizidi kuharibu na kumtesa: inatosha tukumbuke alivyochomwa kwa
chuma cha
moto kuanzia
jicho hadi
sikio. Halafu juhudi zake za kuendelea kuwa kielelezo cha toba kwa wafuasi wake, ambao upande wao walizidi kumtia uchungu hata katika kumtumikia na kumheshimu. Bila kusahau majaribu ya
usiku wa roho yaliyoendelea mpaka katikati ya mwaka
1225, alipoahidiwa
uzima wa milele.
Miaka hiyo ina mashahidi wa pekee, yaani ndugu wanne waliomuuguza mfululizo:
Anjelo Tancredi,
Leo,
Rufino na
Yohane wa Masifu. Wa kwanza kati yao wanajulikana sana kwa jina la
Wenzi Watatu: baadaye wakaja kuandika kwa
utiifu mambo waliyoyaona na kuyasikia. Kwa njia yao tunaweza kufuata hatua kwa hatua maendeleo ya
malaria, iliyomsumbua Fransisko miaka sita mfululizo hata mwisho ikamuua, tena ya
trakoma, iliyosababisha
upofu karibu kamili, pamoja na maumivu ya mfululizo yanayofanana na yale ya macho kuwekwa juu ya miiba na kutokwa machozi.
Ndugu Elia na Kardinali Hugolino walimshughulikia sana, lakini bure. Pamoja na kutambua jambo hilo, katikati ya mwaka 1224 ndugu Elia alipata njozi na kufunuliwa kuwa Fransisko ataishi bado miaka miwili tu.
Safari za
mgonjwa zilizidi kupungua kwa wingi na kwa umbali, zikifanyika hasa kwa kujaribu matibabu na kurudi kila mara kwenye Porsyunkula.
Hata katika hali hiyo Fransisko hakuacha kulihangaikia shirika lake kadiri alivyoona linasogea mbali na karama yake. Ili awe kielelezo kwa wote alizidi kujinyima mahitaji ya mwili, na kutamani arudie maisha yaliyodharauliwa ya mwanzoni na kutumikia wakoma. Ndipo alipowaambia wenzake, “Ndugu, tuanze kumtumikia Bwana Mungu, kwa kuwa mpaka sasa hatujapiga hatua au ni ndogo sana”.
Aliogopa shirika lake litalegea kama mengine mengi, hivyo akatafuta
mbinu za kuliokoa, kusudi kanuni isiwe mwisho wa juhudi za ndugu, bali kichocheo kwa kutafuta ukamilifu. Mbinu mojawapo ni wasia wa Kiroho aliouandika zaidi ya mara moja. Muhimu zaidi ni ule mrefu aliouandika katika wiki za mwisho za maisha yake. Haukukusudiwa kuwa kanuni mpya, ila kusaidia ile iliyoahidiwa kwa Bwana: ni
kumbukumbu,
onyo na
shauri.
Kwanza ni kumbukumbu za uongofu wa Fransisko na za maisha asili ya shirika ambayo ndugu wote wafananishe nayo maisha yao. Katika kumbukumbu hizo hakutaja mateso yote aliyojaliwa na Mungu, bali alifafanua chaguo lake la kumfuata Yesu fukara kama utajiri pekee anaowaachia watoto wake. Hivyo wasia, ukiunganisha maagizo ya kanuni na mang’amuzi ya mwanzilishi, ukabaki katika shirika kama
mwiba mwilini mwa wanaopenda kulegeza
kamba, na kama
changamoto kwa wote kadiri walivyompenda Fransisko, kwa kuwa ndiyo maneno yake ya mwisho aliyoyatoa kwa upendo mkuu akiwa amefanana na Yesu msulubiwa hata mwilini mwake. Ndiyo sababu toka mwanzo wasia ulisababisha shirikani mabishano yaliyohitaji kuingiliwa kati na Mapapa. Upande wa wasia walisimama ndugu waaminifu, ingawa kipindi fulani baadhi yao (
Fraticelli) walipita kiasi hata kujitenga na Kanisa ili kupigania ufukara; baada yao kosa hilo halijarudiwa tena. Baadhi ya marekebisho ya shirika (k. mf.
Wakapuchini) yalijifunga kushika wasia pamoja na kanuni, na hivyo wakafaulu kurudia maisha asili.
Pamoja na kumbukumbu, katika wasia tunakuta maonyo ya mwisho ya Fransisko kuhusu kuheshimu mapadri, kufanya
kazi za mikono, kuishi kama
wakimbizi katika
nyumba duni, na kutoomba
fadhili yoyote kutoka
ofisi za Papa.
Polepole maonyo yakawa mashauri, na hasa shauri kuu lililo lengo la yote yaliyotangulia, kiasi kwamba ni katazo kali. Linahusu ujanja wa wanasheria katika kupotosha maana halisi ya maneno ya kanuni na wasia. Kuyaelewa kunahitaji unyofu uleule wa Fransisko pamoja na nia ya kuyatekeleza. Watakaofanya hivyo watapata
baraka pana kabisa ya Mungu na ya kwake. Kivutio hicho kimejaa upendo wa mzee kwa watoto wake ambao ulijitokeza mara nyingi miaka ya mwisho katika maneno, maandishi na matendo.
Mfano mmojawapo ni
Takwa la Mwisho alilomuandikia Klara ili kuwahimiza
mabibi fukara wadumu mpaka mwisho katika maisha na ufukara wa Yesu. Ni kama wasia mfupi kwa wafuasi wake wa kike, ambao hakuwa na wasiwasi juu ya uaminifu wao, lakini aliwaogopea watashauriwa sana na watu wengine (viongozi wa Kanisa na wanashirika) walegeze masharti ya ufukara. Ndiyo sababu aliwaachia maneno hayo kwa maandishi ili wadumu imara katika nia yao. Historia iliyofuata ikaonyesha Fransisko alitabiri vizuri kuhusu Klara na wenzake, waliopaswa kupambana mfululizo na
kishawishi hicho toka kwa viongozi waliowapenda. Ushindi wa Klara katika kutetea kwa uaminifu ufukara mkuu ulipatikana siku ya mwisho kabla hajafa, alipoletewa kanuni yake imethibitishwa na
Papa Inosenti IV. Katika kanuni hiyo, ambayo katika Kanisa ilikuwa ya kwanza kuandikwa na
mwanamke, Klara alifuata kwa kiasi kikubwa ile ya Fransisko kama thibitisho la
umoja wa Kiroho katika tofauti za mitindo yao ya maisha; pia alinakili humo wasia huo mfupi alioutumia kama
silaha katika mapambano.
Mbali ya maandishi yake, Fransisko alitafuta mbinu nyingine ili kudumisha shirika katika karama yake. Mojawapo ni kuwaagiza watumishi wa shirika watunze Porsyunkula kama kielelezo cha ufukara, kimya na sala ili ndugu wote wakumbuke wanavyopaswa kuishi. Kwa ajili hiyo alitaka wapangwe huko ndugu bora ambao mmojawao akifa, nafasi yake ishikwe na mwingine. Hivyo alisisitiza tena umuhimu wa mifano, ambayo isiwe ya mtu mmojammoja tu, bali ya jumuia nzima pia. Jambo hilo halikutekelezwa mahali pale, lakini katika historia ya shirika tunaona daima ndugu wakiomba ruhusa ya kutekeleza kikamilifu kanuni pamoja na wengine, hasa katika makao ya upwekeni; tunaona pia mchango mkubwa wa jumuia hizo katika kurekebisha kwa mfano wao hali ya utawa mzima. Mfransisko ni ndugu hasa, na maisha yake yanategemea sana jumuia: hawezi kuridhika ashike kanuni kibinafsi katika jumuia iliyolegea; ndiyo sababu ya maombi hayo. Pengine viongozi wenyewe wa shirika walipoona limelegea mno wakaja kuhamasisha wenye nia waunde jumuia za pekee. Namna zote mbili zikazaa matunda tele.
Fransisko, baaada ya kuuguzwa katika jumba la Askofu wa Asizi kwa siku kadhaa, aliomba ahamishiwe Porsyunkula ili afie pale alipoanzia maisha mapya. Alikuwa amebaki mifupa na ngozi tu, isipokuwa tumbo na miguu vimevimba kama kwa safura. Ndipo alipotunga
ubeti wa mwisho wa
Utenzi wa Viumbe Vyote. Mwaka mmoja kabla ya hapo alikwishaongeza ubeti mwingine juu ya
msamaha ili kuwapatanisha Askofu na
Meya wa Asizi. Basi ubeti juu ya
kifo ukaja kukamilisha utenzi mzima kwa kuchungulia uzima wa milele, ambapo sifa za Mungu zinaimbwa bila ya mwisho. Ndivyo alivyojiandaa kufa katika
mapenzi ya Mungu.
Siku za mwisho zilijaa ishara za upendo kwa marafiki wake: njiani alibariki Asizi na kuuombea, akamtabiria Klara kuwa atamuona na kufarijika, akawaita ndugu waliokuwa mbali (hata “kaka”
Yakopa wa Settesoli kutoka Roma), akawagawia vipande vya mkate akifuata mfano wa Yesu. Katika yote alilenga ustawi wa roho zao na wa shirika, tunavyoona hasa katika baraka zake za mwisho alizozitoa kwa kufuata mfano wa mababu wa
Israeli na
Musa. Aliwabariki waliokuwepo na kwa njia yao alikusudia kuwabariki wale wote watakaoingia shirikani mpaka mwisho wa dunia.
Kati ya wote
ndugu Bernardo alipata baraka ya pekee akaandikiwa maneno yafuatayo yawe kumbukumbu kwa wote siku za mbele: “Ndugu wa kwanza aliyenipa Bwana ni ndugu Bernardo, naye ndiye wa kwanza kutekeleza kikamilifu kabisa Injili takatifu akiwagawia maskini mali zake zote. Kwa hiyo na kwa sifa nyingine nyingi napaswa kumpendelea kuliko ndugu mwingine yeyote katika shirika zima. Ndiyo sababu nataka na kuagiza kadiri ninavyoweza kwamba yeyote atakayekuwa mtumishi mkuu ampende na kumheshimu kama nafsi yangu, na vilevile watumishi wengine wa kanda na ndugu wa shirika lote wamjali kama ni mimi mwenyewe”. Ndiyo mbinu ya mwisho ya Fransisko ili kuzuia utawa wake usipotoke: kumuacha mtu ambaye awe kielelezo kwa viongozi na kwa ndugu wengine badala ya mwanzilishi. Kisha kumuacha huyo mwandamizi (si katika uongozi bali katika kazi muhimu zaidi ya kuwa kielelezo), Fransisko hatimaye aliweza kuaga dunia amemaliza kazi yake na kulazwa
uchi ardhini,
usiku kati ya tarehe 3 na 4 Oktoba 1226.
Maandishi asili kuhusu Fransisko
[
hariri |
hariri chanzo]
Baada ya kupitia maisha na maandishi ya Fransisko, ni vema kujua jinsi habari zake zilivyotufikia kwa njia ya maandishi ya watu wengine pia. Baadhi yaliandikwa mapema kabla hajafa. Baadhi ni hati za Kanisa. Baadhi ni mafupi sana na yanamtaja tu katika kusimulia mambo mengine. Baadhi ni kazi ya watu ambao si Wafransisko, tena pengine hawakupenda huo mtindo mpya wa kitawa. Lakini bila ya shaka habari nyingi zaidi zinapatikana katika maandishi ya wafuasi wake. Kati yao ana nafasi ya pekee Klara kwa sababu ya utakatifu wake, ya uhusiano wa ndani na wa muda mrefu na Mt. Fransisko, na ya uaminifu wake katika kumfuata.
Maandishi mengine ya Wafransisko yanatofautiana si tu kwa urefu, kwa mtindo, kwa mpangilio au kwa ufasaha, bali pia kwa malengo na mitazamo. Hasa mabishano katika shirika yalifanya kila mmoja akusanye habari zilizompendeza ili kumchora Fransisko kulingana na msimamo wa kikundi chake: ndiyo sababu ni lazima tulinganishe maandishi yote ili kupata ukweli.
Thoma wa Celano ndiye wa kwanza kuandika kitabu cha maisha ya Fransisko. Alifanya kazi hiyo kwa agizo la
Papa Gregori IX akikusanya
shuhuda zilizotolewa katika
kesi ya kumtangaza Fransisko kuwa mtakatifu (
16 Julai 1228) pamoja na kumbukumbu zake mwenyewe za miaka sita aliyoishi karibu naye. Mwaka
1229 akamkabidhi Papa kitabu hicho ambacho aliipa uzito hasa miaka miwili ya mwisho ya Fransisko, ambapo utakatifu wake uling’aa kwa namna ya pekee. Pamoja na kufuata mtindo wa wasifu wa watakatifu wa zamani, Thoma alisisitiza mambo mapya ya Fransisko: ufukara, unyofu, unyenyekevu, wema kwa maskini, upendo kwa viumbe, mahubiri yasiyo na mapambo, hata madonda ya Msulubiwa. Kitabu hicho rasmi kilikusudiwa hasa kueneza heshima kwa Fransisko, lakini pia kulitetea shirika lake dhidi ya upinzani wa nje.
Kwa kila shirika, heshima inayotolewa kwa
mwanzilishi inaliletea heshima na nguvu katika maisha ya Kanisa, na mara nyingi hata misaada na faida upande wa uchumi. Hivyo tunaelewa mafanikio ya haraka ya ndugu Elia katika kujenga
kanisa kubwa la Mt. Fransisko huko Asizi. Kwa kumtukuza, shirika lilijitukuza. Ukweli huo ni wazi katika mwendelezo wa maandishi juu yake pia.
Miaka iliyofuata (
1230-
1234) zilitungwa sala na nyimbo za liturujia kwa heshima ya mtakatifu huyo mpya. Kati ya watunzi,
Julian wa Speyer aliandika pia maisha yake (
1232-
1235), hasa kwa ajili ya Wafransisko na ya malezi yao. Wakati huohuo (
1232-
1239)
Henri wa Avranches alitunga maisha ya Fransisko kwa mtindo wa shairi.
Katika miaka
1237-
1239 sura yake nyingine ilichorwa na kuenezwa na kitabu kidogo, jina lake “
Agano Takatifu la Mt. Fransisko na Bibi Ufukara”. Kichwa chenyewe kinaonyesha wazi kuwa kitabu kinasisitiza upendo wake kwa Ufukara kama
mchumba wake. Humo yeye anaonekana kama fukara mdogo ambaye alimtafuta sana Ufukara, akamuona katika kilele cha mlima anapokaa, hapo wakasimuliana maisha yao na kufunga agano la upendo na uaminifu. Picha hiyo ikazingatiwa sana mpaka leo.
Hiyo ilikuwa miaka ya mwisho ya uongozi wa ndugu Elia, ambayo ilizidi kuwa na mabishano kati ya Ndugu Wadogo. Hata baada ya kumuondoa madarakani, mabadiliko ya maisha yakaendelea kufanyika na kusababisha maswali juu ya nia halisi ya mwanzilishi. Ndipo (
1240-
1241)
Yohane wa Perugia alipoandika kitabu juu ya asili ya shirika ili kuamsha ule moto uliowaka mwanzoni kati ya wenzi wa Fransisko. Habari zake ni mpya kwa asilimia 60 na kutegemea hasa ushahidi wa
mwenye heri Egidi. Kwa kuwa Yohane hakujitaja kitabu hicho kinaitwa “
Kitabu Kisicho na Jina cha Perugia”.
Miaka ishirini baada ya kifo cha Fransisko hamu ya kujua habari zake ilikuwa imeongezeka ndani na nje ya shirika. Ndiyo sababu wakati wa mkutano mkuu wa mwaka
1244 mtumishi mkuu mpya aliagiza ndugu wote walete kwa maandishi kumbukumbu yoyote waliyonayo juu yake. Kutokana na agizo hilo vikapatikana vitabu viwili tulivyonavyo hata leo: cha kwanza kilitungwa katika miaka
1241-
1247 kikaitwa “
Ngano za Wenzi Watatu”. Kinategemea sana kitabu cha Yohane wa Perugia lakini kinatia mkazo zaidi juu ya Fransisko mwenyewe na kuonyesha njia ya kuongoka na kufanana na Kristo ambayo aliifuata na ambayo inawafaa wote. Cha pili kinaitwa “
Mtungo wa Asizi” (
1244-
1260) kwa kuwa kinakusanya shuhuda za ndugu mbalimbali walioishi naye, pamoja na kuchukua msimamo dhidi ya mabadiliko shirikani.
Lakini kazi ya kuandika upya maisha rasmi ya Fransisko ilikabidhiwa tena kwa Thoma wa Celano, naye akaimaliza mwaka 1247. Kitabu hicho hakikukusudiwa kushika nafasi ya kile alichotangulia kukiandika, bali kukitimiliza kutokana na ushahidi wa wengi, hasa wenzi watatu, waliotuma kumbukumbu zao na za wenzao wa kwanza pamoja na barua kutoka Greccio (
11 Agosti 1246). Kitabu cha pili cha Thoma kilisisitiza utakatifu wa Fransisko kama mkuu kuliko ule wa waanzilishi wengine wote, kwa hiyo ujana wake haukulaumiwa kama mara ya kwanza, Mt. Dominiko anaonyeshwa akimuinamia Fransisko n.k. Vimeongezwa: maneno ya Msulubiwa kwa Fransisko, njozi ya Papa Inosenti III kuhusu kazi yake ya kulitegemeza Kanisa n.k. Fransisko alizidi kulinganishwa na Kristo kama ilivyotarajiwa na wanashirika. Pamoja na hayo kitabu hicho kinatuletea kwa wingi habari za maadili yake, misemo yake na nia zake.
Hata hivyo shirika kwa jumla halikuridhika sana; ndiyo sababu katika miaka
1250-
1252 Thoma akaandika kitabu chake cha tatu ambacho kinakusanya miujiza tu ya Fransisko ili kuzidi kumtukuza yeye pamoja na shirika lake.
Lakini hivyo vitabu vitatu vya Thoma vilionekana kukosa umoja na kuwa virefu mno hasa kwa kuvinakili kwa mikono. Ndicho kisingizio cha kudai maisha ya Fransisko yaandikwe upya katika kitabu kimoja tu. Lengo lingine la ombi hilo lilikuwa kulikinga shirika dhidi ya mashambulizi makali ya walimu wa
chuo kikuu cha Paris waliopinga mambo mapya yaliyoletwa na Ndugu Wadogo, ambao baadhi yao wameambukizwa pia na matabiri ya kizushi ya
abati Yohakimu wa Fiore. Huyo alipanga
historia ya wokovu kwa namna yake akisema mwaka
1260 utakuwa mwanzo wa wakati wa
Roho Mtakatifu ambapo Kanisa litafanywa upya na karama zake. Ndipo Wafransisko hao walipochota mawazo mbalimbali ili kuthibitisha umuhimu wa Fransisko katika hatua hiyo na katika historia ya wokovu jumla.
Basi mwaka huo mkutano mkuu ulimuagiza
Bonaventura wa Bagnoregio, mtumishi wa shirika lote, aandike kitabu kipya. Hicho hakina habari mpya ila kinatumia zile za Thoma wa Celano. Tofauti kubwa ni namna alivyozitumia ili kumuonyesha Fransisko kuwa si
serafi tu (alivyosema Celano) bali ni yule
malaika wa mhuri wa sita mwenye alama ya Mungu aliye hai aliyetabiriwa na
Ufu 7:2 kuwa atapanda toka
Mashariki kufungua wakati mpya. Kwake Mungu aliye hai ndiye Kristo Msulubiwa, na alama yake ndiyo madonda matano aliyomtia Fransisko. Basi, kama ni hivyo, huyo si mtakatifu mmojawapo tu, bali ana nafasi ya pekee katika historia ya wokovu.
Mchoro huo ulikubaliwa kabisa na shirika lote, hivi kwamba mkutano mkuu wa mwaka
1266 ukaweza kuagiza yateketezwe maandishi yote yaliyotangulia kuhusu Fransisko. Lengo lilikuwa wote wamkumbuke tu alivyochorwa na Bonaventura katika kitabu chake rasmi na cha kudumu. Kweli hicho kikanakiliwa sana kwanza kwa mikono, halafu kwa mashine na kufuatwa na wengi katika sanaa, mahubiri na liturujia. Kumbe vitabu vya Celano vikapotea kwa zaidi ya karne tano. Hata ndugu waliopinga mabadiliko ya shirika na msimamo wa kati wa Bonaventura, walimlaumu kwa sababu ya kupunguza habari kadhaa, lakini walipendezwa na jinsi alivyomtukuza Fransisko kuliko watakatifu wote. Kwa kitabu hicho sura yake imeshakamilika.
Vitabu vilivyotungwa baadaye, k.mf. “
Kioo cha Ukamilifu” (
1318), havikuweza kuichangia sana, ingawa vinatusaidia kumuelewa zaidi katika majaribu yake, nia yake na roho yake kwa kuwa vinasimulia bila mpango habari mbalimbali ambazo hazikutumiwa zote na vitabu rasmi. Hasa habari juu ya
upinzani uliompata Fransisko ndani ya shirika hazikuweza kuandikwa katika vitabu vyake rasmi, lisije likapata
aibu. Basi, maandishi hayo ya mwishomwisho yaliziba pengo hilo na kutuonyesha ukweli, kama picha iliyofyatuliwa kwa
kamera bila wahusika kujua wala kujipanga. Vitabu hivyo vilichochea upinzani ndani ya shirika na hata dhidi ya uongozi wa Kanisa.
Baadaye tena (
1328-
1343)
Hugolino wa Montegiorgio na mwenzake fulani wakatunga “
Actus” (= “Matendo” ya Fransisko na wenzake) ambacho kikatafsiriwa kwa
Kiitalia mwishoni mwa
karne XIV.
Tafsiri hiyo, yenye jina la “
Fioretti” (= “
Maua Madogo”, yaani “
Visimulizi Bora”), ikasifiwa sana kwa uzuri wake, ingawa visimulizi vyake si vyote vya kihistoria. Ni kama
manukato yanayotuvutia kwenye roho na utakatifu wa Fransisko, aliyekwishakufa toka siku nyingi, hivi kwamba anakumbukwa kwa mbali lakini kwa namna ya kupendeza zaidi. Miaka iliyopita imechuja ujumbe wake, ambao hivyo unang’aa kwa namna ya pekee katika kitabu hicho kilichosisitiza jinsi Fransisko alivyofanana na Yesu, wazo lililokazwa na Wafransisko wote wa
karne XIV, hasa na
Bartolomayo wa Pisa, mwandishi wa “
Conformitates” (= “
Uwiano Mwingi”).
Tarehe za maisha yake
[
hariri |
hariri chanzo]
1182 Mtoto Yohane alizaliwa na kubatizwa. Baba yake, Petro wa Bernardone, akirudi toka safarini akamtajia jina la Fransisko, yaani Mfaransa Mdogo. Baada ya hapo mtoto akalelewa katika anasa, ingawa hatujui kama ujanani aliulinda
usafi wa moyo au sivyo. Kwa tabia alikuwa na uchangamfu na huruma sana kwa maskini ingawa aliogopa wenye ukoma. Pamoja na adabu njema alipewa pia elimu kidogo kupitia mapadri, halafu akawahi kuanza biashara.
1198 Asizi vilianza vita vya wenyewe kwa wenyewe: inawezekana kwamba Fransisko naye alishiriki kushambulia na kubomoa ngome ya kifalme iliyokuwepo juu ya mji huo.
1202 Asizi ulishindwa vitani na jeshi la Perugia; Fransisko mwenyewe akatekwa na kufungwa huko Perugia. Baada ya mwaka mmoja akarudishwa nyumbani kwa sababu ya ugonjwa na kisha kulipiwa pesa nyingi ili aachiliwe; lakini wakati huo wa mateso alianza kukomaa na kubadilika kimawazo.
1204 Fransisko aliendelea kuugua mwaka mzima.
1205 Fransisko aliondoka tena aende vitani kuikomboa nchi takatifu ya Yesu na kujipatia sifa na cheo, lakini kabla hajatoka mkoa wake akarudi Asizi kutokana na njozi na sauti aliyoisikia. Akaenda kuhiji
Roma kwenye makaburi ya Mitume, ambapo anabadilishana nguo na fukara na kuanza kuombaomba. Katikati ya mwaka uongofu wake ulikuwa umekomaa: katika
karamu ya mwisho aliyowaandalia wenzake alikuwa akifikiria kuoa bibi ufukara. Alipokutana ghafla na mtu mwenye ukoma akashuka kwenye farasi na baada ya kumsaidia pesa akambusu: ndio ushindi mkuu uliofanya kuanzia hapo kusiwe na kitu cha kumzuia. Karibu na mwisho wa mwaka akamsikia Yesu msalabani akimuambia, “Fransisko, nenda ukarekebishe Kanisa langu, kwa kuwa linataka kubomoka”: ndiyo kazi ya utawa atakaoanzisha, ingawa mwanzoni alielewa tofauti, kwamba arekebishe magofu ya kanisa aliposikia sauti hiyo.
1206 Mwanzoni mwa mwaka, baada ya miezi ya mashindano na wazazi wake, waliokuwa wakimshutumu na kumbembeleza na kumtesa, Fransisko aliitwa hukumuni kwa meya: lakini kama mtu wa Mungu akakataa mahakama ya serikali, hivyo kesi akafanyika mbele ya askofu Guido ambapo alimkataa mzazi wake pamoja na mali za urithi hata akamrudishia nguo zake zote. Baada ya kuishi kidogo kama boi kwa Wabenedikto, akahamia Gubbio ambapo akavaa kanzu ya mkaapweke,akisali na kutumikia wakoma. Mnamo Julai akarudi Asizi arekebishe kanisa la mtakatifu Damiano ambapo alitabiri watakuja kukaa masista watakatifu.
1207 Alirekebisha kanisa la mtakatifu Petro na mwisho lile la mtakatifu Maria wa Malaika: kazi za ukarabati zilichukua karibu miaka miwili, kwa kuwa mwenyewe alikuwa akienda kuombaomba mawe ya kujengea, ingawa hakuwa na uzoefu na kazi nzito namna hiyo.
1208 Siku moja wakati wa Misa alisikiliza sehemu ya Injili ambayo Yesu aliwatuma kwa mara ya kwanza mitume wake (Mt. 10:7-10); hapo akaenda kwa padri kupata tafsiri zaidi na maelezo yake, halafu kwa shangwe akaanza kutekeleza, kwa kutupilia mbali mkanda na viatu, kuvaa kamba na kanzu ngumu na kuhubiri toba. Kama siku hiyo, ambapo hatimaye alielewa wito wake, akaendelea daima kuwa mtu wa Injili na mwana wa Kanisa. Tarehe 16 Aprili, baada ya kuhubiri alifuatwa na ndugu Bernardo wa Quintavalle na labda na ndugu Petro Cattani walioamua kujiunga naye; basi akawaongoza kanisani, wakasoma Injili kwa kufungua kitabu mara tatu, wakauza mali zao zote ili kuwagawia maskini kufuatana na waliyoyasoma: ndio mwanzo wa jamaa. Tarehe 23 Aprili ndugu Egidi pia akajiunga nao, na mara wakatawanyika wawiliwawili wahubirie mikoa ya jirani. Ndipo wafuasi walipoongezeka na mwishoni mwa mwaka walifikia kuwa wanane.
1209 Kisha kurudi Asizi wanne wengine wakajiunga nao: hapo wakaamua waende wote Roma ili kupata kibali cha Papa Inosenti III kusudi wawe na hakika ya kuwa maisha yao yanampendeza Mungu, na waeleweke kwa wote kuwa ni Wakatoliki hasa, si wazushi. Baada ya kuvumilia muda fulani wakafaulu kuongea na Papa kwa msaada wa askofu wa Asizi na wa kardinali Yohane wa Mtakatifu Paulo: mara ya kwanza makardinali wengine walibishana na kutaka kupinga ombi hilo; lakini mara ya pili Papa alitoa kwa sauti kibali chake kwa maisha yao ya kitawa na kwa utume wao wa kuhubiri toba. Labda mwaka huohuo Fransisko alianzisha utawa maalumu kwa waamini wanaoishi katika mazingira ya kawaida ya ulimwenguni, waweze kufuata maisha ya Kiinjili kwa ukamilifu mkubwa zaidi.
1210 Jamaa, baada ya kuhama kibanda cha Rivotorto ili kukwepa ugomvi na mkulima mkorofi, walihamia moja kwa moja kwenye kanisa la mtakatifu Maria wa Malaika, ambapo pabaki kielelezo cha kudumu.
1211 Fransisko akaondoka kwa meli aende Sirya akawahubirie Waislamu, lakini safari ikaishia Croatia kutokana na dhoruba; hapo akarudi Italia.
1212 Usiku baada ya Jumapili ya Matawi mtakatifu Klara alitoroka nyumbani, akapokewa na Ndugu Wadogo kwa mienge, akanyolewa kitawa na Fransisko akavikwa kanzu. Baada ya muda akahamia kwenye kanisa la mtakatifu Damiano pamoja na mdogo wake mtakatifu Anyesi aliyemfuata utawani: ndio mwanzo wa utawa wa Mabibi Fukara, ambao wanaishi Kifransisko ndani ya monasteri katika sala na kazi za mikono, bila ya kutoka nje wala kufanya utume wowote.
1213 Alifunga Kwaresima nzima katika kisiwa cha ziwa Trasimeno, halafu akazawadiwa mlima La Verna.
1214 Fransisko aliondoka tena kupitia bara akawahubirie Waislamu wa Moroko, lakini njiani huko Hispania akapatwa na ugonjwa mkali akarudi Asizi, alipowapokea utawani wasomi kadhaa: baadhi yao wakashika kweli njia ya udogo, lakini wengine wakaja kuvuruga utawa kwa kutegemea mno akili yao.
1215 Novemba ulifanyika Mtaguso Mkuu wa IV wa Laterano, ambao Fransisko alihudhuria pamoja na maaskofu na wakuu wengine wa mashirika; labda ndipo alipofunga urafiki na mtakatifu Dominiko, mwanzilishi wa Utawa wa Wahubiri. Baadaye akajitahidi sana kutekeleza maagizo ya mtaguso huo.
1216 Siku mbili baada ya kifo cha Inosenti III makardinali walimchagua Honori III. Fransisko aliendelea kuzungukazunguka Italia kwa ajili ya utume.
1217 Mkutano mkuu wa Ndugu Wadogo ulipoamua wengine waende kuhubiri nje ya Italia kwa Wakristo na wasio Wakristo, Fransisko akaelekea Ufaransa lakini njiani akazuiwa na kardinali Hugolino akarudi Asizi. Kutokana na kutumwa bila ya maandalizi yoyote, ndugu wengi wakapatwa na matatizo mengi.
1218 Honori III alieneza hati yake maalumu ili kuwahakikisha maaskofu wote kuwa Ndugu Wadogo ni Wakatoliki hasa.
1219 Mkutano mkuu ulituma tena ndugu wakahubiri Injili kwa Wakristo na Waislamu. Hapo Fransisko mwenyewe akaenda kati ya Waislamu wa Misri: hakupenda mwenendo wa jeshi la Kikristo lililopigana nao, akatabiri kuwa watashindwa. Upande wake akaenda kumhubiria sultani, lakini kisha kuona hawezi kumuongoa wala kuuawa naye kishahidi akamuomba ruhusa ya kutembelea mahali patakatifu pa Palestina na Sirya.
1220 Tarehe 16 Januari huko Moroko Waislamu waliwaua ndugu Berardo na wenzake wanne waliokwenda kuwahubiria mpaka misikitini: ndio wafiadini wa kwanza wa Kifransisko. Mnamo Aprili au Mei Fransisko, alipopashwa habari za mageuzi ndani ya shirika huko Italia, akarudi kwa ufunuo wa Mungu ashike tena uongozi, lakini alipoona ugumu wa hali ya utawa, na ya kwamba wengi hawataki kumsikiliza tena, akamuomba Papa alipatie shirika kardinali Hugolino kama msimamizi na mkosoaji. Halafu katika mkutano mkuu akajiuzulu akamteua ndugu Petro Cattani aongoze jamaa kwa niaba yake.
1221 Kwa kuwa Petro Cattani kafa mapema tarehe 30 Mei ikambidi Fransisko amchague makamu mwingine, yaani ndugu Elia Bombarone, wakati wa mkutano mkuu uliohudhuriwa na wanashirika elfu tano na uliopata kuwa mkubwa kuliko yote hadi leo. Kwa kuwa walijitengenezea vibanda vya mikeka kutokana na wingi huo, mkutano unajulikana kama mkutano wa mikeka. Mungu alifanya wasikose chakula hata wengi wakashangaa kwa sababu hayakufanyika maandalizi yoyote. Pamoja na kuamua kupeleka ndugu katika nchi mbalimbali, mkutano huo ulipitisha kanuni ndefu iliyohitajika sana kwa sababu ya hali ya shirika, na hasa ongezeko hilo la ajabu. Lakini kanuni hiyo haikuthibitishwa na Papa kwa sababu fulani.
1222 Fransisko alizunguka sana Italia kwa ajili ya utume.
1223 Miezi ya kwanza alikwenda pamoja na ndugu Leo na ndugu Bonisyo kwenye mlima wa Fonte Colombo ili kuandika kanuni fupi na yenye mtindo wa kisheria zaidi kama alivyodaiwa. Upinzani wa ndugu Elia na wengineo ukashindwa katika mkutano mkuu wa Juni, hivyo kanuni ikapelekwa kwa Honori III ambaye akaithibitisha kwa maandishi tarehe 29 Novemba. Katika Misa ya usiku wa Noeli, iliyoadhimishwa huko Greccio katika pango lililoandaliwa na Fransisko, alitokea mtoto Yesu.
1224 Mnamo Julai ndugu Elia alijulishwa katika njozi kwamba Fransisko ataishi bado miaka miwili tu. Mnamo Agosti Fransisko akapanda mlima La Verna afanye mfungo mpaka sikukuu ya Malaika mkuu Mikaeli; huko upwekeni, akiwa katika malipizi na majaribu makali ya usiku wa roho, akatokewa na Yesu mwenye sura ya serafi msulubiwa akajaliwa mwilini madonda yake matano ya msalabani.
1225 Baada ya kurudi kutoka safarini mwezi wa tatu Fransisko alienda kwa mtakatifu Klara, ambapo akabaki mpaka mwezi wa tano kwa sababu ya ugonjwa na ya matibabu yasiyomsaidia kitu. Katika mateso hayo na majaribu ya Shetani, usiku mmoja akaahidiwa uzima wa milele. Kesho yake asubuhi akamshukuru Mungu kwa kumtungia Wimbo wa Ndugu Jua. Mwezi Juni akawapatanisha askofu na meya wa Asizi kwa kuwaimbishia wimbo huo baada ya kuuongezea ubeti kuhusu msamaha. Halafu akaenda kukaa Rieti kwa ajili ya matibabu mbalimbali aliyoyavumilia yote kwa moyo mkuu.
1226 Kuanzia tarehe 6 Februari alisafiri tena kwa matibabu. Mnamo Aprili huko Siena akazidiwa hata usiku fulani alikubali ombi la kuwaandikia ndugu zake wote wasia mfupi kwa maneno matatu, yaani kwamba wapendane, wafuate ufukara na kulitii Kanisa. Baada ya kupata nafuu akaandika sehemusehemu wasia mrefu zaidi ili kuchochea karama ya shirika. Waasizi wakiogopa kwamba mtakatifu wao atakuja kufa mbali wakafanya mpango wa kumrudisha kwao wakamlaza kwenye nyumba ya askofu, lakini Fransisko alipokaribia kufa akaamua kurudi kwenye kanisa la mtakatifu Maria wa Malaika. Katika hiyo safari yake ya mwisho, katikati ya njia, akabariki mji wake. Halafu kabla hajafa akawabariki wafuasi wake wote, hata wale watakaoingia utawani mpaka mwisho wa dunia. Halafu tena akaomba wamlaze ardhini kabisa bila ya nguo afe uchi kama Yesu msalabani tarehe 3 Oktoba; hapo sifa ya madonda yake ikaanza kuenea, na wengi wakaja kuyashuhudia katika maiti yake. Kesho yake, kwa maandamano ya shangwe pamoja na huzuni, akaenda kuzikwa katika
kanisa kuu, lakini njiani waliwapitia mtakatifu Klara na wenzake.
1227 Tarehe 19 Machi, baada ya kufa Honori III, kardinali Hugolino alichaguliwa kuwa Papa kama alivyotabiriwa na Fransisko akajichagulia jina la Gregori IX.
1228 Mwenyewe alikwenda Asizi kusudi amtangaze rafiki yake Fransisko kuwa ni mtakatifu mbinguni (16 Julai).
1230
Masalia ya Fransisko yalihamishiwa katika kanisa kubwa lililojengwa kwa heshima yake: ndio kanisa kuu la shirika lote.
Sala yake
[
hariri |
hariri chanzo]
Ndiwe Bwana Mungu mtakatifu unayetenda maajabu.
Wewe una nguvu. Wewe ni mkuu. Wewe ndiwe mkuu kabisa.
Wewe ndiwe mfalme mwenyezi.
Wewe, Baba mtakatifu, mfalme wa mbingu na nchi.
Wewe ni utatu na umoja, Bwana Mungu wa miungu; ndiwe wema, wema wote, wema mkuu, Bwana Mungu hai na wa kweli.
Wewe ni pendo, upendo; wewe ni hekima, wewe ni unyenyekevu, wewe ni uvumilivu, wewe ni uzuri, wewe ni upole, wewe ni usalama, wewe ni utulivu, wewe ni furaha na heri, wewe ni tumaini letu, wewe ni haki, wewe ni kiasi, wewe ni mali yetu yote ya kututosha.
Wewe ni uzuri, wewe ni upole, wewe ndiwe msimamizi, wewe ni mlinzi na mtetezi wetu, wewe ni nguvu, wewe ni burudisho.
Wewe ni tumaini letu, wewe ni imani yetu, wewe ni upendo wetu, wewe ni utamu wetu wote, wewe ni uzima wetu wa milele: Bwana mkuu na wa ajabu, Mwenyezi Mungu, Mwokozi mwenye huruma.
Sala iliyosambazwa kwa jina lake
[
hariri |
hariri chanzo]
Ee Bwana unifanye niwe chombo cha amani yako.
Palipo chuki nilete mapendo,
Palipo makosa nilete msamaha,
Palipo nshaka nilete imani,
Pasipo matumaini nilete tumaini,
Palipo giza nilete mwanga,
Palipo huzuni nilete furaha.
Ee Bwana unisaidie nitamani zaidi:
Kufariji kuliko kufarijiwa,
Kuelewa kuliko kueleweka,
Kupenda kuliko kupendwa.
Kwa kuwa:
Ni katika kutoa ndipo tunapopokea,
Ni katika kusamehe ndipo tunaposamehewa,
Ni katika kufa ndipo tunapozaliwa katika uzima wa milele. Amina.
SOMA UKISHINDWA KUELEWA KAMUULIZE MAREHEMU BABU YAKO