Wakatoliki, Fundisho la Kuomba Kupitia mnaowaita "Watakatifu", Mf Mtakatifu Francis, mlilitoaga wapi??

Wakatoliki, Fundisho la Kuomba Kupitia mnaowaita "Watakatifu", Mf Mtakatifu Francis, mlilitoaga wapi??

Kasome Church history vizuri hukusu christians persecution hadi kuibuka kwa mfalme Constantino hadi Roman catholicism.
Pia kasome Bible History vizuri kuhusu Septuagint ambayo ilikamilika miaka ya 250 BCE hata huo ukatoliki haukuwepo. Leo hii mtu kala maharage kashiba asasema maandiko yaliandikwa na wakatoliki!!!

Sawa! askofu wa JamiiForum
 
Miongoni mwa jamii yenye watu Bora , wastaarabu , wasomi , waliofanikiwa na ambao sio wanafki ni jamii ya wakatoliki...walokole wanafki sana waliookoka kwa asilimia mia ni wa kuhesabu sana, majungu wao kusengenyana kanisanj wao ..ulitaka kuishi vzr hata kwenye nyumba za kupanga au ujirani ishi na mkatoliki..walokole wakorofi wana uchungu na hasira za karibu san sababu wengi sababu za kuokoka ni historia mbaya na matatizo mabaya ya kwenye maisha
Ukweli 💯
 
Yaan kwamba hamsomi kabisa kabisa maandiko ?.

Mwanadamu Dunia amepewa jina Moja tu la kuombea chochote , nalo ni JINA LA YESU.

Unajiuliza , MTU aliyekufa, Kisha nyinyi wenyewe mliohai mkamuita "Mtakatifu", huyohuyo mnamuomba awaombee Kwa Mungu?.

Mbona ni wazi na suala la akili ndogo tu na huhitajiki kua na Uelewa mkubwa wa masuala ya kiroho ndo ujue kua Mfu Hana lolote alijualo Wala kulisikia wala Hana mawasiliano yoyote yale na Mungu .

Ukiristo wenu ni wa aina gan?
Ni rahisi kuzeeka na UONGO wa kuanzia utotoni
 
Tuachane na hayo ya Nyerere! Tuje kwenye hii hoja yako ya mwisho kuhusu Maria!!

Mary/Maria/Mariamu alikuwa ni mama wa Yesu! Na unafahamu Yesu kwenye biblia alitambulika kama Mwana wa Mungu/Masiya!

Je, ni kosa kumheshimu mama yake Yesu ambaye biblia inamtambua kama Mwana wa Mungu? Ninaamini pia wewe ni binadamu, na hivyo ulizaliwa na mwanamke! Je, ulipokuwa mdogo mahitaji yako yote ya msingi uliomba moja kwa moja kwa baba yako?

Na kama ulipitia kwa mama, shida iko wapi kwa sisi Wakatoliki tukiomba maombi yetu kupitia Mama wa Yesu ambaye ni Maria? Au na jambo kama hili nalo linahitaji kuwepo kwenye maandiko, au linahitaji tu akili ya kuzaliwa!! Au nyinyi ndiyo wale msiowaheshimu mama zenu?
Yesu tu hakumuita Maria "mama" alimwita "mwanamke" nyie hio dhana ya kumuita mama wa Mungu mmeitoa wapi?
 
Yesu tu hakumuita Maria "mama" alimwita "mwanamke" nyie hio dhana ya kumuita mama wa Mungu mmeitoa wapi?
Jibu kwanza hili swali; Kwa nini mnateseka mnapoona Kanisa Katoliki linamheshimu Maria, ambaye alikuwa ni mama yake Yesu? Je, wewe mama yako aliyekuzaa humheshimu?

Au nyinyi ndiyo wale watoto waliotelekezwa na mama zao mlipokuwa wadogo/baada tu ya kuzaliwa; na hivyo kushindwa kuutambua kabisa umuhimu wa mama!
 
Isaya 58:1 inatutaka tusiukalie kimya huu upotofu. Lazima tuwahubiri pale mnapokosea ili mziache njia zenu mbaya na mrejee kwenye ile kweli ya mafundisho ya Yesu Kristo.

Hatutakaa kimya kuwaambia waRC wanapokosea na kuwahubiria ile kweli, maana tukifanya hivyo siku tutayokwenda kukutana na Mungu wetu, tutautolea hesabu ukimya wetu.

Kuhusu kumuheshimu mama yangu, yeye ataheshimiwa kama yasemavyo maandiko na sio vinginevyo.
 
Mtakatifu ni 'official ghost'... Yaani wewe kama unaabudu mizimu basi ule mzimu ambao unajua fika kabisa kule ulipo upo sehemu salama na sahihi kulingana na matendo mema uliofanya wakati ukiishi hapa Duniani; ukiomba kupitia yeye utakusaidia kurahisisha na kuwaisha maombi yako.

Wewe pia unajua kwa namna babu yangu alivyokuwa mgaigai hata akifa hatoboi peponi, basi kwa Watakatifu ni kinyume chake.

Watakatifu ni zile roho zilizothibitika kuupata uzima wa milele.
Ukiomba Mungu na ukaamua kumtumia yeye, basi maombi yako yatafika na yeye atahakikisha na kusimamia unapata majibu.

Kwa kuwa kupata majibu hutegemeana na imani yako; basi atasimama na wewe kwenye majaribu na kuimarisha imani yako ili uyapokee majibu yako. Atakupa ishara ya kujikinga na shetwan ili wewe uweze kuinusuru roho yako.

Mfano ni baadhi ya watu waliokuwa wanaomba kupitia Mt. Rithaa wa Kashia na wametoa shuhuda kadhaa...
 
Isaya 58:1 inatutaka tusiukalie kimya huu upotofu. Lazima tuwahubiri pale mnapokosea ili mziache njia zenu mbaya na mrejee kwenye ile kweli ya mafundisho ya Yesu Kristo.

Hatutakaa kimya kuwaambia waRC wanapokosea na kuwahubiria ile kweli, maana tukifanya hivyo siku tutayokwenda kukutana na Mungu wetu, tutautolea hesabu ukimya wetu.

Kuhusu kumuheshimu mama yangu, yeye ataheshimiwa kama yasemavyo maandiko na sio vinginevyo.
Huna uwezo wa kuikosoa RC. Na hata ukiikosoa, bado utakuwa unapiga tu makelele. Hakuna Mkatoliki anayepoteza muda wake kuwasikiliza nyinyi Wakatekumeni msio ifahamu imani ya Kanisa Katoliki.

By the way, sikio kamwe haliwezi kuzidi kichwa. Na siku zote mkubwa atabakia kuwa mkubwa tu.
 
wakati nasoma hiyo mistari katika Biblia nikaja kugundua Watakatifu kuwaomba sio tatizo kwa kuwa wanafanyakazi kwa karibu na maagizo ya Mungu kuanzia mfalme Nebukadreza walimtokea kwa ndoto lakini Yesu akiwa akiwa katika maombi nao walimtokea na kuzungumza nao na walikuwepo tangu zamani

Daniel Sura 4-17.Hukumu hii imekuja kwa agizo la walinzi, na amri hii kwa neno la watakatifu; kusudi walio hai wapate kujua ya kuwa Aliye juu anatawala katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, tena humtawaza juu yake aliye mnyonge.
18 Mimi, Nebukadreza, nimeiona ndoto hii; na wewe, Ee Belteshaza, eleza tafsiri yake, kwa maana wenye hekima wote wa ufalme wangu hawawezi kunijulisha tafsiri yake; bali wewe waweza, maana roho ya miungu watakatifu inakaa ndani yako.
Luka Sura 9.Haya 29
Ikawa katika kusali kwake sura ya uso wake ikageuka, mavazi yake yakawa meupe, yakimeta-meta.
30 Na tazama, watu wawili walikuwa wakizungumza naye, nao ni Musa na Eliya;
31 walioonekana katika utukufu, wakanena habari za kufariki kwake atakakotimiza Yerusalemu.
 
Huna uwezo wa kuikosoa RC. Na hata ukiikosoa, bado utakuwa unapiga tu makelele. Hakuna Mkatoliki anayepoteza muda wake kuwasikiliza nyinyi Wakatekumeni msio ifahamu imani ya Kanisa Katoliki.

By the way, sikio kamwe haliwezi kuzidi kichwa. Na siku zote mkubwa atabakia kuwa mkubwa tu.
Anayewakosoa sio mimi ila ile roho ya Mungu itendayo kazi ndani yangu kupitia neno lake. Mkiamua kusikia sawa mkiamua kukaidi sawa pia. Maandiko yanasema mnao uhuru wa kuchagua mtakayemtumikia (Yoshua 24:15).
 
Huna roho yoyote ya Mungu ndani yako! Wewe una roho ya ujinga tu.
 
Huna roho yoyote ya Mungu ndani yako! Wewe una roho ya ujinga tu.
Mbona unanishusha viwango mkuu, mimi nina zaidi ya roho ya ujinga, yaani roho ya upumbavu katika neno la Yesu Kristo. Kwani wewe haujui upumbavu katika neno linalohubiriwa ndio Roho ya Mungu yenyewe? BTW najadili vitu vizito sana na mtu empty katika scriptures; ila wacha nikupe hii ikufungue ubongo kidogo.

1 Wakorintho 1:21
Kwa maana katika hekima ya Mungu, dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upumbavu wa lile neno linalohubiriwa.

For after that in the wisdom of God the world by wisdom knew not God, it pleased God by the foolishness of preaching to save them that believe.
 
Back
Top Bottom