'Wakatoliki' Parokia ya Yombo Dovya wapanda miti kusherekea Birthday ya Samia

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Bandugu naona Wakatoliki wa kuchaji wanaendelea kufanya yao. Leo wameshiriki kwenye zoezi la kupanda miti
============
Jumuiya ya Mtakatifu Yohana Parokia ya Yombo Dovya wameungana na kushiriki zoezi la upandaji wa miti katika kata ya Makangalawe Wilayani Temeke ikiwa ni sehemu ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt . Samia Suluhu Hassan katika siku yake ya kuzaliwa .

Wakizungumza baada zoezi hilo la upandaji wa miti lililoambata na ukataji wa keki , wamesema kuwa wameamua kujitokeza katika kushiriki zoezi hilo kwa lengo la kuunga mkono Rais Samia ni kutokana na kazi kubwa na nzuri inayofanya na Dkt Samia kwa Wananchi wake .

Pia wamemtska rais Dkt Samia asitetereke katika uongozi wake , aongoze vyema , asimame kama mwanamke na aendelee kuwaongoza .

Your browser is not able to display this video.
 
Ukielewa tofauti habari kama hizi hazitakusumbua
Kuna Wakatoliki ambao ni wale unaowajua siku zote akina Kitima etc

Kuna Wakato-link ambao ni hawa wanapanda miti na kuandika barua Vatican kwa maandamano.

Kuna tatizo gani Wakatolink wakipanda miti katika siku yao?
 
Huyu mama hata kama anamsapoti Mama Samia hakupaswa kuongea mbele ya umma. Kwanz hakuna mkatoliki anayebeba hii biblia ya kiprotestanti. Pia kakosea kutaja jina la jumuiya yake na mwisho kamaliza kwa kusema "kwa jina la baba mtakatifu".

Kama kuna kiongozi wa CCM yuko nyuma ya haya mambo aache kwa sababu hayana faida kwa chama zaidi ya kukichafua chama.

View: https://www.instagram.com/reel/DUBgb8Witud/?igsh=MXU5aWtqeDEwMHV5dA==
 
Huko tz mbona kuna watu waajabu ajabu?
 
Sioni Mkatoliki hapo; naona genge la malofa tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…