Wakazi: Niliwahi kulala kwenye gari miezi miwili baada ya kufukuzwa home

Wakazi: Niliwahi kulala kwenye gari miezi miwili baada ya kufukuzwa home

Jamaa yaan umeondoka home na lak 9 in two Month equivalent to 15k per day na huku una gari la baba,na bado unaeeza kuomba hela kwa ndgu na jamaa ,alaf unajifanya kuwa umelala njee ya home,daah wakishua bhana,wenzako ndio wamepga msoto wa kutoshaa
Mmeshangaaa saña ujue[emoji1][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38] mshahara wa MTU wa miezi mitatu minne kabisaa hukooo
Kaahhhh
 
Huyu ni mpumbavu pro max nimepewa gari na nyongeza hela ya mafuta pia.
Unalalaje kwenye gari.
Unapiga taxi bubu hela mafuta unayo,chumba kimoja kino pale mnyamala ilikua buku 15-20 kipindi hicho.
Kaenda US kashapoteza miaka ya kutosha karudi hana kitu.
Kurap hajui kadandia tu,
Inawezekana kabisa karudi kwa wazazi tena kulialia.
Pumbavu kabisa,
Baba alikua sawa kufukuza hiki kirusi
 
Liongo hilo jamaa. Anataka kuiga story za mastaa wa marekani kusema kuwa wamelala kwenye gari.
Kibongo bongo haiingii akilini ulale ndani ya gari huku ukiwa na laki 9 mfukoni.

Halafu mzazi gani kibongo bongo anakufukuza na anakupa na gari kabisa.

Lingetafuta uongo mwingine ili aonekane kapigika sio huo uongo wa maigizo yasio na uhalisia.
Umeongea kweli
 
Eti kwenye,watu wamelala beach miaka,watu wanalala koridor za wahindi miaka, kwenye madaraja, mashuleni,makanisani watu wanalala sembuse sofa za gari.
Eti wali maharage,watu wanapiga deshi au wanawinda kwenye misiba ndio wale
 
Rapa namba mbili nchini amesema hamna wakati mbaya ambao hawezi kusahau maishani mwake Kama siku alipofukuzwa nyumbani kwao.

Amesema hayo alipokuwa akiongea na mtangazaji gwiji Jabir Saleh.

" Nilizinguana na mshua nilipomaliza form 4, baba akaniambia niondoke home, kwa hiyo nilichofanya nilichukua gari ya home, nikalilia kwa maza akanipa Kama laki 9 then nikaamsha, kwa miezi miwili mfululizo nilikuwa nalala kwenye gari nashindia wali maharage mtaani, life ilikuwa tafu Sana.

Nashangaa madogo kwenye game wanajifanya Wana street cred halafu hawajawahi hata kuishi nje ya maskani kwa wiki moja,nawashangaa Sana".

Wakuu yapi maoni yenu.
Unakula wali maharage halafu unalalamika? Una 900k plus gari, ...natamani kujua huyu kichaa anatokea familia gani?
 
Saa ndio nini. Amepewa laki 9 na gari juu kaondoka nalo.
Watu wanaondoka hata mia mbovu hawana.
Huyu ni sawa na watoto wa kishua wanaosema wameteseka sana kwa kunywa chai ya rangi. Si bora yeye alikuwa analala kwa gari. Watu wanalala stand tu daily
Ndio hapo watu tumeuza Big G na karanga stendi tuna miaka 10+ mpk kufika 14 mtu unajua kila kitu hata mtu mzima hawezi.
Alafu kuna bwege anapewa gari na hela ya kutosha
Analalama hapa.
Mkurya gani msengerema namna hii
 
Mtu anaingia Dar Hana 50, Hana ndugu Hana pa kulala na anatoboa Huyo ndo mwanaume asimame atambe...hata wenzake eatabaki kusema Mwamba tumekupa maua yako upewe gari na lk 9 juu[emoji41][emoji1745][emoji16][emoji39][emoji39][emoji119][emoji119][emoji119]jamaa aache kutuleta..
 
Liongo hilo jamaa. Anataka kuiga story za mastaa wa Marekani kusema kuwa wamelala kwenye gari.

Kibongo bongo haiingii akilini ulale ndani ya gari huku ukiwa na laki 9 mfukoni.

Halafu mzazi gani kibongo bongo anakufukuza na anakupa na gari kabisa.

Lingetafuta uongo mwingine ili aonekane kapigika sio huo uongo wa maigizo yasio na uhalisia.
Ukumbuke wakazi kweli ni wakishua hasa, huyo ni mtoto wa steven wasira kigogo wa CCM na waziri miaka mingi
 
Jamaa yaani umeondoka home na laki 9 in two Month equivalent to 15k per day na huku una gari la baba, na bado unaeeza kuomba hela kwa ndugu na jamaa, halafu unajifanya kuwa umelala njee ya home, daah wakishua bhana, wenzako ndio wamepiga msoto wa kutoshaa
Hayuko siriaz na Maisha huyu.!
 
Rapa namba mbili? Sidhani hata kama yupo top 50 maana sijawahi kupenda wimbo wake hata mmoja. Anachofanya ni kuforce kurap kwakuwa kakulia katika life la kisela
 
Jamaa wa kishua, halafu anabeza jitihada binafsi za akina Mond. Hakuna msoto hapo, mtu una laki 9 halafu vilevile unalala kwenye gari... unasema umesota?

Aache kuigiza.
Na hapo ukumbuke laki9 ya mwaka 2010 kushuka chini ni sawa na million 5 ha9 kwa sasa, miaka hiyo Madaktari wa Muhimbili wanagoma walikuwa wanalipwa laki 3 Walimu Akianza kazi shule ya Msingi analipwa 144,000/, Sahani ya ubwabwa kwa Mama lishe ilikuwa 5,00/ chipsi yai ilikuwa 7,00/ Soda zilikuwa 300/ Grand malta 500/ nauli kutoka Mwanza hadi Dar ni 20,000 saizi ni 65,000 hadi 120,000/ bajeti ya nchi ilikuwa Trilioni 10 leo ni Trillioni 40+ na baadhi ya Wizara bajeti yake ya Mwaka ilikuwa haifiki hata billioni 5,Tajiri wa kwanza Duniani alikuwa na $40 billioni tu wakati saiz ana $200+billioni
Miaka hiyo Dollar 1 ilikuwa sawa na 1,100 hadi 1,200 saizi ni 2,600/, Miaka hiyo idadi ya Magari yaliyokuwepo nchini toka uhuru yalikuwa chini ya Laki 4 kati ya Watanzania Millioni 30 na baba yake akiwemo.
Aache utani kwenye Masihara.!
 
Rapa namba mbili nchini amesema hamna wakati mbaya ambao hawezi kusahau maishani mwake Kama siku alipofukuzwa nyumbani kwao.

Amesema hayo alipokuwa akiongea na mtangazaji gwiji Jabir Saleh.

" Nilizinguana na mshua nilipomaliza form 4, baba akaniambia niondoke home, kwa hiyo nilichofanya nilichukua gari ya home, nikalilia kwa maza akanipa Kama laki 9 then nikaamsha, kwa miezi miwili mfululizo nilikuwa nalala kwenye gari nashindia wali maharage mtaani, life ilikuwa tafu Sana.

Nashangaa madogo kwenye game wanajifanya Wana street cred halafu hawajawahi hata kuishi nje ya maskani kwa wiki moja,nawashangaa Sana".

Wakuu yapi maoni yenu.

Achana nae wakishua huyo
 
Back
Top Bottom