Wakazi: Niliwahi kulala kwenye gari miezi miwili baada ya kufukuzwa home

Wakazi: Niliwahi kulala kwenye gari miezi miwili baada ya kufukuzwa home

Mi nilifukuzwa nikaondoka na pakti mbili za mahindi makavu ya kukaanga (sio popcorn).Nikawa nalala juu ya mnara wa Voda.
 
Nakumbuka Kipindi cha Mkasi, Salama anamhoji Mimi Mars anamuuliza vipi umeshawahi kupitia msoto, yeye anashangaa anajibu "Msoto Ndio Nini?"...
 
Watu tumeondoka makwetu na mabumunda ya mama na maji unaambiwa utapata tu huko mbele, panda lift ya jirani tukaingia mtaani kuhustle.
enhee,

na wewe aliyekufukuza ni nani na aliyekupa mabumbunda ya mama ni nani, na aliyeku wish well kwamba utapata mbele ni nani, mamaako ?

sawa mgumu, tumesikia
 
Kuna yule binti kasema yeye kwao Singida ila hajawahi kufika,na hataenda hadi kuwe na uwanja wa ndege,hawezi safiri na basi.
 
Comment za watu zinaeleza sana background zao [emoji4][emoji16]
Ndipo wanamtolea hasira Wakazi wa Watu masikini!!![emoji1][emoji1][emoji1]Kila mtu ana background tofauti na sidhani km kakosea Wakazi
 
Kula wali waharage ni ishara ya life gumu?
Huyu atakuwa hajasoma shule zetu za kula Ugali Maharage mwaka kzima
 
Yaani unafukuzwa home na hela na gari, dah wakishua aisee, huyu itakua walimlazimisha amalize chakula akasusa.

BTW, alikuja na ile Bigijii yake studio.
Wakishua afu anaish STAKISHARI🤣😂
 

Rapa namba mbili nchini amesema hamna wakati mbaya ambao hawezi kusahau maishani mwake Kama siku alipofukuzwa nyumbani kwao.

Amesema hayo alipokuwa akiongea na mtangazaji gwiji Jabir Saleh.

" Nilizinguana na mshua nilipomaliza form 4, baba akaniambia niondoke home, kwa hiyo nilichofanya nilichukua gari ya home, nikalilia kwa maza akanipa Kama laki 9 then nikaamsha, kwa miezi miwili mfululizo nilikuwa nalala kwenye gari nashindia wali maharage mtaani, life ilikuwa tafu Sana.

Nashangaa madogo kwenye game wanajifanya Wana street cred halafu hawajawahi hata kuishi nje ya maskani kwa wiki moja,nawashangaa Sana".

Wakuu yapi maoni yenu.
Kabla ya kujadili alichokisema, Hicho cheo cha RAPA NAMBA 2 nani kampa?
 
Liongo hilo jamaa. Anataka kuiga story za mastaa wa Marekani kusema kuwa wamelala kwenye gari.

Kibongo bongo haiingii akilini ulale ndani ya gari huku ukiwa na laki 9 mfukoni.

Halafu mzazi gani kibongo bongo anakufukuza na anakupa na gari kabisa.

Lingetafuta uongo mwingine ili aonekane kapigika sio huo uongo wa maigizo yasio na uhalisia.
Ame copy na ku edit stori ya Rick Ross kwenye kitabu chake The Perfect day to Boss Up amesahau tu kusema alienda club kwenye show akapiga mtungi akamuachia rafiki yake aendeshe gari yeye akalala kushtuka washakula mzinga. 😂😂

Anyway mtoto wa mama alikuwa na 900k ya kipindi hicho ambach probably kwa sasa ni equal to 1M+
 
Back
Top Bottom