A
Anonymous
Guest
Mimi ni mkazi wa Chalinze, Mtaa wa Nero, Darful. Tunaendelea kukabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji mara kwa mara. Wakati mwingine tunakaa hadi mwezi mzima bila kupata maji.
Hadi ninapoandika malalamiko haya, tumekaa takribani wiki mbili bila maji, bila kupewa taarifa yoyote kutoka Idara ya Maji kuhusu sababu ya kukosekana kwa huduma hiyo au lini itarejea.
Kinachotushangaza zaidi ni kwamba mitaa mingine inapata maji wakati sisi tunaendelea kukosa huduma hiyo muhimu.
Tunaomba mamlaka husika itupazie sauti na ichukue hatua za haraka kuhakikisha huduma ya maji inarejea katika eneo letu. Wananchi tunahitaji maji kwa ajili ya matumizi ya kila siku.