Ms Billionaire
JF-Expert Member
- Jul 18, 2020
- 2,452
- 4,955
Nawasalimu kwa Jina la Jamhuri. Kazi iendelee.
Mama Samia, wakazi na wapiga kura wako wa Goba njia ya Tegeta A kwenda kutokea Madawa na njia Tegeta A kuelekea Kulangwa kupitia makanisa ya Katoliki Tegeta A, na Anglikana Tegeta A tuna changamoto kubwa sana ya barabara haitaki kutatuliwa kwa miaka mingi sasa.
Ile njia ni mbovu sana na wakazi wa maeneo hayo waliwahi kumfuata Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa Kumwomba awasadie kupambania kibali cha kurekebisha barabara walichojibiwa na serikali ya mtaa ni hivi: “HIYO SIYO KAZI YENU”
Ikaja kugundulika kwamba ile njia inamwingizia faida kubwa mwenyekiti ya serikali ya mtaa wa Goba Tegeta A kwasababu ana mradi wake wa Bajaji. So anajua akikubali barabara itengenezwe itafanya madaladala yapite kule na yeye atapoteza mradi wake wa Bajaji.
Wakazi wa Tegeta A na Kulangwa tunahitaji karavati kwenye makazi yetu. Mbunge na diwani wamenyamaza labda tukikuomba wewe mama utawakumbusha wajibu wao.
Tunateseka na hiki kipindi cha mvua school bus zinapita na watoto wetu ni hatari sana sehemu zingine karavati zimebomoka kabisa mfano hii njia karibu na kituo cha afya cha Mtakatifu Yohanne Goba Kulangwa njia ni mbovu sana na viongozi wa serikali za mtaa hawataki kutengeneza hiyo njia kwa sababu wanajua watakosa mapato ya miradi yao ya bajaji na pikipiki.
Mama samia tunaomba msaada wa njia hizo kuerekebishwa tuwekewe Karavati tukiwafuata viongozi wa serikali za mtaa hawatoi ushirikiano kwasababu hawataki kupoteza mapato yao ya Bajaji na bodaboda.
Nimeambatanisha ramani ya Goba Kulangwa inayopakana na Tegeta A ambayo inaenda kutokea St. Yohane Health Center kwenda kwenye makazi.
Viongozi, hapo nlipoweka alama nyekundu kuna mto unapita, Karavati limebomoka upande na school bus za watoto wetu zinapita hapo kila siku na watoto. Tunaogopa watoto wasije kusombwa na maji tunaomba serikali kuu itusaidie kama serikali tunazoishi nazo mtaani hazina msaada. TUNAOMBA KARAVATI ENEO HILO. Na tunaomba hizo njia zirekebishwe kwasababu zimechimbika sana kwasababu ya mvua.
Cc Mbunge wa Ubungo, Diwani wa Goba kulangwa, serikali ya mtaa Goba kulangwa na Tegeta A.
Nawasilisha.