KERO Wakazi wa Goba njia ya Tegeta A kwenda Madawa na Kulangwa tuna changamoto kubwa ya Barabara

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Chaguzi za serikali za mitaa ni mwaka huu oktoba
 
Tutabanana nao mwaka huu hadi kieleweke. Huyu wangu anajifanya mjuaji akae kwa kutulia uchaguzi wao wa serikali za mitaa mwaka huu lazima kichafuke na mwakani mbunge lazima ajipange. Watanyooshana wenyewe.
 

Andika yaliyo ya kweli na siyo majungu yako hayo.

Mwenyekiti wa Tegeta A ni kiongozi mzuri sana.

Pamoja na changamoto za kimiundombinu huko Tegeta A, lakini yule jamaa ni msikivu sana na anapambana.

Ninakumbuka zamani Tegeta A haikuwa na Kituo cha Polisi lakini sasa hivi kipo.

Pia usalama wa raia ulikuwa mdogo lakini sasa hivi kuna afadhali kubwa.

Angalau hizi changamoto zingeletwa na mtu anayeijua Tegeta A basi.

Sasa mleta taatifa mwenyewe ni Guantanamoh 😂😂
 
Tutabanana nao mwaka huu hadi kieleweke. Huyu wangu anajifanya mjuaji akae kwa kutulia uchaguzi wao wa serikali za mitaa mwaka huu lazima kichafuke na mwakani mbunge lazima ajipange. Watanyooshana wenyewe.
Sasa kama humjui mbunge wako, huyo mbunge unayetaka kunuwajibisha ni yupi?

Bila shaka hata mwenyekiti wa Mtaa humjui. Unatia aibu!
 
Sasa kama humjui mbunge wako, huyo mbunge unayetaka kunuwajibisha ni yupi?

Bila shaka hata mwenyekiti wa Mtaa humjui. Unatia aibu!
Wewe andika yote ila message sent and delivered. Tukutane october 2024 na waambie hao wenzio. Huto tuvyeo twenu hatusumbui mtu. Mi sina mda wa kukaa eti nigombanie uenyekiti wa serikali ya mtaa? Seriously? Muwe wajibikaji. Kumjua mbunge kunanisaidia nini kama hatatui matatizo ya eneo langu: MWENYEKITI WA SERIKALI YA MTAA WA GOBA TUMEKUJUA JIKESEHE UNAVYOJIKESHA ILA CARAVAT MTAWEKA NA MSIPOWEKA TUTAPELEKA USHAHIDI WA MRADI WENU WA BAJAJI KWA MAMA SAMIA
 

Ninaona umehama Mtaa wa Tegeta A sasa upo Mtaa wa Goba.

Hivi unajielewa kweli?

Ikiwa humjui hata Mbunge wako basi tatizo ni wewe na siyo huyo Mbunge.

Sasa jibu lako hili limethibitisha kwamba umetumwa kuja kusema uongo humu.

Sasa hilo la Mradi wa Bajaji linakuhusu nini?

Unataka kiongozi asiwe na mradi? Awe masikini kama wewe unayelipwa hela kidogo unakuja kuandika ubabaishaji humu?

Kwamba taatifa imefika; sasa umemletea nani humu anayehusika na mada zako zisizoeleweka?
 

Pole
 
Pole sana,unakopeleka malalamiko hawana habari na wewe,mama anaupiga mwingi mitano tena
 
Mnawaonea tu.. wenyeviti hao hawana mishahara wanategemea hela za ninyi mnpoaenda kuandikiwa barua zenu .. wakati ndiye wafu muhimu kwenye mtaa
Bora umueleze mkuu. Hawa watu hawajui majukumu ya viongozi. Kila kiongozi anawafanya sehemu yake na akishamaliza inakuwa basi ni kusubiri.
 
Msijitetee bila sababu za msingi. Nyinyi mna uwezo wa kutoa vibali watu wajitengenezee barabara kwa juhudi zao lakini mnawakwamisha ili miradi yenu isife. Huo ni ujinga
Wewe ndiye mjinga kwa sababu hujui unabishana na nani, na hujui unabishania nini; una upeo finyu kiasi kwamba hujui hata Wilaya yako ni ipi!
 
Matatizo hayo ya barabara kwenye eneo hilo analolalamika mdau ni kweli yapo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Matatizo yapo ila namna anavyoyaeleza siyo sahihi.

Kwanza hajui eneo husika lipo Wilaya gani.

Anasema sababu ya ubovu wa barabara ni mradi wa babaji wa viongozi ambao wanataka barabara iwe mbovu ili daladala zisipite na bajaji zipate abiria.

Pia anadai mimi ni kiongozi wa huko.

Mimi kama mwenyeji wa huko, pia ni mtaalamu na biashara ya bajaji ninapingana na anayoyaeleza kwa maana kwamba si kweli kwamba bajaji inahitaji barabara mbovu.

Pia mimi siyo kiongozi wa huko na wala sina maslahi yeyote kwenye siasa za Tegeta A, japo ninapajua vizuri.

Nimemjaza na yeye kajaa!
 
Nimekuelewa mkuu, asubuhi njema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa Mbezi Msumi kuna issue kama hiyo hiyo. 👍
 
HAMEN TU SHIDA NN IF U CANT THEM JOIN THEM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…