KERO Wakazi wa Isevya – Muhimbii (Dar) tunaathiriwa na vumbi la barabara iliyotelekezwa

KERO Wakazi wa Isevya – Muhimbii (Dar) tunaathiriwa na vumbi la barabara iliyotelekezwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Sisi ni Wakazi wa Mtaa wa Isevya, Muhimbili – Ilala, Dar es Salaam. Kuna kipande cha barabara kimefukuliwa kwa zaidi ya miezi miwili sasa. Baada ya kufukuliwa walimwaga kokoto mara moja tu, tangu hapo hakuna kilichofanyika.

Kwa sasa tunaoga vumbi kama maji 😔Watoto, wazee na wagonjwa tunaumwa mafua na kikohozi kila siku. Ni eneo muhimu lenye shughuli nyingi lakini hali ni mbaya sana.

Tumejaribu kuvumilia na kutoa taarifa bila mafanikio. Tunaamini kwa nguvu ya JF sauti yetu inaweza kuokoa afya na maisha ya wananchi 🙏
 
Back
Top Bottom