KERO Wakazi wa Kongowe na Misugusugu tunateseka na harufu kali kutoka kiwanda cha pombe

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wakazi wa Kongowe na Misugusugu, Kibaha, tumekuwa tukikabiliwa na changamoto ya harufu kali inayotoka katika kiwanda cha pombe kilichopo Misugusugu.

Harufu hiyo hujitokeza zaidi kati ya saa 7 na saa 9 usiku, wakati ambapo wananchi wengi wanakuwa wamepumzika. Hali hii inatukosesha utulivu na kutuathiri katika maisha yetu ya kila siku.

Awali, tulilalamikia tatizo hili na kiwanda kilitozwa faini, jambo lililopelekea hali hiyo kutoweka kwa muda. Hata hivyo, kwa sasa harufu hiyo imeanza tena, na tunalazimika kuvumilia usumbufu huo usiku.

Tunaomba mamlaka husika zifuatilie suala hili na kuhakikisha kiwanda kinachukua hatua za kudumu kudhibiti harufu hiyo ili kulinda afya na ustawi wa wakazi wa Kongowe na Misugusugu.
 
Halafu kuna watu wanajiita NEMC na PCCB katika vitu vya kufuta nchi hii ni hao, sijawahi kuona wanachofanya
 
Harufu ya bia hata haiboi mbona

Ushawahi kuishi karibu na mskiti wewe? Yaan kila muda wanafungulia speaker afu wanaanza kuongea kiarabu hata km ni saa kumi usiku 😁
 
Back
Top Bottom