Wakazi wa Mbeya mjini wasipodhibitiwa watajenga hadi juu ya Kawetere, matokeo yake si mazuri baadae

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
8,308
Reaction score
12,812
Wakuu,
Kuna jambo la muda mrefu linanipa wasiwasi sana kuhusu namna mji wa Mbeya unavyokua.

Sasa hivi ukipita maeneo mbalimbali utakuta kila kona kuna ujenzi, mara nyingi bila mpangilio wa mji.

Wengine wameanza hata kupanda kuelekea Kawetere, eneo ambalo kiasili ni mlima wenye vyanzo vya maji na mandhari ya kipekee.

Swali kubwa: tukiruhusu hali hii iendelee bila udhibiti, nini kitatokea baada ya miaka 10–20?

🔹 Madhara ya mazingira: Uharibifu wa vyanzo vya maji, mmomonyoko wa udongo, na hatari ya maporomoko ya ardhi.
🔹 Madhara ya kijamii: Kukosekana kwa huduma za msingi kama barabara, maji na mifumo ya taka kwa sababu maeneo hayakupangwa.
🔹 Madhara ya kisheria: Baadaye serikali inaweza kuamuru bomoabomoa, jambo linaloleta hasara kubwa kwa wananchi.

Kwa sasa inavyoonekana, jitihada za kupanga mji hazilingani na kasi ya watu kujenga hovyo.

Hali hii ikiachwa iendelee, Mbeya inaweza kupoteza hadhi yake ya kipekee na kubaki ni mji usiopangika wenye changamoto nyingi za kimaisha. Uholela huu upo hata kwenye mpangilio wa usafiri katikati ya mji. Stendi ya Kabwe nayo ni kama haipo sababu yeyote pale anafanya lolote wakati wowote (magari binafsi kuegesha,soko mjinga,bajaji, daladala vyote vimetapakaa stendi ya Kabwe)

Ushauri wangu:
Serikali za mitaa, mamlaka ya ardhi na mji, pamoja na wananchi wenyewe, wanapaswa kushirikiana kupanga, kudhibiti na kutekeleza sheria za mipango miji.

Vinginevyo kizazi kijacho kitakuja kulalamika kwa makosa tuliyoyafanya leo.

Kwa sasa ni mara 100 uende ukaishi Tukuyu uwe unakuja kufanyia kazi Mbeya mjini. Mji umekuwa kero vibaya sana as if hakuna uongozi.
 
nchi ikiongozwa bila kufuaa Sheria kikamilifu , huwa ni taabu sana huku morogoro vyanzo vya maji vyote vimevamiwa na wakulima na wafugaji. Hata tanga napo pameharibika sana.

Mkoloni UK alijizuia yeye na wananchi wasiharibu mazingira, lakini ulipo kuja Uhuru, ikiwa ni uhuru wa manyani.

Waafrika ni kama Bado kujitambua na kujitawala
 
Tuna tatizo pahala sio bure. Kuna wakati unajiuliza kwanini tuna Wizara ya Ardhi na maofisi ya mipango miji, hawa wanafanya nini miji karibia yote ujenzi holela ni tatizo kubwa sana. Na hili sio la kuwalaumu wananchi Bali wasimamizi, what are they doing!
 
Mkoloni miaka zaidi ya 60 iliyopita aliweza kupanga miji. Mji ukipangwa hata umasikini unapungua.
Nyerere alikaa zaidi ya miaka 20, lakini jiji la Dar es salaam akaliongoza kisiasa,
Wewe imagine kama mu UK angekuwepo mpaka 90's ivi Tanganyika ingekuwa mbali sana kiuchumi na mashuleni gavo watoto wangebonga ngeli.

Huwezi kuwa mzalendo bila kuwa na maarifa sahihi ya kiuchumi
 
Na hapo ukifuatikia utakuta n viongozi wa CCM wahusika wa ugawaji wa maeneo hayo,
CCM ya Nyerere ni takataka kabisa
 
Tuna tatizo pahala sio bure. Kuna wakati unajiuliza kwanini tuna Wizara ya Ardhi na maofisi ya mipango miji, hawa wanafanya nini miji karibia yote ujenzi holela ni tatizo kubwa sana. Na hili sio la kuwalaumu wananchi Bali wasimamizi, what are they doing!
Acha watu wawe huru,fitna zimezidi
 
Nyerere alikaa zaidi ya miaka 20, lakini jiji la Dar es salaam akaliongoza kisiasa,
Wewe imagine kama mu UK angekuwepo mpaka 90's ivi Tanganyika ingekuwa mbali sana kiuchumi na mashuleni gavo watoto wangebonga ngeli.

Huwezi kuwa mzalendo bila kuwa na maarifa sahihi ya kiuchumi
Hili li shithole muingereza alifaa kuendelea kutawala mpaka leo kabisa ,naunga mkono hoja yako .Tamaa ya ngedere wachache kuongoza wakati qualities za uongozi hamna ndio iliyopelekea huu upuuzi na kutufikisha hapa tulipo .
 
Alafu akaleta sera za ujamaa ,zilikuja kuwapokonya wapigania uhuru na wazawa Haki ya kumiliki uchumi wao wa TZ, hili lilikuwa kosa kubwa sana ,

Leo hii uchumi wa TZ unamilikiwa na wahindi na waarabu. Tunachekwa kwa kweli

Alikuwa ni mzalendo asiyejua mbinu za kujenga uchumi imara na wakisasa utakao dumu vizazi na vizazi
 
Wakuu,
Kuna jambo la muda mrefu linanipa wasiwasi sana kuhusu namna mji wa Mbeya unavyokua.

Sasa hivi ukipita maeneo mbalimbali utakuta kila kona kuna ujenzi, mara nyingi bila mpangilio wa mji.

Wengine wameanza hata kupanda kuelekea Kawetere, eneo ambalo kiasili ni mlima wenye vyanzo vya maji na mandhari ya kipekee.

Swali kubwa: tukiruhusu hali hii iendelee bila udhibiti, nini kitatokea baada ya miaka 10–20?

🔹 Madhara ya mazingira: Uharibifu wa vyanzo vya maji, mmomonyoko wa udongo, na hatari ya maporomoko ya ardhi.
🔹 Madhara ya kijamii: Kukosekana kwa huduma za msingi kama barabara, maji na mifumo ya taka kwa sababu maeneo hayakupangwa.
🔹 Madhara ya kisheria: Baadaye serikali inaweza kuamuru bomoabomoa, jambo linaloleta hasara kubwa kwa wananchi.

Kwa sasa inavyoonekana, jitihada za kupanga mji hazilingani na kasi ya watu kujenga hovyo.

Hali hii ikiachwa iendelee, Mbeya inaweza kupoteza hadhi yake ya kipekee na kubaki ni mji usiopangika wenye changamoto nyingi za kimaisha. Uholela huu upo hata kwenye mpangilio wa usafiri katikati ya mji. Stendi ya Kabwe nayo ni kama haipo sababu yeyote pale anafanya lolote wakati wowote (magari binafsi kuegesha,soko mjinga,bajaji, daladala vyote vimetapakaa stendi ya Kabwe)

Ushauri wangu:
Serikali za mitaa, mamlaka ya ardhi na mji, pamoja na wananchi wenyewe, wanapaswa kushirikiana kupanga, kudhibiti na kutekeleza sheria za mipango miji.

Vinginevyo kizazi kijacho kitakuja kulalamika kwa makosa tuliyoyafanya leo.

Kwa sasa ni mara 100 uende ukaishi Tukuyu uwe unakuja kufanyia kazi Mbeya mjini. Mji umekuwa kero vibaya sana as if hakuna uongozi.
Siyo mbeya tu hiyo hali ipo TZ nzima
 
Tanzania kila mahali ni ujenzi holela tu...

Mbeya sasa hivi imejengwa jengwa hivyo kama Mbagala au Tandale...

Ukianza kuingia Nsalaga, Uyole unakutana na uchafu wa nyumba...

Hapo bado hujaanza kuingia ndani ndani...
 
Acha watu wawe huru,fitna zimezidi
Uhuru usiokuwa na utaratibu ni ghasia. Mji wa Mbeya kwa sasa pale katikati imekuwa ghasia makazi kuanzia Gombe mpaka Isanga ni ghasia mtu akiamka asubuhi anachimba msingi popote anaanza kujenga vyumba viwili vyake.

Hatuna Madiwani?! Hatuna ofisi za ardhi Mipango Miji. Wanafanya nini?!
 
Back
Top Bottom