Wakazi wa Mbeya mjini wasipodhibitiwa watajenga hadi juu ya Kawetere, matokeo yake si mazuri baadae

Wakazi wa Mbeya mjini wasipodhibitiwa watajenga hadi juu ya Kawetere, matokeo yake si mazuri baadae

Uhuru usiokuwa na utaratibu ni ghasia. Mji wa Mbeya kwa sasa pale katikati imekuwa ghasia makazi kuanzia Gombe mpaka Isanga ni ghasia mtu akiamka asubuhi anachimba msingi popote anaanza kujenga vyumba viwili vyake.

Hatuna Madiwani?! Hatuna ofisi za ardhi Mipango Miji. Wanafanya nini?!
Tabia za CHUKI na kudharau mtu anaejitafuta imetufikisha hapo,watu wa Mbeya wanapenda freedom sasa nyumba za kupanga zimekuwa chache ukiacha.mkeo ukaenda kuhangaika anakutana na vitimbi,tabu yote ya nini! Maisha ya kuchunguzana nani anataka,kila mtu aishi maisha yake.
Mimi huko ni home mji huo una shida vibanda kibao sabbu kipato hakiko stable,ukilima bei mbaya ukifanya biashara hakuna mnunuzi,nani anataka majoto.
 
Nilikuwa na matumaini na dodoma ila kwa uongozi huu mbovu ata dodoma mipango inaweza potea ikawa hovyo tu.
 
Tabia za CHUKI na kudharau mtu anaejitafuta imetufikisha hapo,watu wa Mbeya wanapenda freedom sasa nyumba za kupanga zimekuwa chache ukiacha.mkeo ukaenda kuhangaika anakutana na vitimbi,tabu yote ya nini! Maisha ya kuchunguzana nani anataka,kila mtu aishi maisha yake.
Mimi huko ni home mji huo una shida vibanda kibao sabbu kipato hakiko stable,ukilima bei mbaya ukifanya biashara hakuna mnunuzi,nani anataka majoto.
Mipango miji wangewapanga sasa sio watu kujijengea tu!
 
Hayo yote ni madhara ya kutawaliwa na CCM kwa mda marefu,cha ajabu mnaendelea kuimba kuwa October mnatiki tena.
 
Alafu akaleta sera za ujamaa ,zilikuja kuwapokonya wapigania uhuru na wazawa Haki ya kumiliki uchumi wao wa TZ, hili lilikuwa kosa kubwa sana ,

Leo hii uchumi wa TZ unamilikiwa na wahindi na waarabu. Tunachekwa kwa kweli

Alikuwa ni mzalendo asiyejua mbinu za kujenga uchumi imara na wakisasa utakao dumu vizazi na vizazi
Nasikia Kuna mpango wa kumtangaza mwenye Heri.Hivi huo mchakato umefikia wapi Jamani.
 
Ujue unaweza kuwa unaipenda nchi Yako , ila ukawa hauna maarifa sahihi ya kiuchumi,
Serikali ya 1,2 issues za mipango miji hawakujihusisha kabisa
Angalau Nyerere alisomesha, alitibu kila mtu na kuajiri kila mtu.

Waliofuata hawakuweka mipango
hawakuajiri, hawakusomesha, na mbona hawaweki mipango.
 
Angalau Nyerere alisomesha, alitibu kila mtu na kuajiri kila mtu.

Waliofuata hawakuweka mipango
hawakuajiri, hawakusomesha, na mbona hawaweki mipango.
Hao watu waliosomeshwa na kuajiriwa na Nyerere, hawakuwa na purchasing power, na kama ukiwa nayo unaoneka mwizi, .

Ilifikia Hatua mpaka mawaziri walikuwa wanakunywa pombe za kienyeji badala ya bia, ss hapo serikali itapataje mapato ?.
Alafu hapo hapo serikali kupitia CCM wanajenga vilabu vya pombe za kienyeji kila mahali nchi nzima.

Ss jiulize vilabu vya pombe za kienyeji na viwanda vya bia, ni kipi kati ya hapo kinachoingiza mapato kwa wingi? Ni wazi awamu ya Kwanza kwenye uchumi hawakujua wanachofanya.


Ukitaka kununua gari ,basi ilikuwa kama kosa vile, ss huku Nyerere amejenga General tyres pale Arusha ,
Ila kumiliki gari ni mtiti , ndio maana kiwanda kikafa kwa kukosa wateja ,

Inasikitisha sana kuwa na viongozi wasiojua kukuza uchumi
 
Tanzania kila mahali ni ujenzi holela tu...

Mbeya sasa hivi imejengwa jengwa hivyo kama Mbagala au Tandale...

Ukianza kuingia Nsalaga, Uyole unakutana na uchafu wa nyumba...

Hapo bado hujaanza kuingia ndani ndani...
Unamaliza view nzuri za mlima nyoka na huko kwingineko Nsalaga inakukaribisha na vijumba kila kimoja kimegeukia kwake, barabara za shida ukienda Gombe ndo balaa sasa hivi wanajenga kwenda mlimani kule mkabala na bonde la Isyesye ukija Isanga kule mlimani vibanda vinajengwa kwenda mlimani kwenye vyanzo vya maji...unajiuliza halmashauri mipango miji na wizara hawaoni hii italeta athari kubwa sana miaka michache ijayo maana miundo ya maji taka ni issue na mazingira yanaharibiwa
 
Wakuu,
Kuna jambo la muda mrefu linanipa wasiwasi sana kuhusu namna mji wa Mbeya unavyokua.

Sasa hivi ukipita maeneo mbalimbali utakuta kila kona kuna ujenzi, mara nyingi bila mpangilio wa mji.

Wengine wameanza hata kupanda kuelekea Kawetere, eneo ambalo kiasili ni mlima wenye vyanzo vya maji na mandhari ya kipekee.

Swali kubwa: tukiruhusu hali hii iendelee bila udhibiti, nini kitatokea baada ya miaka 10–20?

🔹 Madhara ya mazingira: Uharibifu wa vyanzo vya maji, mmomonyoko wa udongo, na hatari ya maporomoko ya ardhi.
🔹 Madhara ya kijamii: Kukosekana kwa huduma za msingi kama barabara, maji na mifumo ya taka kwa sababu maeneo hayakupangwa.
🔹 Madhara ya kisheria: Baadaye serikali inaweza kuamuru bomoabomoa, jambo linaloleta hasara kubwa kwa wananchi.

Kwa sasa inavyoonekana, jitihada za kupanga mji hazilingani na kasi ya watu kujenga hovyo.

Hali hii ikiachwa iendelee, Mbeya inaweza kupoteza hadhi yake ya kipekee na kubaki ni mji usiopangika wenye changamoto nyingi za kimaisha. Uholela huu upo hata kwenye mpangilio wa usafiri katikati ya mji. Stendi ya Kabwe nayo ni kama haipo sababu yeyote pale anafanya lolote wakati wowote (magari binafsi kuegesha,soko mjinga,bajaji, daladala vyote vimetapakaa stendi ya Kabwe)

Ushauri wangu:
Serikali za mitaa, mamlaka ya ardhi na mji, pamoja na wananchi wenyewe, wanapaswa kushirikiana kupanga, kudhibiti na kutekeleza sheria za mipango miji.

Vinginevyo kizazi kijacho kitakuja kulalamika kwa makosa tuliyoyafanya leo.

Kwa sasa ni mara 100 uende ukaishi Tukuyu uwe unakuja kufanyia kazi Mbeya mjini. Mji umekuwa kero vibaya sana as if hakuna uongozi.
Hali ni mbaya sana, mkuu! Siasa ya CCM ndio chanzo!
 
Tanzania kila mahali ni ujenzi holela tu...

Mbeya sasa hivi imejengwa jengwa hivyo kama Mbagala au Tandale...

Ukianza kuingia Nsalaga, Uyole unakutana na uchafu wa nyumba...

Hapo bado hujaanza kuingia ndani ndani...
Dah! Nsalaga kulikuwa kijijini sana huko nakumbuka nilikuwa nikienda kumsalimia Bibi yangu maji tulikuwa tunachota kwenye mifereji
 
Dah! Nsalaga kulikuwa kijijini sana huko nakumbuka nilikuwa nikienda kumsalimia Bibi yangu maji tulikuwa tunachota kwenye mifereji

Sasa hivi hakushikiki, nyumba kama uchafu ni kama upo Kibera Nairobi...
 
Back
Top Bottom