BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Sisi wakazi wa Shamaliwa A na B wengi wetu hatuna huduma ya Maji kwa muda wa zaidi ya mwezi sasa kutokana na wahusika wanaotengeneza Barabara kwa nia ya kuboresha wameharibu mabomba na hivyo Mamlaka ya Maji kulazimika kukata maji.
Wanachofanya wanaotengeneza Barabara ni jambo jema lakini sasa kama ujenzi wao unasababisha mateso ya kukosekana kwa maji ni jambo ambalo linatuumiza wengi wetu
Tunalazimika kununua maji ya kisima ambayo mengine sio safi na salama, pia gharama ya kununua maji imekuwa kubwa kiasi kwamba ndoo moja tunanunua kwa Tsh. 500 na ukitaka maji masafi kabisa ndoo moja ni Tsh. 1,000.
Imefikia hatua Bodaboda wanaona bora wabebe madumu ya maji kuliko kubeba abiria kwa kuwa akibeba madumu manne au Matano kwa trip moja anakuwa amepata Shilingi 2,000 hadi 2,500 tofauti na kupata bukubuku ya kubeba Abiria.
Tunaomba Mamlaka za Maji na hao wahusika wanaohusika na ujenzi kuchukua hatua mapema kwa kuwa Wananchi tunateseka na hali yetu sio nzuri.
Majibu ya Waziri ~ Waziri Aweso: TARURA na MWAUWASA wanafanya mchakato wa kurejesha maji kwa Wakazi wa Shamaliwa - Mwanza