Wakazi wa Swaswa Dodoma na Mafuriko

Wakazi wa Swaswa Dodoma na Mafuriko

Ilazo na Swaswa mafuriko yanasumbua.
Ukitaka kiwanja njoo Iyumbu, Ihumwa, Nala.
 
Wakazi wa Swaswa jijini Dodoma waanza kujiandaa na mafuriko, ni kitu kimenishangaza sana mara baada ya kuspend muda kwa wiki yote iliyopita katika jiji hili. kuna mwenyeji wangu amekuwa akinishauri nije kujenga Dom nikasema ngoja niende, zunguruka na madalali kutafuta viwanja ndio nikaonyeshwa Swaswa. Bahati ikawa yangu, baada ya kuachana na dalali si nikarudi eneo lile, jirani akanitonya kuwa niwe makini kununua viwanja maeneo hayo kwasababu hata wao wameshaanza kujiandaa na mafuriko kwa mvua zitakazokuja kwani kila mwaka kuna mafuriko. nilishangaa sana katikati ya jiji miundombinu haidhibiti mafuriko kwenye maeneo yenye viwanja vizuri namna ile. akaniambia pia Swaswa kuna migogoro ya viwanja balaa....kwakweli kiwanja ni kuzuri sana lakini sijajua kama kweli alichosema jirani ni sahihi au alikuwa anambania mshikaji asipate pesa, na hasa lile la migogoro. wenyeji wa Dodoma naomba mtutonye tafadhali anayeyajua mazingira hayo.

Hapo ni Swaswa
Kuna Nkuhungu, Ilazo, Nzughuni, Mbwanga, Changombe ya Chini, Kizota,Msalato kuna sehem ni balaa Mvua zikinyesha hakupitiki
Dodoma maeneo mengi Mvua kubwa zikinyesha kunajaa maji
Mwez wa nne nilishuhudia nyumba kali zimejaaa maji Miundombinu ya Dodoma bado sio mizuri ukinunua kiwanja unatakiwa uangalie
Unakuta nyumba nzuri ila imejaaa maji kiasi kwamba unamuonea huruma mwenye nyumba
Msikurupuke kujenga dodoma et kisa mji wa serikali oooh mtaishia kulia kwa mafuriko ya mvua

Dodoma ya Sasa sio kama ya enzi za Magufuli Dodoma ya sasa hivi imeanza kupoteza mvuto
Enzi hizo watu walikimbilia dodoma wanajenga hila now hamna issue Dodoma kama sio mwajiriwa dah kwa jua lile unaweza kudata kwanza maisha ya Dodoma yako juu

Unaweza kuja Dar ukatafuta issue ukafanya na ukaendesha Maisha ila Dodoma kama ujaajiriwa isee ni ngumu sana kwanza Biashara kule ni ngumu na ni za msimu wanachuo wasipokuwepo basi mambo hayaendi
 
Huko swaswa nyumba hujaa maji ka bwawa kipindi cha mvua
 

Tulia Kwanza Utapigwa Halafu Achana Na Madalali Utaliwa, Viwanja Millions 2 Unapata Tena Nala Chuo Cha DECA

Huku watu wanajenga balaa, halafu tanesco wamehamasisha ujenzi sana baada ya kuanza kusambaza nguzo na nyaya.
Pia chuo (DECCA) kinachangia.
 
hamaanishi kwamba maji hayatoki kwenye mabomba, anamaanisha kuna mafuriko wakati wa mvua.
Ninapafahamu sana Kikuyu mkuu, hakuna shida ya mafuriko kipindi cha mvua wala hakuna shida ya maji ya DUWASA.
 
kiwanja milioni 2 dodoma? hahaha.
Huamini au? Bahati yako nimetoka Dodoma ngekupeleka viwanja vilivo sehem sahihi kwa bei hizo halafu usingeamini.
Kuwa makini na madalali utawatajirisha.
 
Back
Top Bottom