Wake Up Call. Tanzania tunakwama wapi? Tumekubali kubuzurwa na watawala wa ovyo?

Wake Up Call. Tanzania tunakwama wapi? Tumekubali kubuzurwa na watawala wa ovyo?

Haya mambo yanafikirisha sana, inawezekana tatizo letu lipo zaidi ndani ya vichwa vyetu kuliko kule tunapopafikiria kwenye Katiba Mpya..

Naona dalili hata kama Katiba Mpya itakuja, lakini bado tabia zetu za "ukondoo" tulizorithi miaka mingi iliyopita zikaendelea kutukwamisha kufikia malengo yetu ya kudai haki zetu, tumekuwa wakimya, wapole, tunaotegeana, wakulalamika kwa miaka mingi sana.
 
Kila ngazi kuanzia juu mpaka chini, taasisi za serikali wafanyakazi 85%, wanapokea maagizo toka chama tawala.
Na hao wafanyakazi wana familia zinawategemea, utegemee wagome wakubwa wao wawatimue kazi.
 
tupo hapa tulipo kwasababu yakuwaacha mabwanyenye warelax na sio kuwapa pressure itakayowajulisha kila mara wao ni watumishi wetu.
Watumishi wenye majibu ya dharau na kejeli. Kweli leo mfanyakazi wako nyumbani akujibu kama Mwigulu si utamvunja mguu? Je hawa tuliowapa dhamana wana jeuri gani?
 
Chile rais walimtengua madarakani lkn raia bado waliendelea kuandamana.
Greece ilitokea ajali ya treni, waziri wa usafiri akajiuzulu lkn raia waliendelea kuandamana mpk waziri mkuu akaomba radhi.
South Africa umeme kukatika na kutokuwa na imani na rais wameingia barabarani kuandamana.
Tunisia wameingia barabarani baada ya maneno ya kibaguzi aliyotoa rais wao.
nk
nk
nk
 
Mods msije kufuta uzi mtakua mmenikosea (mmetukosea) haki ya kikatiba na tutafika mahakamani ikibidi.

Ujerumami wanadai kuongezewa mishahara Germany 'mega strike': Public transport network halted over pay

Ufaransa wanaandamana kukataa kubadilishwa sheria ya mafao

Israel wanagoma katiba kubadilishwa kuwa ya kidikteta Netanyahu said to now back overhaul freeze; anti-riot police clear out Tel Aviv rally

Ureno wameandamana kuhusu hali ngumu ya maisha Thousands protest in Portugal over cost-of-living crisis

Sir Lanka wameandamana kuhusu uchaguzi Sri Lanka Police Fires Tear Gas at Election Protest; 15 Injured

Kenya wanaandamana hali ngumu ya maisha Kenya protests: Raila Odinga's convoy tear-gassed in Nairobi

South Africa wanaandamana hali ngumu ya maisha S. Africa Police, Soldiers Deploy for Opposition-Led Protests

Sisi Tanzania tunaishiaje kulalamika mitandaoni kuhusu katiba mpya? Kuhusu hali ngumu ya maisha? Demokrasia? Kubakwa kwa uchaguzi? N.k.

Tulilogwa na nani? Najiuliza tu!!

Erythrocyte Mmawia brazaj Arovera Mrs Lissu
Mbona sijaona ulizo likielekea kwa mwanakijiji yeyote 🤔
 
Chile rais walimtengua madarakani lkn raia bado waliendelea kuandamana.
Greece ilitokea ajali ya treni, waziri wa usafiri akajiuzulu lkn raia waliendelea kuandamana mpk waziri mkuu akaomba radhi.
South Africa umeme kukatika na kutokuwa na imani na rais wameingia barabarani kuandamana.
Tunisia wameingia barabarani baada ya maneno ya kibaguzi aliyotoa rais wao.
nk
nk
nk
Hii nchi ni ngumu sana. Tutatukwanwa sana na akina Madelu lakini kila mtu atakuambia kudai haki hakukuletei ugali mezani
 
Wewe mwenyewe ulietoa wazo kwanini usiwe mstari wa mbele kuimplement hoja yako vinginevyo wewe ni keyboard warrior kama wenzako
 
Mku unahitaji kufikiri kabla ya kutaka kuandamana. Usifikiri Mh.Mbowe kudai haki kwa kutumia busara hajui kitu. Yule Jama anajua anachofanya na atafika mbali. Chadema tunatakiwa tutulie ili mambo yasivurugike. Hebu na ww omba busara kwa Mwenyezi Mungu akuzawadie hekima ikusaidie na kuongoza wanafamilia yako.
 
Back
Top Bottom