Wake Up Call. Tanzania tunakwama wapi? Tumekubali kubuzurwa na watawala wa ovyo?

Haya mambo yanafikirisha sana, inawezekana tatizo letu lipo zaidi ndani ya vichwa vyetu kuliko kule tunapopafikiria kwenye Katiba Mpya..

Naona dalili hata kama Katiba Mpya itakuja, lakini bado tabia zetu za "ukondoo" tulizorithi miaka mingi iliyopita zikaendelea kutukwamisha kufikia malengo yetu ya kudai haki zetu, tumekuwa wakimya, wapole, tunaotegeana, wakulalamika kwa miaka mingi sana.
 
Kila ngazi kuanzia juu mpaka chini, taasisi za serikali wafanyakazi 85%, wanapokea maagizo toka chama tawala.
Na hao wafanyakazi wana familia zinawategemea, utegemee wagome wakubwa wao wawatimue kazi.
 
tupo hapa tulipo kwasababu yakuwaacha mabwanyenye warelax na sio kuwapa pressure itakayowajulisha kila mara wao ni watumishi wetu.
Watumishi wenye majibu ya dharau na kejeli. Kweli leo mfanyakazi wako nyumbani akujibu kama Mwigulu si utamvunja mguu? Je hawa tuliowapa dhamana wana jeuri gani?
 
Chile rais walimtengua madarakani lkn raia bado waliendelea kuandamana.
Greece ilitokea ajali ya treni, waziri wa usafiri akajiuzulu lkn raia waliendelea kuandamana mpk waziri mkuu akaomba radhi.
South Africa umeme kukatika na kutokuwa na imani na rais wameingia barabarani kuandamana.
Tunisia wameingia barabarani baada ya maneno ya kibaguzi aliyotoa rais wao.
nk
nk
nk
 
Mbona sijaona ulizo likielekea kwa mwanakijiji yeyote πŸ€”
 
Hii nchi ni ngumu sana. Tutatukwanwa sana na akina Madelu lakini kila mtu atakuambia kudai haki hakukuletei ugali mezani
 
Wewe mwenyewe ulietoa wazo kwanini usiwe mstari wa mbele kuimplement hoja yako vinginevyo wewe ni keyboard warrior kama wenzako
 
Mku unahitaji kufikiri kabla ya kutaka kuandamana. Usifikiri Mh.Mbowe kudai haki kwa kutumia busara hajui kitu. Yule Jama anajua anachofanya na atafika mbali. Chadema tunatakiwa tutulie ili mambo yasivurugike. Hebu na ww omba busara kwa Mwenyezi Mungu akuzawadie hekima ikusaidie na kuongoza wanafamilia yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…