Pakacha,
mm nasema haswa kile ninachokiona kwa macho au kuthibitisha baada ya kusikia au ww hali halisi unaionaje, kwa mfano Zanzibar mpaka sasa hakuna gazeti huru, absolutely huru,T.V huru(sjuwi saivi maana cable si kila mchakura jaani kama mm anaimudu),hata hao wajuba na wakaidi wanaothubutu kusema hutumia majukwaa mengine au vyombo vya habari vya bara. SMZ haijaelewa kitu fulani ambacho SMT wana enjoy kule bara, kwamba, kuwa na uhuru wa maoni na vyombo huru vya kutolea maoni kunaisadia serikali na vyombo vyake kuwa karibu na wananchi kwa kujikosoa,kujitathmini na kujirekebisha, huwezi kukiona kisogo chako ila mtu aliyenyuma yako. Leo kama si uhuru wa vyombo vya habari kule bara, kwa mfano tu, watu kama kina Abdallah Zombe wangeendelea kutumia vibaya dhamana zao na kuwadhuru watu bila hatia au vita vya ufisadi visingefikia hatua ilipo(japo hairidhishi) lakini ndo mwanzo. Bado nasisitiza kuwa licha ya katiba ya zanzibar kuweka wazi uhuru wa maoni na kujieleza, bado serikali haijaachia forums za kuruhusu fursa hiyo ya kikatiba kwa uwazi. Na kwa hivyo basi ndo maana SMZ imekuwa ikiindesha nchi kama giningi, mambo siri siri tuuu na kiuchawi uchawi mpaka kuche.