Haya haya wana JF, taarifa za kuaminika zinasema kwamba, wakenya sita miongoni mwa wakenya walioingia Bongo Dar es Salaam kushiriki katika tamasha la Utamaduni la Jumuiya ya nchi za Afrika mashariki ambalo linatarajiwa kufungwa hapo kesho Jumamosi, wametoroka na kujichanganya na wabongo ili kukwepa kurudi kwao kesho.
Hali hii ilitegemewa sana kujitokeza kutokana na mwenendo wa washiriki kutoka nchi zingine za Uburundi, Kenya, Uganda na Sudan ya Kusini, kukosekana katika viwanja vya Taifa muda mwingi wa tamasha, badala yako wamekuwa wakijimwa CBD kulishangaa jiji lenye kila aina ya urembo, jambo hili limesababisha kuviacha vikundi vya Tanzania pekee kutumbuiza kwa wiki nzima sasa.
Baadhi ya washiriki toka hizo nchi walioojiwa na vyombo vya habari, walisikika wakisema kwamba, hii ni Mara yao ya kwanza kufika Tanzania, hawakutegemea kuikuta Dar es Salaam katika ikiwa na maendeleo kiasi hiki, wengi wamesifia, Amani, usafi, mpangilio wa mji, Kariakoo, BRT na vyakula.