Wakenya huu mswada uliopitishwa na wabunge wa Jubilee Alhamisi unaathiri vipi uchaguzi ujao?

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2016
Posts
1,817
Reaction score
4,061
Hbari nimeitoa The Citizen Tv, wapinzani wanalalamika wabunge wa Jubilee wamepisha muswada ambao utawewezesha kuiba uchaguzi wa October 26

Ila sijaelewa huu juswada unahusu nini exactly na utaathiri vipi uchaguzi ?

Wadau Tony254 MK254 @Samuel999 MwendaOmo Jay456watt KENPAULITE COLLOH-MZII RELOADED nisaidieni

Jubilee Party MPs on Thursday morning pushed through a motion to reduce the maturity time of publication of two electoral reform Bills to one day from the previous 14 days.

Dominance of Jubilee Party played a key role in the successful passing of the contested motion with 144 MPs voting for and 53 voting against.
Speaking outside Parliament after NASA MPs walked out in protest, Kiminini MP Chris Wamalwa accused Jubilee of plotting to make changes to the electoral laws that to favour them in next month’s fresh presidential poll.

Opposition MPs accused Jubilee lawmakers of rushing to Parliament to amend the Election Laws Amendment Act to allow the ruling party “rig the election in October 26 presidential poll.

The passing of the motion led to the immediate collapse of the consultative talks between the Independent Electoral and Boundaries Commission, NASA and Jubilee Party representatives
 
kuna mswada ambao naibu rais William Ruto anataka upitishwe utakaowapunguzia wale majaji wa Supreme court nguvu na mamlaka...mswada huu ukipitishwa, majaji hawatakuwa na mamlaka ya kufuta uchaguzi na kuamrisha urudiwe upya...Kumbuka Ruto ana tamani kuwania wadhifa wa urais mwaka wa 2022...
 
NASA should go to court so as to petition these amendments. Uhuru is preparing clauses in the law that will enable him rig the election. He is doing everything to remain in office, so NASA be careful.
 
Siasa za kenya wakati mwingine zinafundisha na kuwa mfano wa kuigwa lakini wakati mwingine zinasikitisha sana
 
Siasa za Kenya ukizifuatilia sana unaweza kuwa chizi, hawa hawa Uhuru na Rutto walipambana sana kupata katiba mpya, baadae wakawa wanapita kuisifia na kuiaminisha dunia kwamba katiba ya Kenya is the best, hata vumbi halijafutika tayari imeonekana na dosari... wanasemaga siku ya kufa nyani, miti yote aliyozoea kuiparamia siku zote inaanza kuteleza...wakenya chokochoko hii, kuna kitu mnakitafuta, Mungu hajaribiwi, ukibeep yeye anapiga...chondechonde..kila siku mnakuja na jipya..kwanini lakini?
 
kuna mswada ambao naibu rais William Ruto anataka upitishwe utakaowapunguzia wale majaji wa Supreme court nguvu na mamlaka...mswada huu ukipitishwa, majaji hawatakuwa na mamlaka ya kufuta uchaguzi na kuamrisha urudiwe upya...Kumbuka Ruto ana tamani kuwania wadhifa wa urais mwaka wa 2022...
Hawa watu hawafai kabisa. Wanataka kuachiana nchi. Kwamba akitoka Uhuru aingie Ruto ikulu.
 
wakati mwingine huwa natamani uongozi wa Magu kidogo....yaani hapa Kenya imekuwa ni sarakasi za kipumbavu for the last 6 months...vuta nikuvute ujinga mtupu...siasa za kijinga kwel kwel...wakati nchi kama ethiopia na tanzania ziko zinakimbia kwa haraka, Kenya ni IEBc, sijui Supreme court, sijui Nasa, sijui Jubilee, sijui election date imeahirishwa, sijui Chiloba, sijui maandamano, sijui matusi...smh
 
Hawa viongozi wa Jubilee wanataka kuturudisha mbali sana, wanafaa kukubali kwamba katiba nzuri lakini pia inakata pande zote mbili, sio kila ikikinzana na matakwa yao wanabadilisha gia angani. Hatuwezi kubadilisha katiba kwa ajili ya watu wachache, je vipi siku tukipata rais asiyejaribiwa itakuaje kama watakua wamechakachua katiba, atatunyoosha bila pakukimbilia au kutokea.

Rais Uhuru bado unayo kura yangu lakini kwa hili naomba mkulu achia, wacha kabisa. Tunahitaji katiba nzuri iendelee kwa ajili ya vizazi vya leo na kesho. Tumeona athari za katiba mbaya, leo hii hata majirani wanatamani sana kupata katiba nzuri kama yetu na wengi wanasoma namba kila siku, hamna haja ya kuturudisha nyuma tuwe kama wao.

Hii kwa kweli imeniuma.
 
wakati mwingine huwa natamani uongozi wa Magu kidogo....yaani hapa Kenya imekuwa ni sarakasi za kipumbavu for the last 6 months...vuta nikuvute ujinga mtupu...siasa za kijinga kwel kwel...wakati nchi kama ethiopia na tanzania ziko zinakimbia...smh
Katiba ya Kenya ilikuwa imekaa vizuri sana. Imepunguza nguvu za rais kwa kiasi kikubwa tofauti na Tanzania ambapo rais ni mungu-mtu.
Sasa anachokifanya Uhuru ni kuirudisha Kenya hatua 50 nyuma. Pathetic!
 
wakati mwingine huwa natamani uongozi wa Magu kidogo....yaani hapa Kenya imekuwa ni sarakasi za kipumbavu for the last 6 months...vuta nikuvute ujinga mtupu...siasa za kijinga kwel kwel...wakati nchi kama ethiopia na tanzania ziko zinakimbia...smh
Kweli kabisa, kila jambo lazima liwe na mipaka, sasa Kenya ni kama mambo yamesimama, haijulikani kesho itakuwaje, na dalili zinaonyesha ndio kwanza mambo yanazidi kuparaganyika... Sonko naye leo amecharuka kwa matusi, Jumatatu maandamano... haijulikani uchaguzi upo ama haupo,.. kila siku inakua hafadhali ya jana...chuki zinazidi miongoni mwa makabila...jamaniii. Hali hii ya uncertanity ikashazoeleka huwa haimaliziki, inakuwa ni sehemu ya maisha ya jamii husika.
 
Watu badala ya kufikiria maendeleo yao na ya nchi yao sasa kila siku kuwaza siasa na kujawa na wasiwasi.. Kenya sasa ni hatari
 
kuna mswada ambao naibu rais William Ruto anataka upitishwe utakaowapunguzia wale majaji wa Supreme court nguvu na mamlaka...mswada huu ukipitishwa, majaji hawatakuwa na mamlaka ya kufuta uchaguzi na kuamrisha urudiwe upya...Kumbuka Ruto ana tamani kuwania wadhifa wa urais mwaka wa 2022...
kwa hiyoleo ndio walikuwa na mjadala kupunguza maturity time ya hizo miswada kusainiwa? au maturity time ya nini?
 
Hawa viongozi wa Jubilee wanataka kuturudisha mbali sana, wanafaa kukubali kwamba katiba nzuri lakini pia inakata pande zote mbili, sio kila ikikinzana na matakwa yao wanabadilisha gia angani. Hatuwezi kubadilisha katiba kwa ajili ya watu wachache, je vipi siku tukipata rais asiyejaribiwa itakuaje kama watakua wamechakachua katiba, atatunyoosha bila pakukimbilia au kutokea.

Rais Uhuru bado unayo kura yangu lakini kwa hili naomba mkulu achia, wacha kabisa. Tunahitaji katiba nzuri iendelee kwa ajili ya vizazi vya leo na kesho. Tumeona athari za katiba mbaya, leo hii hata majirani wanatamani sana kupata katiba nzuri kama yetu na wengi wanasoma namba kila siku, hamna haja ya kuturudisha nyuma tuwe kama wao.

Hii kwa kweli imeniuma.
Mimi ninaamini katiba nzuri ni ile inayoleta ufumbuzi wa matatizo ya wananchi walio wengi, ambao ni masikini, sio inayotoa ufumbuzi wa matatizo ya wanasiasa, ukisikiliza kwa makini sana huo unaoitwa uzuri katika katiba hiyo ya Kenya, mengi sana yanawalenga wanasiasa na viongozi wa juu, sio wananchi, mambo kama haya ya kupinga matokeo, kumpunguzia rais madaka na kadhalika, karibu yote yanawagusa wanasiasa au watu wa tabaka la juu. Kuna matatizo ya msingi yanawakabili wakenya tangu wapate uhuru 1963, tujiulize tangu katiba nzuri ipatikane, je kuna unafuu gani uliopatikana katika;
1) Kupunguza ukabila unaohatarisha nchi kugawanyika vipande vipande
2)Rushwa inayozidi kuongezeka na kuzidisha ugumu wa maisha
3) Kupunguza pengo la umasikini kati ya tajiri na masikini
4) Kushughulikia dhuluma iliyosababisha wachache matajiri na wanasia kujiridhisha ardhi ya wananchi wanyonge walioporwa na wakoloni kama ilivyopendekezwa katika The wako report
5) kuimarisha usalama ambao unazidi kuzorota
6) kuongeza ajira kwa vijana
7)Upatikanaji wa chakula cha uhakika(Food security)

Kama katiba haiwezi kuwapatia wakenya majibu katika hayo, basi huo uzuri wa katiba kwao hawatouona zaidi ya kuhudhuria mikutano ya wanasiasa ambao ndiyo wanufaika wakubwa wa hii katiba nzuri.
Nawakilisha
 
Kawaida ya Watanzania haswa nyie wa mlengo wa CCM mnapoijadili katiba ya Kenya huwa ni kama mumekaririshwa, yaani hayo yote umeandika hapo yameshughulkiwa pakubwa na katiba yetu mpya. Huwa mnajaribu kutumia huko kukaririshwa ili kuwaonyesha Watanzania kwamba hamna umuhimu wa wao kufuata katiba mpya. Huwa mnatumia nguvu nyingi sana.

Kwa ajili ya katiba mpya
- Maendeleo yameenea kwenye gatuzi zote hata maeneo ambayo yalikua yametelekezwa maiaka yote
- Maskini wa chini wameanza kuona haki ikitendeka
- Ukabila unapungua pakubwa maana watu walikua wameaminishwa raslimali zote zinaishia kati au Nairobi, leo hii mikoa na gatuzi zote zimepata fursa ya kutumia raslimali zao vizuri. Ni kama watu wa Mtwara waanze kuona umuhimu wa gesi.

Kuna vitu vingi sana ambavyo naweza kuandika, na kuna mada na hoja tulichangia sana humu, lakini kwa sababu upo kwa ajili ya kutafuta makosa hutaona chochote kizuri. Utatumia nguvu nyingi sana kupata wapi pa kukosoa ili uwatamaushe Watanzania wenzio wanaotamani kuwa na katiba mpya.
 
Usianze kujishuku na kujihami mapema, mimi nimeuliza maswali ungenijibu badala ya kunishutumu. Sijasema hakuna mambo mazuri yaliyopatikana, ila nimesema mengi mazuri yanawalenga watu wakubwa na wanasiasa, na nimekua very specific kuainisha maeneo ambayo yanawagusa wananchi, hivi kweli bila aibu unasema ukabila Kenya umepungua, kweli unasema maneno hayo wewe bila aibu hata chembe? 2) Hivi kweli rushwa imepungua Kenya?, mwaka jana imeshika namba tatu duniani, 3) Hivi unataka kusema usalama wa raia wa Kenya umeimarika wakati Kenya imekua kinara Afrika katika extra judicial killings 2016, 4) Hivi unasema pengo la masikini na tajiri Kenya linapungua?. 5) Unataka kusema malalamiko ya ardhi yaliyofanyiwa kazi na tume ya wako yamefanyiwa kazi?, 6)Unataka tuamini kiwango cha unemployment kinashuka au kinaongezeka?. Kama unasema katiba mpya umeyapatia ufumbuzi hayo na ukatupa na ushahidi, basi kweli ni katiba nzuri, vinginevyo ni nyie wachache wanasiasa na watu wa hali nzuri ndiyo mnaouona huo uzuri
 
Siasa za Kenya ukizifuatilia sana unaweza kuwa chizi, hawa hawa Uhuru na Rutto walipambana sana kupata katiba mpya, baadae wakawa wanapita kuisifia na kuiaminisha dunia kwamba katiba ya Kenya is the best, hata vumbi halijafutika tayari imeonekana na dosari... wanasemaga siku ya kufa nyani, miti yote aliyozoea kuiparamia siku zote inaanza kuteleza...wakenya chokochoko hii, kuna kitu mnakitafuta, Mungu hajaribiwi, ukibeep yeye anapiga...chondechonde..kila siku mnakuja na jipya..kwanini lakini?
Kwani hao wawili wantofautiana vipi na hawa NASA jameni? Wanasiasa wa NASA walifurahia sana majority ruling kule supreme court sasa iweje ati majority vote bungeni nayo sasa ni kitu kibaya?
 
Ndiyo ninawasngaa, nilianza kwa kusema siasa za Kenya ukizifuatilia unaweza kuwa chizi, nikamalizia kwa kusema "likiisha hili linakuja lingine, kwanini lakini?", wakitoka NASA, wanakuja Jubilee, hakuna hata wakumuamini.
 
Usianze kujishuku na kujihami mapema, mimi nimeuliza maswali ungenijibu badala ya kunishutumu. Sijasema hakuna mambo mazuri yaliyopatikana, ila nimesema mengi mazuri yanawalenga watu wakubwa na wanasiasa, na nimekua very specific kuainisha maeneo ambayo yanawagusa wananchi, hivi kweli bila aibu unasema ukabila Kenya umepungua, kweli unasema maneno hayo wewe bila aibu hata chembe? 2) Hivi kweli rushwa imepungua Kenya?, mwaka jana imeshika namba tatu duniani, 3) Hivi unataka kusema usalama wa raia wa Kenya umeimarika wakati Kenya imekua kinara Afrika katika extra judicial killings 2016, 4) Hivi unasema pengo la masikini na tajiri Kenya linapungua?. 5) Unataka kusema malalamiko ya ardhi yaliyofanyiwa kazi na tume ya wako yamefanyiwa kazi?, 6)Unataka tuamini kiwango cha unemployment kinashuka au kinaongezeka?. Kama unasema katiba mpya umeyapatia ufumbuzi hayo na ukatupa na ushahidi, basi kweli ni katiba nzuri, vinginevyo ni nyie wachache wanasiasa na watu wa hali nzuri ndiyo mnaouona huo uzuri

Sijishuku, ila ni kile huwa nawaona nguvu ambazo mnatumia kuonyesha Watanzania jinsi hamna umuhimu wa katiba mpya huku mkiorodhesha 'mapungufu' mliyokaririshwa.
Mimi ni Mkenya ambaye nimeishi Kenya tangu wakati tukiwa na katiba mbovu ya zamani kama yenu hiyo hadi leo ambapo tuna katiba bora Afrika. Nimeona matunda ya umuhimu wa katiba nzuri, nimeyafurahia.

Chuki za kikabila zilikua zimekithiri maana Wakenya kwenye wilaya za mbali walikua wameaminishwa kwamba raslimali zote zinaliwa Nairobi na kabila moja. Lakini leo hii watu wanajivunia vilivyomo ndani yao na baina yao. Wakenya wengi wamefunguliwa macho na kumgundua adui wao.

Tulizoea machafuko ya kikabila kila wakati wa uchaguzi, tulizoea kuona makabila makubwa kila moja likiwa na mgombea urais wake, lakini leo hii Wakenya wamejikusanya kwenye milengo miwili, Jubilee au NASA.

Changamoto zipo, lakini ukilinganisha na maisha ya kabla ya katiba mpya, wengi tunaona afueni. Ipo siku extra-judicial killings zilikua kama matukio ya kila siku. Polisi walikua wanapiga wananchi risasi kiholela, mauaji kila mahali, lakini leo wanawajibishwa, inabidi wanakua makini sana. Sio kama huko kwenu mara SMG mnakimbizana hadi Nairobi, mara miili ya watu inakutwa kwenye fukwe mara huku mara kule, tulikua tumezoea mambo kama hayo mnayoyapitia leo.

Hata mazuri ya ardhi huwezi kuyaona maana umekita kwenye kutafuta mabaya, lakini tunaona jinsi ilivyo ngumu kunyakua kipande cha ardhi kwenye Kenya ya leo. Kuna miaka watu walikua wanagawana nchi kama nyama. Juzi hapa naibu wa rais amepoteza viwanja alivyokua amenyakua, nguvu zake za urais zilishindwa kufanya kazi.

Kama nilivyosema kuna mengi, lakini hata nikiyaandika humu itakua kama najaribu kupasua ukuta kwa kichwa, maana ndivyo mlivyo.......
 
Acha kutuingiza choo cha kike wewe, taarifa zote zinaonyesha hayo niliyokutajia yanaongezeka mwaka hadi mwaka leo unasema yanapungua, acha maneno weka muziki, ajenda kubwa kwenye uchaguzi mwaka huu ilikuwa ni rushwa, security, unemployment na hali ngumu ya maisha, insecurity Kenya inaongoza Africa kwa sasa, google uone hali ilivyo, unemployment inakaribia 48%, haijawahi kutokea tangu Kenya ipate uhuru wake, rushwa ndiyo usisema, rais mwenyewe amesalimu amri haiwezi, wewe unatuletea filimbi hapa, inflation is the highest hapa EAC, achana na Burundi na SS, acha maneno ya kienyeji wewe, Kenya kwa sasa ipo kwenye very bad shape than any time before.
 
Back
Top Bottom