MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Hivi wewe uelewa wako ukoje?, huko shule ulienda kufuata nini?, mimi sijazungumzia wala kulinganisha na Tanzania, mimi nimezungumzia katiba ya Kenya, nikawa ninasema katiba nzuri lazima ijubu na kutafutia kero za wananchi, acha kulinganisha na Tanzania kwanza, tukimaliza hapa ndiyo tulinganishe maendeleo yanayotokea Kenya na Tanzania, ninaamini utakimbia au kurusha matusi. Mimi nilikutajia mambo saba ambayo niliyatafsiri kama shida za msingi zinazowakabili wananchi walio wengi Kenya, nikakuuliza vipi hii katiba mpya imejibu matatizo hayo?
1)Ukabila
2)Rushwa
3)Insecurity
4)unemployment
5)Pengo kati ya masikini na tajiri
6)Food security
7)Gharama za maisha kupanda
8)Dhuluma za watu kutorudishiwa ardhi zilizochukuliwa na wakoloni, baada ya uhuru zikachukuliwa na wanasiasa
Kuhusu jinsi ya kuchagua mawaziri, au kupinga matokeo, yote hayo uliyosema yanawalenga wanasiasa na viongozi wa juu, je katiba hii ni kwa ajili ya wanasiasa au hata watu wa chini?, hayo niliyoyataja ndiyo yanayowagusa watu wa chini, je yameshughulikiwa kwa kiasi gani?
Ninakuomba kwa sasa sahau kidogo kuhusu Tanzania, toa majibu, je tangu kutumika kwa hii katiba mpya, kati ya hayo mambo nane lipi limepatiwa ufumbuzi japo kupungua, changamoto za uchumi ni jambo la kawaida lakini tunataka kuona progress, sio kila mwaka hali inakuwa mbaya kuliko mwaka jana, tafadhali sana usitoke nje ya hayo niliyokuuliza, nijibu kwanza hayo mambo nane, ulinganishe kabla ya kuanza kutumika katiba mpya na baada ya kutumia katiba mpya, hali ya hayo mambo nane ikoje kwa sasa?
Inabidi nikujibu maana naona huu uzi una wasomaji wengi, hivyo kuna wadau wengi wanafuatilia huu mjadala, bure siwezi kupote muda ingekua ni wewe tu maana nyie ni kama 'robots', mnaishi kwa kukaririshwa.
Kwanza Tanzania haikwepi kutajwa humu kwa sababu kadhaa
- Kwamba wewe hapo ni Mtanzania unayeiponda katiba yetu, hivyo lazima kwanza ibidi niangalie hali ya Tanzania na kulinganisha na ya kwetu. Ni kama mtu anayekula kwenye taka/dampo anatoa ushauri kwa watu wanaokula manyumbani, huku akijifanya mshauri wa umuhimu wa lishe bora. Hivyo wewe hapo huna 'moral right' ya kuponda katiba ya Kenya maana upo kwenye dampo, kabisa maeneo ya taka, huna taarifa na chochote kinachohusiana na katiba nzuri, na wala hutegemei hata kwenye siku za hivi karibuni, labda miaka ya baadaye sana.
- Pili, mnapoponda katiba ya Kenya, lazima tuangalie majirani na kujilinganisha nao, yaani kwa kifupi nchi zote zilizotuzunguka hamna hata moja yenye sifa za kutuhoji. Tuko bora hatua mia moja huko mbele, hamna jirani hata mmoja kwenye level yetu. Matukio yenu ya kisiasa yapo tunayaona kila siku, mpo nyuma sana.
Katiba mpya nimekuambia imehusika pakubwa kwenye kurekebisha kero tulizokua nazo, inawezekana haijakamilisha asilimia 100% maana ni mchakato, sio tukio la siku moja, kuna uovu ulikua umekita mizizi tangu hata kabla ya nchi kupata uhuru, hivyo yote hayawezi kurekebishwa kwa mpigo mmoja. Lazima jitihada endelevu zitumike katika kufanikisha malengo ya katiba.
Cha msingi ni kwamba kila siku tunaona mafao na matunda ya katiba mpya nzuri, maana kila nikilinganisha na kipindi tukiwa na katiba dhalimu kama ya kwenu, naona afueni sana.
Tulizoea kuona
- Nyumba zikichomwa moto wakati wa uchaguzi
- Watu wakifukuzwa na kuwa wakimbizi kwenye nchi yao kila tukikaribia uchaguzi
- Mauaji ya Wakenya kisa ukabila
- Unyakuzi wa ardhi kiholela bila kuajibishwa
- Ufisadi wa wazi, hatamu hii mawaziri wamewajibishwa watano tukiona, kisa walitajwa tu.
- Rais kuwa na madaraka ya kuteua kwa kutumia vigezo vyake binafsi anavyovijua, kama ilivyo kwenu leo hii
- Uchumi wetu ulikua kwa asilimia 3%, leo hii tunapeta
- Miili ya watu ilikua inakutwa imetupwa maeneo, kama tunavyoona kwenu huku mkisema hao ni wahamiaji
- Tuizoea marais waliokua hawajaribiwi au kutajwa, kila walichokisema au amri zao zkilikua kama sheria
- Teuzi zilikua zinafanywa kwa misingi ya kikabila na ukanda bila aibu, leo hii kila uteuzi unahojiwa na kupitia bunge na taasisi zingine.
Hayo ni machache tu, naweza kuyaandika humu hadi msinzie mkiyasoma.
Kwa kifupi ni kwamba hatujafika, lakini hatua tunazopiga sasa hivi ni za mwendo kasi, tofauti na ilivyokua hapo awali. Katiba mpya imesababisha
- Ushindani baina ya gatuzi, kila gatuzi inajaribu kujinadi kwamba ndio salama kwa wawekezaji
- Miundo mbinu kama barabara za lami zimefika hadi Lodwar na Maralal maeneo ambapo walikua hawahisi kama wao Wakenya
- Shule karibia zote zimeunga kwenye umeme
- Tumeboresha mifumo ya afya, elimu n.k
- Usawa kwenye ugavi wa raslimali, maana ndio chanzo cha marumbano kwenye jamii
Changamoto zilizopo tunaendelea kuzikabili na kuvumbua mikakati tofauti ya kukabiliana nazo, ukuzingatia nchi yetu ni ndogo, na asilimia kubwa ni kame tupu ambapo ni tofauti na Tanzania ambayo ni muungano wa nchi mbili na ardhi kubwa yenye rotuba bila ukame wowote na madini na vivutio bora vya utalii kuzidi nchi zote Afrika lakini bado mnatajwa kwenye nchi maskini wa kutupwa.