Wakenya huu mswada uliopitishwa na wabunge wa Jubilee Alhamisi unaathiri vipi uchaguzi ujao?

Wakenya huu mswada uliopitishwa na wabunge wa Jubilee Alhamisi unaathiri vipi uchaguzi ujao?

NASA should go to court so as to petition these amendments. Uhuru is preparing clauses in the law that will enable him rig the election. He is doing everything to remain in office, so NASA be careful.

Watu walisema haraka sana kwamba kwa jirani yetu kuna demokrasia kubwa na kudharau hapa kwetu. Sijasikia wakijutia semi zao haya yakitokea.
 
Usianze kujishuku na kujihami mapema, mimi nimeuliza maswali ungenijibu badala ya kunishutumu. Sijasema hakuna mambo mazuri yaliyopatikana, ila nimesema mengi mazuri yanawalenga watu wakubwa na wanasiasa, na nimekua very specific kuainisha maeneo ambayo yanawagusa wananchi, hivi kweli bila aibu unasema ukabila Kenya umepungua, kweli unasema maneno hayo wewe bila aibu hata chembe? 2) Hivi kweli rushwa imepungua Kenya?, mwaka jana imeshika namba tatu duniani, 3) Hivi unataka kusema usalama wa raia wa Kenya umeimarika wakati Kenya imekua kinara Afrika katika extra judicial killings 2016, 4) Hivi unasema pengo la masikini na tajiri Kenya linapungua?. 5) Unataka kusema malalamiko ya ardhi yaliyofanyiwa kazi na tume ya wako yamefanyiwa kazi?, 6)Unataka tuamini kiwango cha unemployment kinashuka au kinaongezeka?. Kama unasema katiba mpya umeyapatia ufumbuzi hayo na ukatupa na ushahidi, basi kweli ni katiba nzuri, vinginevyo ni nyie wachache wanasiasa na watu wa hali nzuri ndiyo mnaouona huo uzuri
Nakubaliana na wewe mkuu yaani katiba inawa favor wanasiasa badala ya wananchi. Kwaiyo ukiingia kiundani wananchi wanachezeshwa shere tu mkuu.
 
Mimi ninaamini katiba nzuri ni ile inayoleta ufumbuzi wa matatizo ya wananchi walio wengi, ambao ni masikini, sio inayotoa ufumbuzi wa matatizo ya wanasiasa, ukisikiliza kwa makini sana huo unaoitwa uzuri katika katiba hiyo ya Kenya, mengi sana yanawalenga wanasiasa na viongozi wa juu, sio wananchi, mambo kama haya ya kupinga matokeo, kumpunguzia rais madaka na kadhalika, karibu yote yanawagusa wanasiasa au watu wa tabaka la juu. Kuna matatizo ya msingi yanawakabili wakenya tangu wapate uhuru 1963, tujiulize tangu katiba nzuri ipatikane, je kuna unafuu gani uliopatikana katika;
1) Kupunguza ukabila unaohatarisha nchi kugawanyika vipande vipande
2)Rushwa inayozidi kuongezeka na kuzidisha ugumu wa maisha
3) Kupunguza pengo la umasikini kati ya tajiri na masikini
4) Kushughulikia dhuluma iliyosababisha wachache matajiri na wanasia kujiridhisha ardhi ya wananchi wanyonge walioporwa na wakoloni kama ilivyopendekezwa katika The wako report
5) kuimarisha usalama ambao unazidi kuzorota
6) kuongeza ajira kwa vijana
7)Upatikanaji wa chakula cha uhakika(Food security)

Kama katiba haiwezi kuwapatia wakenya majibu katika hayo, basi huo uzuri wa katiba kwao hawatouona zaidi ya kuhudhuria mikutano ya wanasiasa ambao ndiyo wanufaika wakubwa wa hii katiba nzuri.
Nawakilisha
Umeongea facts kabisa mkuu.
 
Ndiyo ninawasngaa, nilianza kwa kusema siasa za Kenya ukizifuatilia unaweza kuwa chizi, nikamalizia kwa kusema "likiisha hili linakuja lingine, kwanini lakini?", wakitoka NASA, wanakuja Jubilee, hakuna hata wakumuamini.
Lakini ki msingi sio siasa za Kenya mbovu sababu sheria,mikakati ,kupunguzwa uwezo wa offisi ya rais ,tume kadhaa zilizopo - hizi zote ni ishara kwamba siyo siasa mbovu .Sema kile kibovu ni ubinafsi wa wanasiasa ndio unaharibu.
 
Lakini ki msingi sio siasa za Kenya mbovu sababu sheria,mikakati ,kupunguzwa uwezo wa offisi ya rais ,tume kadhaa zilizopo - hizi zote ni ishara kwamba siyo siasa mbovu .Sema kile kibovu ni ubinafsi wa wanasiasa ndio unaharibu.
Kwani siasa maana yake ninini?, siasa haimaanishi katiba tu, au sheria tu, hapana, ni mchanganyiko wa yote hayo na muhimu zaidi ni kwa jinsi gani watu au viongozi wanavyoishi au kuongoza kwa kufuata sheria na taratibu mlizojiwekea, inawezekana msiwe hata na katiba, lakini viongozi wakawa wanaongoza vizuri kwa kufuata misingi ya jamii husika

Katiba ni kitabu tu, hakina uwezo wa kutekeleza yaliyomo humo,mwatekelezaji ni sisi, tusipokuwa na utashi wa kuyatekeleza basi katiba inakua haina maana yoyote ile, ni kama utimilifu na uzuri wa Bible na msahafu, lakini maovu yanaendelea kama kawaida, sababu kubwa ni kwamba hakuna mtu wa kusimamia utekelezaji wake, angeshuka mwenyewe Mungu na rungu lake mkononi, ukikosea anakutwanga papo kwa papo, wote tungefuata. Muhimu zaidi ni kumpata msimamizi bora, mfano mzuri ni hapa Tanzania, hatujabadili katiba, ila tumebadili msimamizi, mambo yamebadilika kabisa ukilinganisha na utawala uliopita, Kikwete hata tungempa katiba nzuri kiasi gani, uwezo wake wa kusimamia mambo mbalimbali ulikua mdogo sana.
 
NASA should go to court so as to petition these amendments. Uhuru is preparing clauses in the law that will enable him rig the election. He is doing everything to remain in office, so NASA be careful.
Baada ya kuiga Eurobond na SGR money unategemea nn?
 
Siasa za Kenya ukizifuatilia sana unaweza kuwa chizi, hawa hawa Uhuru na Rutto walipambana sana kupata katiba mpya, baadae wakawa wanapita kuisifia na kuiaminisha dunia kwamba katiba ya Kenya is the best, hata vumbi halijafutika tayari imeonekana na dosari... wanasemaga siku ya kufa nyani, miti yote aliyozoea kuiparamia siku zote inaanza kuteleza...wakenya chokochoko hii, kuna kitu mnakitafuta, Mungu hajaribiwi, ukibeep yeye anapiga...chondechonde..kila siku mnakuja na jipya..kwanini lakini?
Ruto alikuwa against Katiba hii..Pitia vizuri utaona alifanya na kampeni nchi nzima kuipinga.
 
Kwani hao wawili wantofautiana vipi na hawa NASA jameni? Wanasiasa wa NASA walifurahia sana majority ruling kule supreme court sasa iweje ati majority vote bungeni nayo sasa ni kitu kibaya?
Majority rule inayopingana na Katiba. Wewe punga kwelu
 
NASA should go to court so as to petition these amendments. Uhuru is preparing clauses in the law that will enable him rig the election. He is doing everything to remain in office, so NASA be careful.

NASA know that if ballots are counted physically even by Angels will never win elections for the coming 100 years if they continue preaching hatred, tribalism, and keep on insisting on Jaluolism since they do not have number of votes in their favor. Note Baba has been aggressively leading demos so as to get rid of Luhyas and Somalis thrown out of IEBC while openly protecting his clansmen, consequently Somalis and practically half of Luhyas have deserted Baba!! Unfortunately, the flower boy Hon Musyoka has not noticed Baba's target. The Parliament has to ensure that both manual and electronic presidential procedures are adhered to and not only on electronic votes. In Germany or USA even U.K. do the same, why not Kenya.
 
Jamani tuache propaganda hamna mahali mswada huo umeiguzia supreme court ila mswada wenye unajaribu kuponya matatizo supreme court iliraise...msawada wenyewe ni mzuri if you go through it, itatuepushia matatizo mengi...imechapishwa kwenye gazeti za leo tuna fursa ya kuipitia tuache kuskiza propaganda



Surely what's wrong with NASA?
1. They went to Supreme Court saying some Form 34 A's were not signed by POs. The change pushed by Jubilee makes it a criminal offence for any PO to fail to sign Form 34A
2 They went to Supreme Court saying that CECs who are also Constituency Returning Officers did not sign Form 34B's. The amendment we seek will make it a criminal offence with a jail term of 5 years if they fail to sign 34 B's
3. They went to Supreme Court alleging that Wafula Chebukati announced the results before receiving all 34 A's and 34 B's. This amendment binds the National Returning Officer to receive all 34 As and 34Bs, validate them and reconcile them before announcing the Presidential Result
4. They went to Supreme Court saying that in some areas the electronic transmission failed due to unavailability of 3G and 4G networks. Agreed. This amendment makes the actual manual original Form 34A is the single source of truth in case there is no connectivity in a polling station
5. Good corporate governance demands that there is continuity in any organisation. If Wafula Chebukati is unwell at any one time, surely the IEBC should be able to perform.
6. As parliament we are required to vote with a two-thirds majority for motions and bills with far reaching consequences on the governance of this country.This amendment requires the same two thirds threshold on the decision of the Supreme Court and the IEBC.
NASA should be giving Jubilee a medal
 
wakati mwingine huwa natamani uongozi wa Magu kidogo....yaani hapa Kenya imekuwa ni sarakasi za kipumbavu for the last 6 months...vuta nikuvute ujinga mtupu...siasa za kijinga kwel kwel...wakati nchi kama ethiopia na tanzania ziko zinakimbia kwa haraka, Kenya ni IEBc, sijui Supreme court, sijui Nasa, sijui Jubilee, sijui election date imeahirishwa, sijui Chiloba, sijui maandamano, sijui matusi...smh
Aisee usimkufuru Mungu nyie mna raisi bora kabisa katika afrika
 
Acha kutuingiza choo cha kike wewe, taarifa zote zinaonyesha hayo niliyokutajia yanaongezeka mwaka had
Acha kutuingiza choo cha kike wewe, taarifa zote zinaonyesha hayo niliyokutajia yanaongezeka mwaka hadi mwaka leo unasema yanapungua, acha maneno weka muziki, ajenda kubwa kwenye uchaguzi mwaka huu ilikuwa ni rushwa, security, unemployment na hali ngumu ya maisha, insecurity Kenya inaongoza Africa kwa sasa, google uone hali ilivyo, unemployment inakaribia 48%, haijawahi kutokea tangu Kenya ipate uhuru wake, rushwa ndiyo usisema, rais mwenyewe amesalimu amri haiwezi, wewe unatuletea filimbi hapa, inflation is the highest hapa EAC, achana na Burundi na SS, acha maneno ya kienyeji wewe, Kenya kwa sasa ipo kwenye very bad shape than any time before.

Naona unazungukia pale pale bila kupiga hatu yoyote na kunipotezea muda.
Hayo unayotaja hapo ni changamoto za kiuchumi ambazo zinakumba mataifa yote. Tanzania hapo enzi za Jakaya ilikua kwa asilimia 7.2, leo hii mumerudi nyuma hadi 6.9

Kwa kifupi ukizingatia wakati tulikua na katiba mbovu kama ya kwenu, kuna mambo mengi sana yameboreshwa
- Wakati wa katiba mbovu, uchumi wa nchi yetu ulikua kwa asilimia 3, leo hii unakua kwa zaidi ya asilimia 5
- Wakati ule Kenya ilikua inaorodheshwa kwenye nchi maskini kama Tanzania, leo hii ni uchumi wa kati
- Tulizoea vita vya kikabila, kuchomeana nyumba kila wakati wa uchaguzi, leo hii tunaona maamuzi yanafanywa na mahakama huru. Sio kama kwenu rais anatangazwa moja kwa moja bila jinsi ya kulalamika.
- Maendeleo tunaona yanafikia maeneo ya mbali ambayo yalitelekezwa
- Tunaona mawaziri wanachaguliwa kwa kuzingatia sifa, wanapitia bunge na taasisi kadhaa kabla ya kukubalika, awali ilkua kama Tanzania ambapo sifa za waziri ilmradi anajua kusoma na kuandika tu.

kama nilivyokuambia nikiamua kuandika manufaa ya katiba mpya, hapa naweza kuorodhesha zaidi ya elfu moja, lakini haitakua na umuhimu wowote maana wewe hapo ulishakaririshwa. Hivyo kwaheri....
 
NASA know that if ballots are counted physically even by Angels will never win elections for the coming 100 years
Mmh! With all the smear campaigns preached on unga crisis and rampant corruption in the country, still NASA can't win? If that is the case, why Uhuru is becoming so ferocious and losing democratic direction? Since he is still in power Uhuru was expected to maintain calmness, humility and keep on waiting for the people of Kenya to decide. But now he seems to be making an attempt to divert the democratic channels forcing his way back to state house.
 
Kawaida ya Watanzania haswa nyie wa mlengo wa CCM mnapoijadili katiba ya Kenya huwa ni kama mumekaririshwa, yaani hayo yote umeandika hapo yameshughulkiwa pakubwa na katiba yetu mpya. Huwa mnajaribu kutumia huko kukaririshwa ili kuwaonyesha Watanzania kwamba hamna umuhimu wa wao kufuata katiba mpya. Huwa mnatumia nguvu nyingi sana.

Kwa ajili ya katiba mpya
- Maendeleo yameenea kwenye gatuzi zote hata maeneo ambayo yalikua yametelekezwa maiaka yote
- Maskini wa chini wameanza kuona haki ikitendeka
- Ukabila unapungua pakubwa maana watu walikua wameaminishwa raslimali zote zinaishia kati au Nairobi, leo hii mikoa na gatuzi zote zimepata fursa ya kutumia raslimali zao vizuri. Ni kama watu wa Mtwara waanze kuona umuhimu wa gesi.

Kuna vitu vingi sana ambavyo naweza kuandika, na kuna mada na hoja tulichangia sana humu, lakini kwa sababu upo kwa ajili ya kutafuta makosa hutaona chochote kizuri. Utatumia nguvu nyingi sana kupata wapi pa kukosoa ili uwatamaushe Watanzania wenzio wanaotamani kuwa na katiba mpya.
Gatuzi ninini
 
Naona unazungukia pale pale bila kupiga hatu yoyote na kunipotezea muda.
Hayo unayotaja hapo ni changamoto za kiuchumi ambazo zinakumba mataifa yote. Tanzania hapo enzi za Jakaya ilikua kwa asilimia 7.2, leo hii mumerudi nyuma hadi 6.9

Kwa kifupi ukizingatia wakati tulikua na katiba mbovu kama ya kwenu, kuna mambo mengi sana yameboreshwa
- Wakati wa katiba mbovu, uchumi wa nchi yetu ulikua kwa asilimia 3, leo hii unakua kwa zaidi ya asilimia 5
- Wakati ule Kenya ilikua inaorodheshwa kwenye nchi maskini kama Tanzania, leo hii ni uchumi wa kati
- Tulizoea vita vya kikabila, kuchomeana nyumba kila wakati wa uchaguzi, leo hii tunaona maamuzi yanafanywa na mahakama huru. Sio kama kwenu rais anatangazwa moja kwa moja bila jinsi ya kulalamika.
- Maendeleo tunaona yanafikia maeneo ya mbali ambayo yalitelekezwa
- Tunaona mawaziri wanachaguliwa kwa kuzingatia sifa, wanapitia bunge na taasisi kadhaa kabla ya kukubalika, awali ilkua kama Tanzania ambapo sifa za waziri ilmradi anajua kusoma na kuandika tu.

kama nilivyokuambia nikiamua kuandika manufaa ya katiba mpya, hapa naweza kuorodhesha zaidi ya elfu moja, lakini haitakua na umuhimu wowote maana wewe hapo ulishakaririshwa. Hivyo kwaheri....
Hivi wewe uelewa wako ukoje?, huko shule ulienda kufuata nini?, mimi sijazungumzia wala kulinganisha na Tanzania, mimi nimezungumzia katiba ya Kenya, nikawa ninasema katiba nzuri lazima ijubu na kutafutia kero za wananchi, acha kulinganisha na Tanzania kwanza, tukimaliza hapa ndiyo tulinganishe maendeleo yanayotokea Kenya na Tanzania, ninaamini utakimbia au kurusha matusi. Mimi nilikutajia mambo saba ambayo niliyatafsiri kama shida za msingi zinazowakabili wananchi walio wengi Kenya, nikakuuliza vipi hii katiba mpya imejibu matatizo hayo?
1)Ukabila
2)Rushwa
3)Insecurity
4)unemployment
5)Pengo kati ya masikini na tajiri
6)Food security
7)Gharama za maisha kupanda
8)Dhuluma za watu kutorudishiwa ardhi zilizochukuliwa na wakoloni, baada ya uhuru zikachukuliwa na wanasiasa

Kuhusu jinsi ya kuchagua mawaziri, au kupinga matokeo, yote hayo uliyosema yanawalenga wanasiasa na viongozi wa juu, je katiba hii ni kwa ajili ya wanasiasa au hata watu wa chini?, hayo niliyoyataja ndiyo yanayowagusa watu wa chini, je yameshughulikiwa kwa kiasi gani?

Ninakuomba kwa sasa sahau kidogo kuhusu Tanzania, toa majibu, je tangu kutumika kwa hii katiba mpya, kati ya hayo mambo nane lipi limepatiwa ufumbuzi japo kupungua, changamoto za uchumi ni jambo la kawaida lakini tunataka kuona progress, sio kila mwaka hali inakuwa mbaya kuliko mwaka jana, tafadhali sana usitoke nje ya hayo niliyokuuliza, nijibu kwanza hayo mambo nane, ulinganishe kabla ya kuanza kutumika katiba mpya na baada ya kutumia katiba mpya, hali ya hayo mambo nane ikoje kwa sasa?
 
Gatuzi ninini

Ugatuzi ni devolution mkuu. Gatuzi ni hizo sub counties na counties zilizopewa mamlka kiasi kujipigia bajeti na kuamua maendeleo wanayotaka kwenye gatuzi zao na mambo kama hayo. Gavana, MCA(madiwani), bunge za county na maseneta ndo wahusika wakuu kwenye shughuli za kufanikisha ugatuzi.
 
I understand the decision by Supreme Court to annul 2017 Presidential results was purely based on majority ruling. C.J Malaga was in fact praised worlwide what was termed as
historical ruling!
What i see now is that the Parliament is currently exercising it' s power which is line with the constitution of Kenya in the same manner with the supreme court ruling. There is absolutely nothing wrong with that!
My advice to NASA is for them to fully participate in the coming election otherwise they should stop complaining.
 
Poleni kenya. Ivi sisi waafrika ikulu ni peponi???????!!!!!!
 
Back
Top Bottom