Naona unazungukia pale pale bila kupiga hatu yoyote na kunipotezea muda.
Hayo unayotaja hapo ni changamoto za kiuchumi ambazo zinakumba mataifa yote. Tanzania hapo enzi za Jakaya ilikua kwa asilimia 7.2, leo hii mumerudi nyuma hadi 6.9
Kwa kifupi ukizingatia wakati tulikua na katiba mbovu kama ya kwenu, kuna mambo mengi sana yameboreshwa
- Wakati wa katiba mbovu, uchumi wa nchi yetu ulikua kwa asilimia 3, leo hii unakua kwa zaidi ya asilimia 5
- Wakati ule Kenya ilikua inaorodheshwa kwenye nchi maskini kama Tanzania, leo hii ni uchumi wa kati
- Tulizoea vita vya kikabila, kuchomeana nyumba kila wakati wa uchaguzi, leo hii tunaona maamuzi yanafanywa na mahakama huru. Sio kama kwenu rais anatangazwa moja kwa moja bila jinsi ya kulalamika.
- Maendeleo tunaona yanafikia maeneo ya mbali ambayo yalitelekezwa
- Tunaona mawaziri wanachaguliwa kwa kuzingatia sifa, wanapitia bunge na taasisi kadhaa kabla ya kukubalika, awali ilkua kama Tanzania ambapo sifa za waziri ilmradi anajua kusoma na kuandika tu.
kama nilivyokuambia nikiamua kuandika manufaa ya katiba mpya, hapa naweza kuorodhesha zaidi ya elfu moja, lakini haitakua na umuhimu wowote maana wewe hapo ulishakaririshwa. Hivyo kwaheri....
Hivi wewe uelewa wako ukoje?, huko shule ulienda kufuata nini?, mimi sijazungumzia wala kulinganisha na Tanzania, mimi nimezungumzia katiba ya Kenya, nikawa ninasema katiba nzuri lazima ijubu na kutafutia kero za wananchi, acha kulinganisha na Tanzania kwanza, tukimaliza hapa ndiyo tulinganishe maendeleo yanayotokea Kenya na Tanzania, ninaamini utakimbia au kurusha matusi. Mimi nilikutajia mambo saba ambayo niliyatafsiri kama shida za msingi zinazowakabili wananchi walio wengi Kenya, nikakuuliza vipi hii katiba mpya imejibu matatizo hayo?
1)Ukabila
2)Rushwa
3)Insecurity
4)unemployment
5)Pengo kati ya masikini na tajiri
6)Food security
7)Gharama za maisha kupanda
8)Dhuluma za watu kutorudishiwa ardhi zilizochukuliwa na wakoloni, baada ya uhuru zikachukuliwa na wanasiasa
Kuhusu jinsi ya kuchagua mawaziri, au kupinga matokeo, yote hayo uliyosema yanawalenga wanasiasa na viongozi wa juu, je katiba hii ni kwa ajili ya wanasiasa au hata watu wa chini?, hayo niliyoyataja ndiyo yanayowagusa watu wa chini, je yameshughulikiwa kwa kiasi gani?
Ninakuomba kwa sasa sahau kidogo kuhusu Tanzania, toa majibu, je tangu kutumika kwa hii katiba mpya, kati ya hayo mambo nane lipi limepatiwa ufumbuzi japo kupungua, changamoto za uchumi ni jambo la kawaida lakini tunataka kuona progress, sio kila mwaka hali inakuwa mbaya kuliko mwaka jana, tafadhali sana usitoke nje ya hayo niliyokuuliza, nijibu kwanza hayo mambo nane, ulinganishe kabla ya kuanza kutumika katiba mpya na baada ya kutumia katiba mpya, hali ya hayo mambo nane ikoje kwa sasa?