Wakenya, jamaa wanaandaa kukimbia kutokea Nairobi hadi Moshi Tanzania

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Halafu sio wanariadha wa kila siku tuliowazoea, hawa ni wadau wa kawaida tu, wanafanya maandalizi ya kukimbia kutokea Nairobi hadi Moshi, Tanzania kwa siku tano.

Yaani mzuka wa ajabu sana huu, dah!
Yote wanafanya kule Strava.

nai_arusha.jpg
 
Mtupe siri ni githeri ndio inatoa iyo energy au hua mnakula nn ndugu zetu lol

Sent using Jamii Forums mobile app

Siri wala hata sio msosi, ni kuwa obsessed na kitu unachokipenda, ukiwa na utashi wa kitu fulani unakiwaza muda wote, unajitia shauku la kufa mtu, yaani hadi ukifanikishe, unakua chizi fulani hivi. Akina Elon Musk na Ronaldo ndio zao hizi.

Elon Musk kuna wakati hujifungia ofisini wiki inaisha, kwa siku anapiga kazi masaa 17, wafanya kazi wanamuaga jioni na kumkuta asubuhi.
Ronaldo hupiga zoezi masaa manne kila siku, siku tano kwa wiki, inyeshe mvua ya masika au jua liangaze la kupasua vichwa huwa habadilishi hiyo ratiba.

Mimi binafsi pia nimejitoa ufahamu kwenye kitu fulani napambana nacho, nimefanya maamuzi ya huu uchizi na kuupokea kichwa kichwa. Nina imani Afrika tukiamua, kila kitu kinawezekana.
 
Ni hizo jamii huko pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku wazungu wakiwashtukia kuwa mnatumia mitishamba kuongeza nguvu ambayo wakipima kwa vipimo vyao inashindikana mmekwisha
 
Hauhitaji mitishamba kuyafanya haya, kumbuka sio mashindano, jamaa watakimbia siku tano ina maana watakua wakikodi na kulala kwenye mahoteli.
Ukipania unayafanya, unaweza ukaanza hapo kitaa, siku moja unakwenda kilomita moja halafu taratibu kadiri siku zinavyokwenda unaongeza kilomita, ipo siku utajikuta unaunganisha Dar-Moro.
Pia kama kukimbia kunashindikana basi nunua baiskeli, unakatiza nayo hadi mikoani.
Kuna madogo hapa Kenya waliendesha baiskeli hadi Mecca kuhiji
 
Hawa jamaa niliwakubali sana...walitoka msa, nairobi wakakatiza mpka moyale na kuingia ethiopia km sikosei

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu sio wanariadha wa kila siku tuliowazoea, hawa ni wadau wa kawaida tu, wanafanya maandalizi ya kukimbia kutokea Nairobi hadi Moshi, Tanzania kwa siku tano.

Yaani mzuka wa ajabu sana huu, dah!
Yote wanafanya kule Strava.

View attachment 1303668
Hongereni sana majirani. Miaka ya nyuma (enzi za kina Filbert Bayi) hata sisi tulikuwa wazuri kwenye riadha lakini alipokuja Waziri wa Elimu Joseph Mungai (ndugu yenu) akafuta michezo mashuleni na kila kitu kuanzia hapo kikaenda ovyo kabisa. Yaani tumefeli kwenye michezo yote!🤔...
 
Hehehe!! Huwa napenda mnavyojua kuelekeza vidole vya lawama Kenya kwa kila pungufu lenu, hamna siku hata moja huwa mnajielekezea kidole wenyewe. Mzembe siku zote hakosi mtu wa kumlaumu kwa kila anguko, ila wenye bidii wakidondokea pua hunyanyuka na kufuta vumbi na kulianzisha upya.
Huyo Mungai sio mara ya kwanza kuwaskia mkimlaumu kwa kila kitu huko kwenu, ila ni vigumu kuwaelewa kwenye haya ya lawama, mara mlaumu Mungai, mara ujamaa, mara Mkapa, mara Kikwete, mara mzee ruksa, mara Mjerumani aliyewakoloni mwanzo, mara vita vya Idd Amin, mara Kenya....yaani lawama kushoto kulia.
Leo hii mzee Magufuli ndio yaani mumemlaumu hadi kajizeekea balaa...hehehehe

Ni desturi mbovu sana ya kuishi maisha ya kulaumu laumu tu, na lipo hata kwenye maofisini huko, hakuna anayekubali kuwajibika, kwamba kete imesimama kwake na yeye ndiye anategemewa, lazima atatafuta wapi pa kuisogeshea.
Tungewaiga kwenye hayo ya lawama kwenye kainch ketu haka ambako zaidi ya nusu yake n kame tupu na hatuna madini dah! yaani sijui tungeshi vipi...
 
Hehehe!! Huwa napenda mnavyojua kuelekeza vidole vya lawama Kenya kwa kila pungufu lenu, hamna siku hata moja huwa mnajielekezea kidole wenyewe. Mzembe siku zote hakosi mtu wa kumlaumu kwa kila anguko, ila wenye bidii wakidondokea pua hunyanyuka na kufuta vumbi na kulianzisha upya.
Huyo Mungai sio mara ya kwanza kuwaskia mkimlaumu kwa kila kitu huko kwenu, ila ni vigumu kuwaelewa kwenye haya ya lawama, mara mlaumu Mungai, mara ujamaa, mara Mkapa, mara Kikwete, mara mzee ruksa, mara Mjerumani aliyewakoloni mwanzo, mara vita vya Idd Amin, mara Kenya....yaani lawama kushoto kulia.
Leo hii mzee Magufuli ndio yaani mumemlaumu hadi kajizeekea balaa...hehehehe

Ni desturi mbovu sana ya kuishi maisha ya kulaumu laumu tu, na lipo hata kwenye maofisini huko, hakuna anayekubali kuwajibika, kwamba kete imesimama kwake na yeye ndiye anategemewa, lazima atafuta wapi pa kuisogeshea.
Tungewiga kwenye hayo ya lawama kwenye kainch ketu haka ambako zaidi ya nusu yake n kame tupu na hatuna madini dah! yaani sijui tungeshi vipi...
Haha! Hatulaumu lakini ukweli lazima usemwe, sasa utajirekebishaje kama hujatafuta kujua mzizi wa tatizo? Mbona hata Kenya huwa mnalaumu sana, mmeshamlaumu sana Moi, mara Jomo Kenyatta, mara tatizo nchi ni kame, mara sijui Mchina kafanyaje!🤣🤣 Hii ndiyo Afrika, kila mmoja anapambana na hali yake...
 
Na mm naomba kujiunga wakati mkirudi toka Moshi kwennda Kajiado hadi Nairobi
nidokeze Malazi na msosi, wasije niacha njiani
pia michango nichangie kwa Dola au Kenya Money
 
Haha! Hatulaumu lakini ukweli lazima usemwe, sasa utajirekebishaje kama hujatafuta kujua mzizi wa tatizo? Mbona hata Kenya huwa mnalaumu sana, mmeshamlaumu sana Moi, mara Jomo Kenyatta, mara tatizo nchi ni kame, mara sijui Mchina kafanyaje!🤣🤣 Hii ndiyo Afrika, kila mmoja anapambana na hali yake...

Tofauti yetu na nyie ni kwamba sisi tutalaumu lakini tunapambana na kusonga mbele, ila nyie mumekaa hapo hapo mnalaumu, mpaka leo hamsikiki kwenye michezo, mkiulizwa mnalaumu kote kote. Sisi utatusikia tukilaumu Kenyatta, Moi ila hapo hapo utatuona kwenye mapicha kama haya.

Olympic+medal+count+%28top+15+countries%29+rank+by+Gold.jpg
 
Hongereni sana majirani. Miaka ya nyuma (enzi za kina Filbert Bayi) hata sisi tulikuwa wazuri kwenye riadha lakini alipokuja Waziri wa Elimu Joseph Mungai (ndugu yenu) akafuta michezo mashuleni na kila kitu kuanzia hapo kikaenda ovyo kabisa. Yaani tumefeli kwenye michezo yote!🤔...

Bishop Hiluka
Huyu hapa mwingine mwenye jina la Kikenya..yaani Njaga
Naye naona kakurupuka, hapa mtamsema hadi raha

2253297_tapatalk_1577354951190.jpeg
 
Haha! Siwezi kumlaumu mtu kwa kabila lake au sehemu anayotokea, hata kwenye suala la Joseph Mungai niliposema ndugu yenu ilikuwa jokes tu ila wewe ukachukulia serious. Kama ni kufanya madudu mbona huyu haingii hata robo ya ujinga wa viongozi wengine wengi wa mambo ya ovyo...
 
Tofauti yetu na nyie ni kwamba sisi tutalaumu lakini tunapambana na kusonga mbele, ila nyie mumekaa hapo hapo mnalaumu, mpaka leo hamsikiki kwenye michezo, mkiulizwa mnalaumu kote kote. Sisi utatusikia tukilaumu Kenyatta, Moi ila hapo hapo utatuona kwenye mapicha kama haya.

Olympic+medal+count+%28top+15+countries%29+rank+by+Gold.jpg
Sawa bhana, endeleeni kupiga mapicha sisi tutaendelea kuwa wapenzi watazamaji...
 
Tofauti yetu na nyie ni kwamba sisi tutalaumu lakini tunapambana na kusonga mbele, ila nyie mumekaa hapo hapo mnalaumu, mpaka leo hamsikiki kwenye michezo, mkiulizwa mnalaumu kote kote. Sisi utatusikia tukilaumu Kenyatta, Moi ila hapo hapo utatuona kwenye mapicha kama haya.
Olympic+medal+count+%28top+15+countries%29+rank+by+Gold.jpg
Tukifanya vitu kama hivi. 😎
4363903_cu44hdaw8aejpy_jpegf4b2ddab08fed12d5a49c21c32fa9ff2
 
Back
Top Bottom