Wakenya mna tatizo gani?

Emmanuel Robinson

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2013
Posts
1,856
Reaction score
1,793
*Hivi majuzi TV ya CITIZEN ya nchini Kenya ilitumia lugha isiyo ya kistaarabu dhidi ya Rais Magufuli kwa kumuita "mkaidi" walipokuwa wakikosoa mikakati yake ya kupambana na janga la Corona ambayo wao wanaona ni mikakati isiyofaa. Baada ya siku kadhaa, Tv hiyo ilijishtukia na kuanza kuomba msamaha kwa Rais Magufuli na Watanzania wote kwa siku 7 mfululizo na bado wanaendelea kuzihesabu.

Kinachonishangaza mimi ni comments zilizo nyingi kwenye social media za Tv hiyo ambapo Wakenya wengi wanaikosoa Tv hiyo kwa kuomba msamaha na wengine wanaona ni vema Tv hiyo ingeendelea kutukana Rais Magufuli. Sio mara ya kwanza kwa majirani zetu hawa kufakamia mambo ya Tanzania na kusahau changamoto zao za Ukabila na Al Shabaab. Kama ni Corona, wao wamethibitisha visa zaidi ya 260 lakini Tanzania haijafikia hata visa 200. Wamethibitisha vifo 11, Tanzania imethibitisha vitano tu. Kenya huwezi kuwa Rais kama kabila lako ni la wachache maana wenzetu wana ukabila kuanzia kwenye mauziano ya nyanya sokoni hadi kwenye chaguzi za Rais.

Mwaka jana kiongozi wao mmoja alisema kama polisi wasingewafukuza Watanzania kwenye eneo lake basi angeamuru wananchi wake kushika mawe na kuwatoa Watanzania kwa nguvu. Ukiachana na hayo, wenzetu wanadai Mlima Kilimanjaro uko kwao, Tanzanite iko kwao na hata Babu wa Loliondo walisema ni wa kwao.

Jirani akiacha mambo yake na kuanza kuhangaika na maisha yako ujue kuna kitu umemzidi na anaumia. Hali hiyo inanifanya nijivunie kuwa "Mtanzania" maana ni taifa ambalo watu wake wanakupigia kura bila kujua kabila lako na hawahitaji kulijua, wanaitana kaka na dada hata kama hawajuani na ukiuliza njia unasindikizwa tena bila masharti. Hayo pamoja na rasilimali tulizonazo ndio mambo yanayowaumiza jirani zetu. Ninawapa pole na ninakuomba *Mungu ibariki Tanzania* uzi huu ni kwa hisani ya rafiki yangu kutoka whatsapp
 
Hapa kwetu unaweza kuwa rais bila kuwa mwanaccm? CCM wapo wangapi nchi hii? Hapo tofauti yetu na Kenya ni Nini?
 
Tusihangaike na wakenya,tuhangaike na corona,tukiishinda watanyamaza.
Mkuu Kama hatupimi na kwenye mabasi tunajazana still tuna confirmed cases 200 na vifoo kadhaa,hapo tunatoboa vipi? Labda kile kitengo za IT cha January kirudi kazini kuchakachua data otherwise huko mbele ni aibu
 
Kwanini mnaumizwa na wakenya kutusema vibaya, wapuuzeni, wachaneni nao, nyie mkiishi uswahilini mtakufa saa mbili asubuhi kwa pressure, wengine tunanawiri kwa kusemwa vibaya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa Wakenya wameumia sana baada ya kuingia serikali ya awamu ya tano imewapigwa stop mambo mengi sana ambayo walikuwa wanafaidika nayo ikiwemo ajira za kazi walikuwa wamejazana sana TZ sasa hawapati vibali vya ajira za kazi tena unless awe na professional isiyopatikana hapa TZ. Pia wamepigwa stop kwenye Tanzanite walikuwa wanashirikiana na wahindi kutorosha madini yetu kwenda India mpaka wakawa wasafirishaji wa pili duniani wa Tanzanite hayo ni baadhi ya mambo yanayowafanya waichukie Tanzania lakini haturudi nyuma mpaka watanyooka tu kama ambavyo tunavyowanyoosha wasaliti wa ndani. HAPA KAZI TU!
 
Nyinyi mlipochoma moto vifaranga vyao mlikuwa mnawaza nini ?
 
Wewe una waona wakenya wana akili timamu?.
yaani hao hawana tofauti na wanyama .
Angalia taarifa zao za habari.
haipiti siku utasikia kuna mtu kampige mwenzie shoka kamuua,mara mtu kakatwa masikio kwa kisu yaani ni mambo ya ajabu ajabu tu.

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"
 
Swali la msingi; Je, kwa ujumla wake ni mkaidi au wanamsingizia? Tuiweke kwanza Corona pembeni tujibu hili swali. πŸƒπŸƒπŸƒπŸ’¨πŸ’¨
 
They are smarter, hawaamini juju kama wabongo wengi
 
"Mbingu haiwezi kuwa na wivu na dunia hata siku moja"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanatuambia ukweli toka lini ugonjwa unaoepukika kisayansi ukaepukika kwa maombi, ishiii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…