Emmanuel Robinson
JF-Expert Member
- May 29, 2013
- 1,856
- 1,793
*Hivi majuzi TV ya CITIZEN ya nchini Kenya ilitumia lugha isiyo ya kistaarabu dhidi ya Rais Magufuli kwa kumuita "mkaidi" walipokuwa wakikosoa mikakati yake ya kupambana na janga la Corona ambayo wao wanaona ni mikakati isiyofaa. Baada ya siku kadhaa, Tv hiyo ilijishtukia na kuanza kuomba msamaha kwa Rais Magufuli na Watanzania wote kwa siku 7 mfululizo na bado wanaendelea kuzihesabu.
Kinachonishangaza mimi ni comments zilizo nyingi kwenye social media za Tv hiyo ambapo Wakenya wengi wanaikosoa Tv hiyo kwa kuomba msamaha na wengine wanaona ni vema Tv hiyo ingeendelea kutukana Rais Magufuli. Sio mara ya kwanza kwa majirani zetu hawa kufakamia mambo ya Tanzania na kusahau changamoto zao za Ukabila na Al Shabaab. Kama ni Corona, wao wamethibitisha visa zaidi ya 260 lakini Tanzania haijafikia hata visa 200. Wamethibitisha vifo 11, Tanzania imethibitisha vitano tu. Kenya huwezi kuwa Rais kama kabila lako ni la wachache maana wenzetu wana ukabila kuanzia kwenye mauziano ya nyanya sokoni hadi kwenye chaguzi za Rais.
Mwaka jana kiongozi wao mmoja alisema kama polisi wasingewafukuza Watanzania kwenye eneo lake basi angeamuru wananchi wake kushika mawe na kuwatoa Watanzania kwa nguvu. Ukiachana na hayo, wenzetu wanadai Mlima Kilimanjaro uko kwao, Tanzanite iko kwao na hata Babu wa Loliondo walisema ni wa kwao.
Jirani akiacha mambo yake na kuanza kuhangaika na maisha yako ujue kuna kitu umemzidi na anaumia. Hali hiyo inanifanya nijivunie kuwa "Mtanzania" maana ni taifa ambalo watu wake wanakupigia kura bila kujua kabila lako na hawahitaji kulijua, wanaitana kaka na dada hata kama hawajuani na ukiuliza njia unasindikizwa tena bila masharti. Hayo pamoja na rasilimali tulizonazo ndio mambo yanayowaumiza jirani zetu. Ninawapa pole na ninakuomba *Mungu ibariki Tanzania* uzi huu ni kwa hisani ya rafiki yangu kutoka whatsapp