MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Sikusudii kusema kwa niaba ya Wakenya, ila nashangaa kama wao kitu gani hicho Citizen wanaombea msamaha, kiukweli hayo ya Magufuli kusema hatofunga makanisa, misikiti, mipaka na maeneo yote ya misongamano na kuambia watu waendelee na maisha yao kama kawaida yangesemwa na rais Uhuru, angetamani kuihama Kenya maana huku kwetu tunatambua urais ni taasisi ya umma na lazima uendeshwe kitaalam sio kwa hisia au imani za mtu au dini.