Wakenya na Kingereza

game over

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2016
Posts
10,727
Reaction score
24,840
Nimekuwa nikiliangalia hili kwa kitambo kidogo,
Nimetembelea Kenya mara kadhaa na nimeshangazwa kwa kweli.
Tofauti na Tanzania ambapo matumizi ya Kingereza kwa sehemu kubwa ni mashuleni na sehemu chache sana zenye miingiliano ya wageni, Kenya unakuta kila mkenya anaongea Kingereza, pamoja na kuwa wengi wao wanaongea, kuandika na kuelewa Kiswahili, nadiriki kusema matumizi ya kingereza na kiswahili Kenya ni 50/50.
Utakuta mkenya ana hali ngumu mno ya maisha lakini anaongea kingereza hatari, mtu hana hata 10 mfukoni, jua kali, amechomekea suti kachumbali na tai, koti la suti la mtumba oversize, njaa imempiga mbaya ila anaongea kingereza kizuri mno huwezi amini, wakati huku tz watu wanakwambia kingereza bila hela ni sawa na kupiga kelele, hali ni tofauti kabisa kwa hawa majirani zetu, mtu anaishi Kibera kwenye banda lakini anaongea kingereza kama anaishi Nottingham.
Sijui mnajifunzaje wenzetu maana sie tulishashindwa na tunasemaga kilikujaga na meli bwana,
kuna bwana yule anaitwa prof Lumumba nani sijui, anaandikaga tweeter Kingereza kigumu hata waingereza wenyewe hawaelewi, sijui hata hao anaowaandikia kama huwa wanaelewa.

Hahahahaha,
Nihitimishe kwa Kusema, Kwa kweli kwa hili kwangu mimi binafsi majirani mmekuwa na mchango mkubwa sana Kuniongezea siku za Kuishi.πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Mimi sijaelewa kabisa mkuu kuwa ukiongea kiingereza ndio usomi/utajiri au vp?
Kuwa na kitu au kutokuwa nacho kunahusianaje na kiinglish?

Hii ni lugha tu kama kimakonde, ukizaliwa na ukakikuta kinaongelewa ndicho utakachoongea.
HIVI unaelewa kuwa Wakenya hawana lugha yao rasmi ya kuwasiliana kama taifa?

Tz tuna kiswahili na hii ndiyo lugha inayotufanya tuwasiliane, lkn wao wana lugha za kimakabila, kwa hiyo walilazimika kuwa na lugha ya kuwaunganisha ambapo Kiingereza ndicho kimeokoa jahazi, na sasa wanajitahidi kiswahili kibovu ili waendane na jirani zao.
Simaanishi kuongea kiingereza ni vibaya hasa ukizingatia ndiyo lugha ya dunia kibiashara, bali najaribu kueleza sababu ya wao kuongea lugha hii zaidi
 
limbukeni mwingine huyu! Yuko overexcited na lugha ya Queen.
 
Mkuu unamatatizo kwenye akili yako nenda kapate dawa upone ugonjwa wako wa akili ya kitumwa!
 
kama watu ndio wana fikra kama zako [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Mungu awasamehe
 
Mkuu unamatatizo kwenye akili yako nenda kapate dawa upone ugonjwa wako wa akili ya kitumwa!
hahaha, nakupa nafasi nyingene usome tena bandiko pengine utang'amua walau sehemu ya mantiki ya bandiko langu
 
Kujua lugha zaidi ya moja kuna faida kubwa sana. Hasa lugha za kimataifa. Kuna fungua milango mingi ya maisha. Waingereza wenyewe wanapenda watoto wao wajifunze Spanish, French au Germany
 
kama mimi na wewe tunaelewana kiswahili na tunakimudu vizuri, Kuna haja gani ya kutumia Lugha ya Kigeni?
 
Inamaana ulituharibu sana mkuu lakini hii generation ya watoto waliosoma English medium itatuokoa
 
kama mimi na wewe tunaelewana kiswahili na tunakimudu vizuri, Kuna haja gani ya kutumia Lugha ya Kigeni?
Haina haja, lugha sio ufahari au utajiri bali lugha kusudio kubwa ni mawasiliano, nitatumia kifaransa/kiingereza/kijerumani pale tu ninapolazimika kuwasiliana na mtumiaji wa lugha husika endapo hajui kutumia lugha yangu.
Hivi leo wasawahili tuamke ghafla wote tuanze kuongea kimalikia bila sababu yoyote ni ulimbukeni na ujuha
 

Kama jinsi huwa nasema mara nyingi, Kenya hatuna kile kitu huitwa 'herd mentality', au kufugwa wote kwenye zizi moja la lugha, tunaongea lugha nyingi tukianza na zetu za asili, halafu Kiswahili na Kingereza zinatuunganisha kama taifa na pia kutuunga kwenye mataifa mengine.
Mwisho wa siku umuhimu wa lugha ni ueleweke unachokisema kwenye mawasiliano, na kila lugha ina mafao yake
- Lugha ya asili inaniunganisha na asili yangu kwa mababu zangu, sio kuishi kama sharobaro lisilo na kwao
- Kiswahili kinanisaidia kuwasiliana na watu wasio wa asili yangu ndani ya taifa na pia nchi jirani
- Kingereza kina umuhimu mkubwa sana kwangu kwenye michongo yangu, biashara za kimataifa bila kingereza unakua zero, maisha ya sasa yanategemea utaalam wa lugha ya kingereza, hata Wachina na nchi za mashariki na bara Asia wamelitambua hili na wapo mbioni kuhakikisha raia wake hawachelewi kujiunga kwenye lugha hii.

Cha msingi, lazima uwe mjanja wa lugha sio unakaa kwenye mabanda ya Tandale kama zezeta asiye na mbele wala nyuma, jifunze na kuongea walau lugha tano. Lakini usitelekeze yako ya asili, kama Msukuma ongea mpaka chote, kama Mnyakyusa jua lugha ya sili yako.

Utafiti wa kisayansi uligundua kwamba watu wenye uwezo wa kuongea na kuandika lugha kadhaa huwa bora hata kimawazo. Wafundisheni watoto wenu na vijana wa kwenu kama mnataka kuwa washindani kimataifa, la sivyo fursa zitakua zinawapita, viongozi wenu wakiogopa kutoka na kusingizia eti wanabana matumizi.
 
Kujua lugha zaidi ya moja kuna raids kubwa sana. Hasa lugha za kimataifa. Kuna fungus milango mingi ya maisha. Waingereza wenyewe wanapenda wastoto wao wajifunze Spanish, French au Germany
Nakubaliana na wewe,
Hata mimi sasa hivi najifunza Kiitaliano, nikipata walau basics nitaanza French, Lugha ya Tano. Lakini Tunavyochukulia hizi Lugha ni Tofauti sana, and probably that was my point.
 
Kumbe akili za watu wachache kama wewe ndio huwa zinawachafulia sifa watanzania? Naona wenzako wameamua kukuelemisha. Safi sana. Uzi wako wakuwaponda wakenya kuhusu mambo yasioeleweka umekugeukia.
 
Jirani huku Kwamtogole tunakijua Kimalkia na sisi tuna watch BBC World News. Unafikiri bado tuko kwenye Things Fall Apart?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…