game over
JF-Expert Member
- Jan 1, 2016
- 10,727
- 24,840
Nimekuwa nikiliangalia hili kwa kitambo kidogo,
Nimetembelea Kenya mara kadhaa na nimeshangazwa kwa kweli.
Tofauti na Tanzania ambapo matumizi ya Kingereza kwa sehemu kubwa ni mashuleni na sehemu chache sana zenye miingiliano ya wageni, Kenya unakuta kila mkenya anaongea Kingereza, pamoja na kuwa wengi wao wanaongea, kuandika na kuelewa Kiswahili, nadiriki kusema matumizi ya kingereza na kiswahili Kenya ni 50/50.
Utakuta mkenya ana hali ngumu mno ya maisha lakini anaongea kingereza hatari, mtu hana hata 10 mfukoni, jua kali, amechomekea suti kachumbali na tai, koti la suti la mtumba oversize, njaa imempiga mbaya ila anaongea kingereza kizuri mno huwezi amini, wakati huku tz watu wanakwambia kingereza bila hela ni sawa na kupiga kelele, hali ni tofauti kabisa kwa hawa majirani zetu, mtu anaishi Kibera kwenye banda lakini anaongea kingereza kama anaishi Nottingham.
Sijui mnajifunzaje wenzetu maana sie tulishashindwa na tunasemaga kilikujaga na meli bwana,
kuna bwana yule anaitwa prof Lumumba nani sijui, anaandikaga tweeter Kingereza kigumu hata waingereza wenyewe hawaelewi, sijui hata hao anaowaandikia kama huwa wanaelewa.
Hahahahaha,
Nihitimishe kwa Kusema, Kwa kweli kwa hili kwangu mimi binafsi majirani mmekuwa na mchango mkubwa sana Kuniongezea siku za Kuishi.😀😀😀😀😀😀