Kama jinsi huwa nasema mara nyingi, Kenya hatuna kile kitu huitwa 'herd mentality', au kufugwa wote kwenye zizi moja la lugha, tunaongea lugha nyingi tukianza na zetu za asili, halafu Kiswahili na Kingereza zinatuunganisha kama taifa na pia kutuunga kwenye mataifa mengine.
Mwisho wa siku umuhimu wa lugha ni ueleweke unachokisema kwenye mawasiliano, na kila lugha ina mafao yake
- Lugha ya asili inaniunganisha na asili yangu kwa mababu zangu, sio kuishi kama sharobaro lisilo na kwao
- Kiswahili kinanisaidia kuwasiliana na watu wasio wa asili yangu ndani ya taifa na pia nchi jirani
- Kingereza kina umuhimu mkubwa sana kwangu kwenye michongo yangu, biashara za kimataifa bila kingereza unakua zero, maisha ya sasa yanategemea utaalam wa lugha ya kingereza, hata Wachina na nchi za mashariki na bara Asia wamelitambua hili na wapo mbioni kuhakikisha raia wake hawachelewi kujiunga kwenye lugha hii.
Cha msingi, lazima uwe mjanja wa lugha sio unakaa kwenye mabanda ya Tandale kama zezeta asiye na mbele wala nyuma, jifunze na kuongea walau lugha tano. Lakini usitelekeze yako ya asili, kama Msukuma ongea mpaka chote, kama Mnyakyusa jua lugha ya sili yako.
Utafiti wa kisayansi uligundua kwamba watu wenye uwezo wa kuongea na kuandika lugha kadhaa huwa bora hata kimawazo. Wafundisheni watoto wenu na vijana wa kwenu kama mnataka kuwa washindani kimataifa, la sivyo fursa zitakua zinawapita, viongozi wenu wakiogopa kutoka na kusingizia eti wanabana matumizi.