GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Ingawa wakati mwingine Watanzania na Wakenya hushambuliana kwenye mitandao ya kijamii, haimaanishi kuwa ni maadui. Utani wao ni kama ugomvi wa watoto wanaofuatana kuzaliwa.
Linapokuja suala la shida au changamoto, uhalisia wa mahusiano yao hujithihirisha. Husaidiana.
Ingawa Watanzania na Wakenya ni ndugu wanaopendana, Wakenya wanaonekana wana roho nzuri sana. Takwimu zinaonesha kuwa Kenya imeshaifanyia Tanzania mambo mengi mazuri kuliko iliyofanyiwa na Tanzania.
1. Wakati wa vita vya Kagera, Kenya iliipatia Tanzania ushirikiano uliowezesha JWTZ kuteka ndege ya Libya ikiwa na wanajeshi wa Libya waliokuwa wanaenda kumsaidia Idd Amin.
2. Kagera ilipokumbwa na tetemeko la ardhi, Kenya ilituma msaada wa kuwasaidia wahanga.
3. Baada ya Tundu Lissu kupigiwa risasi, alienda kutibiwa Nairobi nchini Kenya. Sijui kama angepata huduma bora kama hiyo kama angepelekwa Kigali nchini Rwanda.
4. Baada ya Godbless Lema kuamua kukimbia nchini kwa madai kuwa maisha yake yalikuwa hatarini, ni Kenya ndiyo ilimsaidia kutorokea huko alikokimbilia. Inasemekana Serikali ya Tanzania ilitaka Lema arudishwe nchini lakini Kenya ikagoma. Vipi kama angepitia Uganda, Museveni angekubali?
5. Baada ya mwimbaji wa nyimbo za Injili, Rose Muhando kuugua, alienda kupata matibabu nchini Kenya. Hakutumia fedha zake binafsi. Alihudumiwa kwa fedha na rasilimali za Wakenya. Sijui ingekuwaje kama angeipata hiyo changamoto akiwa nchini Burundi. Ndiyo maana baada ya kupona, alitunga wimbo kuishukuru Kenya kwa kumsaidia.
6. Serikali ya Kenya ilipokamata dhahabu iliyosadikika ilitoroshwa kutoka Tanzania, Rais Uhuru Kenyatta aliamuru zirejeshwe Tanzania. Hakujali kuwa Tanzania ilishawahi kuchoma vifaranga vilivyotoka Kenya. Zilirejeshwa kwa kutumia ndege ya Jeshi la Kenya, nafikiri.
7. Baada ya Wamasai wa Loliondo kuparurana na Jeshi la Polisi, majeruhi wa Kimasai walienda kutibiwa nchini Kenya. Walikuwa na amani zaidi kwenda kutibiwa nchi jirani, Kenya, kuliko nchini kwao.
Kwa mifano hiyo michache na mingi inayofanana nayo, ni halali Watanzania wakisema "Mungu ibariki Kenya".