Tony254
JF-Expert Member
- May 11, 2017
- 16,017
- 16,431
Tayari wanatawala hicho kipande cha North West Kenya.Duh...si kwa sifa hizo..waingizeni jeshini Sasa..alafu muwape hicho kipande watawale
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tayari wanatawala hicho kipande cha North West Kenya.Duh...si kwa sifa hizo..waingizeni jeshini Sasa..alafu muwape hicho kipande watawale
So serikali haiwaingiliiTayari wanatawala hicho kipande cha North West Kenya.
Hahahaha, jukumu la kwamba la Serikali zote makini ni kulinda raia wake dhidi ya maadui wa ndani na nje ya nchi, hilo ndio jukumu mama( Primary responsibility of any responsible government), Serikali ikifikia hatua ya kutaka raia wake wajilinde wenyewe hiyo ni " Failed Government'.unataka silaha zao zichukuliwe wajilinde vipi? mipaka ya kenya na Ethiopia na South Sudan ni mikubwa .. kabila kutoka upande huo mwingine wa mpaka zitakuwa zinawashambulia ovyo ovyo... Serikali inashughulika tu WaKenya wakianza kushambuliana wenyewe kwa wenyewe..
Kwahiyo huko GoK haitawali wao wapo na nchi yao sio?, sasa kwanini mnalalamika mkiwekwa katika kundi la "Failed state?"Tayari wanatawala hicho kipande cha North West Kenya.
Hahahaha, jukumu la kwamba la Serikali zote makini ni kulinda raia wake dhidi ya maadui wa ndani na nje ya nchi, hilo ndio jukumu mama(Primary responsibility of any responsible government), Serikali ikifikia hatua ya kutaka raia wake wajilinde wenyewe hiyo ni " Failed Government'.
Upumbavu wenu umepiliza mipaka, kwani hawa wafugaji wamepewa silaha na mafunzo na Serikali, "_does GoK Kenya has any control on them?, they are bandits who own guns illegally, that's why they kill police and law enforcement staff. Do you consider illegal arm holders to be reserve armies?. Kenya is real a Failed state.Dis-arming them would be very un-fair , ... endelea na mbwe-mbwe zako za failed govt.
The govt uses reserves from the community who are trained and given guns to provide extra policing
There are bandits and there are true community reserves.Upumbavu wenu umepiliza mipaka, kwani hawa wafugaji wamepewa silaha na mafunzo na Serikali, "_does GoK Kenya has any control on them?, they are bandits who own guns illegally, that's why they kill police and law enforcement staff. Do you consider illegal arm holders to be reserve armies? Kenya is real a Failed state.
Tuna police reserve maeneo hayo. Hawa reserve wamepewa mafunzo na silaha na serikali ya Kenya. Tatizo ni hawa reserve ni wachache na wana bunduki nzee kushinda wafugaji, ile unapiga risasi moja kisha unakoki tena ndio upige risasi nyingine.Upumbavu wenu umepiliza mipaka, kwani hawa wafugaji wamepewa silaha na mafunzo na Serikali, "_does GoK Kenya has any control on them?, they are bandits who own guns illegally, that's why they kill police and law enforcement staff. Do you consider illegal arm holders to be reserve armies?. Kenya is real a Failed state.
Tunazungumzia hawa wenye silaha za kivita kinyume cha sheria na Serikali inajua lakini ni kama vile umeshindwa kushughulika nao. Sasa Kenya mtapataje amani kama hizi sila zipo mikononi mwa watu masikini kama hawa?, wakati wowote hizi silaha zinaweza kuingia katika miji mikubwa na kusababisha maafa.Tuna police reserve maeneo hayo. Hawa reserve wamepewa mafunzo na silaha na serikali ya Kenya. Tatizo ni hawa reserve ni wachache na wana bunduki nzee kushinda wafugaji, ile unapiga risasi moja kisha unakoki tena ndio upige risasi nyingine
Tunazungumzia hawa wenye silaha za kivita kinyume cha sheria na Serikali inajua lakini ni kama vile umeshindwa kushughulika nao. Sasa Kenya mtapataje amani kama hizi sila zipo mikononi mwa watu masikini kama hawa?, wakati wowote hizi silaha zinaweza kuingia katika miji mikubwa na kusababisha maafa.
Kwahiyo mumewashindwa kuwadhibiti?, kifupi ni kwamba Serikali ya Kenya imeshindwa kuwalinda raia wake ndio sababu wameamua kujilinda wenyewe, hiyo ndio sifa kubwa inayoifanya nchi kuwekwa katika kundi la " Failed state".Wamekuwa na silaha kwa miaka zaidi ya arubaini na bado maisha inaendelea hapa Kenya. Wanaolia ni akina Uganda ambao wanataka kuiba ng'ombe ila hawataki mapigo. Ukiiba ng'ombe ya mwenzako kuwa tayari kupigwa na tena usilie, mwiba wa kujidunga hauambiwi pole.
Halafu tukirudi kwa mawazo ya kuwanyang'anya silaha, serikali imefanya hivyo zaidi ya mara tano kuanzia miaka ya 1980's lakini kila mara wakipokonywa, wanaenda kununua kutoka South Sudan au Ethiopia. Kuna picha maarufu ya rais Moi akichoma bunduki nyingi zilizorundikwa pamoja. Hawa watu wakikosa silaha, jamii ya Watoposa inatokea South Sudan, inakuja kuwaua na kuiba ng'ombe zao.
Wacha wajilinde kwani shida iko wapi? Wewe endelea kutuita failed state tu sisi maisha inaendeleaKwahiyo mumewashindwa kuwadhibiti?, kifupi ni kwamba Serikali ya Kenya imeshindwa kuwalinda raia wake ndio sababu wameamua kujilinda wenyewe, hiyo ndio sifa kubwa inayoifanya nchi kuwekwa katika kundi la " Failed state".
Shida ni kukosekana kwa usalama na raia kuuliwa Mara kwa Mara, kumbuka kuna mauaji yanaendelea Mara kwa Mara huko Kenya, hizi silaha zinazomilikiwa kiholela zonatumika pakubwa katika hayo matukio ya ujambazi, sio jambo la kulichukulia poa kwasababu huwezi jua kama kuna siku wewe au jamaa yako wa karibu anaweza kuathirika kutoka na hizi silaha.Wacha wajilinde kwani shida iko wapi? Wewe endelea kutuita failed state tu sisi maisha inaendelea
Speaking of Congo....hakuna operation Tz imeshindwa
Nigeria's Boko Haram, Libya, kuna makundi kule Egypt, Ethiopia, na kwa hizi Tz hamughusi hata kidogo. Hizi nchi zina jeshi za maana kuliko Tz kwa mbali tena sana, ila kuna makundi wanasumbua ndani ya chi! Mambo ya vita na siasa si mchezo.Hakuna Taifa lolote linaloshindwa kuwadhibiti raia wake, labda "Failed state". Hivi inakuingiaje akili kweli nchi inajua kwamba kuna jamii Fulani au kikundi cha watu kinamiliki silaha za kivita na hakuna hatua zozote zinazochuliwa ili kuwanyang'anya hizo silaha, taja nchi yoyote zaidi ya DRC, SS, Somalia na Kenya.
Hao Karamoja waliokuja ni wale ambao hawajulikani kama wanasilaha, kumbuka hata huku Tanzania bado kuna watu wanazo silaha, lakini Serikali haijui, ila Serikali ikijua, lazima wataifuata na kuichukua. Hata hao Karamoja ni miongoni mwa wale wachache ambao wamezificha na Serikali ya Uganda haijui, ikitokea wizi kama huo, lazima Serikali ya Uganda watazifuatilia hizo silaha ili wazichukue.
Tofauti na Kenya ni kwamba, Kenya mnajua jamii zenye silaha lakini mnaogopa kwenda kuzichukua, yaani Serikali inaogopa raia wake?, kweli Kenya ni Failed state
Njooni nyinyiFighting rebels comprising of forced child soldiers sio kitu cha kujivunia[emoji23][emoji23]
Wakati mwengine ninashindwa kushangaa jinsi mlivyo na akili ndogo kuelewa. Hakuna nchi inayovumilia raia wake kumiliki silaha haramu, lazima wataanzisha juhudi/mapambano kuzitafuta, hizo nchi zote ulizotaja wapo katika vita ili kuzikamata hizo silaha, Kenya mnasema ni muhimu hao watu kumiliki silaha haramu ili kujilinda na maadui zao.Nigeria's Boko Haram, Libya, kuna makundi kule Egypt, Ethiopia, na kwa hizi Tz hamughusi hata kidogo. Hizi nchi zina jeshi za maana kuliko Tz kwa mbali tena sana, ila kuna makundi wanasumbua ndani ya chi! Mambo ya vita na siasa si mchezo.
Tanzania watu wenyu ni watulivu na washamba pia, serikali inawadanganya na kuwatisha kirahisi rahisi, haimaanishi eti mko sawa, ni ile hampendi fujo. Waoga waoga hivi. [emoji23][emoji23]
Wakati mwengine ninashindwa kushangaa jinsi mlivyo na akili ndogo kuelewa. Hakuna nchi inayovumilia raia wake kumiliki silaha haramu, lazima wataanzisha juhudi/mapambano kuzitafuta, hizo nchi zote ulizotaja wapo katika vita ili kuzikamata hizo silaha, Kenya mnasema ni muhimu hao watu kumiliki silaha haramu ili kujilinda na maadui zao.
Katika hizo nchi ulizotaja, taja nchi ambayo haipo katika mapambano ya kuzikamata hizo silaha, kwa ujumla hizo nchi zote zipo katika vita na hivyo vikundi vyenye silaha, haiwezikani ndani ya nchi kuwepo na silaha haramu, Serikali inajua nani mwenye kumiliki silaha haramu, na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa, hiyo hutokea katika "Failed states" pekee.
Shida hua ni maendeleo, mahali ambapo hapana uchumi siku zote panaachwa na kutengwa hata na serekali.... Hii ndio maana kuna wakati flani mwaka uliopita Kenya na Ethiopia walitia mkataba kwamba kutajengwa industrial complex hapo mpakani mwa Kenya na Ethiopia kama vile mpaka wa north na south korea.....Duh! Sio mchezo. Inaelekea ni ngumu sana ku-maintain order pande hizo hao jamaa wakichafukwa roho.
Yafaa muweke vikosi vya kueleweka huko mpakani kuzuia smuggling ya hizo silaha.
Katika hilo hakuna cha kujitetea, ni jukumu la nchi kuhakikisha usalama katika maeneo yake yote bila kujali kuna maendeleo au hakuna, kuna nchi nyingi sana zinaumasiki mkubwa zaidi ya huko Turkana na Pokot, lakini bado usalama umeimarishwa, Serikali kamwe haiwezi kuvumilia uvunjifu wa amani na sheria kwa watu kumiliki silaha kinyume cha sheria.Shida hua ni maendeleo, mahali ambapo hapana uchumi siku zote panaachwa na kutengwa hata na serekali.... Hii ndio maana kuna wakati flani mwaka uliopita Kenya na Ethiopia walitia mkataba kwamba kutajengwa industrial complex hapo mpakani mwa Kenya na Ethiopia kama vile mpaka wa north na south korea.....
Ukiangalia vile hali ilivyo, kule upande wa ethiopia kuna wanamgambo flani ambao wanapigana na serekali huko, badala ya Ethiopia kuwapiga na majeshi, Ethiopia ilichukua jamii flani na kuwa hami na mabunduki ili wapigane na hao wanamgambo wengine kwa niaba yao....
Juzi (Mwezi wa April) kuna kampuni ya Kenya ilipewa kandarasi kuziba vichochoro border ya Kenya na Ethiopia ili kuzulia smuggling ya watu,bidhaa na silaha, lakini kabla kuanza kazi, serekali ya Kenya ilienda kujulisha Ethiopia, katika huo mkutano hao wanamgambo wa serekali wakapinga hilo jambo vibaya na wakasema hawatokubali Kenya kuziba vichochoro....
Kenya ikarudi na ikaanza kuziba vichochoro, kilichofwata ni kampuni hio ilishambuliwa kwa risasi wakati wanaziba, hadi ikabidi KDF watumwe mbio mbio waende wapambane nao
--------------------
APRIL 1 2020 Tension is high in Moyale town after Ethiopian gunmen, said to be unhappy with the closure of Kenyan border to arrest the spread of coronavirus, attacked a team of local contractors.
The contractors, who started work on Monday, had been hired by the county administration to dig tunnels on the borderline to stop entry and exit from Kenya.
Source told the Nation that the gunmen opened fire on the workers as they excavated a tunnel on Wednesday morning, ripping apart the fuel tank of an excavator .
Gunshots rent the air as the gunmen in military uniform engaged the Kenya Defence Forces (kdf) in sporadic exchange of fire and running battles.
"kdf has rushed to quell the tension and as we speak there is calm."
A Kenya Chamber of commerce official told the Nation that Ethiopian traders and security forces were unhappy with Nairobi's decision to close the border.
Reports indicate Ethiopian Takabas, the equivalent of Kenyan police reservists, expressed their displeasure and vowed to keep the border open.
A local was hit by a stray bullet and was treated at a local hospital and discharged.
“They got in touch with the Federal Government of ethiopia which responded and dispersed the militia,” the source said.
The fight followed a meeting between Moyale security team and the Ethiopian government over the trenches.
County commissioner Evans Achoki confirmed the incident.
Kenya closed the border in an attempt to contain the spread of coronavirus, an announcement that was made by Marsabit Governor Mohamed Ali on March 29.
He, however, noted that there were unauthentic crossing points and called on the national government to ensure police are stationed in the porous areas.
Ethiopian ambassador to Kenya Alem Meles said he could not comment at the time as he was waiting for briefing from Addis Ababa.
-------------------------------------------------------------------------
Ethiopian gunmen open fire on Kenyan workers in Moyale
KDF walipoitwakupambana na hao militia wa Ethiopia, upande huo mwengine anakoangalia huyo mwanajeshi ni ndani ya Ethiopia
![]()
![]()
![]()
Baada ya hapo sasa ilibidi KDF wenyewe ndo wachuku kazi ya kuziba vichochoro kwa mpaka wa Kenyana Ethiopia
![]()
Kwahivyo hizo sehemu za kwenye wapokot mpaka wa Kenya Uganda na ule upande wa Ethiopia, South Sudan ni labda sote tuamue kwa pamoja kuondoa mabunduki kutoka mikononi mwa wananchi, tena baada ya hapo tupeleke maendeleo hilo eneo lote, lakini eti nchi moja au nchi mbili zikiamua kuondoa bunduki,hizo jamii hua zinaenda kwa nchi ya tatu kununua bunduki, naskia huko unaweza kupata AK47 na elfu tatu pesa za Kenya, Hio ni bei ya Mbuzi mmoja, utakuta jamaa ana mbuzi elfu moja....