Kule kaskazini mwa Msumbiji sasa hivi kuna mapigano makali sana kati ya vikundi vya kigaidi vya kiisilamu na majeshi ya Msumbiji, baadhi ya miji imetekwa na hao magaidi, hiyo miji imepakana na Tanzania.
Kama tukizembea ni rahisi sana kusini mwa Tanzania kukapata athari itokanayo na hivyo vita, magaidi wanaweza kuingia Tanzania kujificha, kuutafuta chakula, au kuuza silaha ili wapate pesa za kugharimia vita.
Tanzania tumepeleka vikosi vya POLISI na JWTZ kulinda huo mpaka kwa wingi sana, sidhani kama hata panya ataweza kuvuka huo mpaka. Ni udhahifu kwa Serikali yoyote kushindwa kuimarisha usalama wake kwa kisingizio cha ukosefu wa amani wa nchi jirani, Burundi na DRC zimekua katika vita kwa miaka mingi, lakini tulifanikiwa kuwazuia wasitetereshe usalama wa Tanzania, GoK ni dhahifu sana, hilo lazima mkubali.