Wakenya tushukuru Mungu kwa demokrasia yetu, watani wetu wamebanwa hadi wanalia toshaaa, wanakiri kwamba nchi yao sasa imekuwa 'Police State'

style imechukuliwa kenya sema tz hatuui kama nyie,btw una idadi ya watu wsliokufa toka uchaguzi uishe ???????

Tz hamuui kwa sababu watu wenu waoga, wakiskia mikwara kama hiyo wanaufyata na kujifungia ndani, hadi nakumbuka Mange Kimambi alibaki kuandamana mwenyewe kule Marekani, na hata wachache walioandamana naye walificha nyuso zao. Kenya watu hutoka, nyomi balaa, maandamano kama ya Kikenya ni vigumu sana kukamilika bila maafa.
Ndio imetuwezesha kupata katiba bora kuliko zote ukanda huu, tumeendelea kiuchumi na kijeshi na kutawala EAC na Kati kwa kila kitu ikiwemo kielimu....
Nyie mna kila kitu lakini maskini wa kutupwa maana uwoga wa kuthubutu, hamna jeuri ya kuhoji, leo hii spika wenu amekua mungu mtu..

Ona picha hapa ya Watanzania walioandamana na Mange Kimambi, wameficha nyuso, yaani watu wako Ulaya lakini full uwoga

maxresdefault.jpg

Angalia hapa maandamano ya Kikenya
9b2475cd342c4ea18ae3d0893175357a_18.jpg
 
Jamaa anasema bofya link, wakati hakuna link. Anatafuna miraa huyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Una uhakika kwamba hamna link? Hebu rudi usome taarifa ya mada hii kwanza kisha uniambie baada ya sentensi ya mwisho utaona nini hapo chini. Hii tabia ya baadhi yenu, ya bendera fata upepo, kukurupuka ovyo ovyo na uvivu wa kujisomea wenyewe na kujiongeza, ndio kitu ambacho kinawatafuna na kuwajaza ulofa wa aina yake.
 
Boss umebofya hiyo link hapo na ukasoma taarifa yenyewe? Au umetangulia tu kutupia comment ya kishabik? Hii ni sifa mbaya sana kwa nchi yenu. Wakenya tumeishi kwenye hali kama hiyo ya 'police state' chini ya utawala wa rais mstaafu Daniel Arap Moi, almaarufu Nyayo. Usitamani kuyaona yale ambayo sisi tuliyashuhudia. Wazazi wetu wakivamiwa usiku wa manane na kuzabwa makofi, huku wakinyanyuliwa juu kwa juu na kutupwa kwenye landcruiser na kutawacha tukijiuliza kama ndio itakuwa siku yetu ya mwisho ya kuwaona kwa macho yetu mawili.
Kumbe mnakijua kiswahili vizuri hivi...
 
Huifaham Tz wewe. Wacha nikuache na ujinga wako, nchi yako ako na hali mbaya, unajifanya kuwa concerned na Tz. Baki hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mada sio kunihusu mimi binafsi au ufahamu wangu kuhusu masuala ya nchi ya Tz. Taarifa ipo wazi na inahusu ripoti rasmi kutoka kwa mashirika 65 ya kutetea haki za kibinadam na kidemokrasia. Kama unaona ni uongo tudhibitishie kwamba yote yanayosemwa na tunayoyaona, kuhusu ukandamizaji wa upinzani, wanahabari na kuminywa kwa haki za wananchi sio kweli kabisa. La sivyo, pita kimya kimya.
 
Tutakuja ku copy mikakati ya kenyatta alivyo wadhibiti hawa NGOs..Hata baada ya serikali yake kuua watu 200 wakati wa chaguzi, Kufunga Tv zote kenya kwa wiki mbili, NGOs sasa wamekamatwa pabaya..waki jaribu kuongea kidogo wanafunguliwa kesi ya KRA😂😂😂
Naona hapa kuna lakujifunza
 
Hongera zenu kwa kuwa wanaume waoga. Naona mmejikita kwenye kuikashifu demokrasia ya Kenya ila hamuisifii wala hamdhubutu kuitaja Tz. Sitawakwaza, acha tukubaliane tu, kwamba Kenya kwenye demokrasia bado sana na Tz ndio ina demokrasia kamili, ya kuigwa na nchi zote duniani.

Achana na longolongo. Wee lete democracy index.
 
  • Thanks
Reactions: Oii
Achana na longolongo. Wee lete democracy index.
Freedom in the World 2018, hizi ndio nchi kumi duniani zinazoangaziwa
kwa kuminya demokrasia, kukandamiza wanahabari na haki za kisiasa za wananchi wao.
FitW7_820px_Country_Trend_Arrows-cropped.png
 
Tutakuja ku copy mikakati ya kenyatta alivyo wadhibiti hawa NGOs..Hata baada ya serikali yake kuua watu 200 wakati wa chaguzi, Kufunga Tv zote kenya kwa wiki mbili, NGOs sasa wamekamatwa pabaya..waki jaribu kuongea kidogo wanafunguliwa kesi ya KRA😂😂😂
Naona hapa kuna lakujifunza
Eti TV zote kafungwa kwa wiki mbili?? Mbona usiweke hicho kitu unavuta chini na uondoke hapo upesi!
 
Tz hamuui kwa sababu watu wenu waoga, wakiskia mikwara kama hiyo wanaufyata na kujifungia ndani, hadi nakumbuka Mange Kimambi alibaki kuandamana mwenyewe kule Marekani, na hata wachache walioandamana naye walificha nyuso zao. Kenya watu hutoka, nyomi balaa, maandamano kama ya Kikenya ni vigumu sana kukamilika bila maafa.
Ndio imetuwezesha kupata katiba bora kuliko zote ukanda huu, tumeendelea kiuchumi na kijeshi na kutawala EAC na Kati kwa kila kitu ikiwemo kielimu....
Nyie mna kila kitu lakini maskini wa kutupwa maana uwoga wa kuthubutu, hamna jeuri ya kuhoji, leo hii spika wenu amekua mungu mtu..

Ona picha hapa ya Watanzania walioandamana na Mange Kimambi, wameficha nyuso, yaani watu wako Ulaya lakini full uwoga

maxresdefault.jpg

Angalia hapa maandamano ya Kikenya
9b2475cd342c4ea18ae3d0893175357a_18.jpg
UZURI WEWE SIYO MGENI NA WABONGO,UNATUJUA VIZURI UNAFIKI WETU....ILA TAKE THIS FROM ME...HALI NI MBAAAAYAAAAAA SANA,SANA TU.
 
Chuki za ccm kwa upinzani zinazidi mara mia chuki za kikabila Kenya.
Hiyo ni simple mind kama jina lako,hakuna nchi iliyokamilika 100percent,ila sehemu yenye Ukabila,udini,ukanda ni hatari sana,Siasa za Tz zinachange kila wakati na asilimia kubwa ya wanasiasa waTz ni wachumia tumbo iwe CCM CDM,Cuf,ACT,Tadea wote wanahangaikia matumbo yao
 
Una uhakika kwamba hamna link? Hebu rudi usome taarifa ya mada hii kwanza kisha uniambie baada ya sentensi ya mwisho utaona nini hapo chini. Hii tabia ya baadhi yenu, ya bendera fata upepo, kukurupuka ovyo ovyo na uvivu wa kujisomea wenyewe na kujiongeza, ndio kitu ambacho kinawatafuna na kuwajaza ulofa wa aina yake.
Lakini si ni kweli unatafuna miraa buda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mada sio kunihusu mimi binafsi au ufahamu wangu kuhusu masuala ya nchi ya Tz. Taarifa ipo wazi na inahusu ripoti rasmi kutoka kwa mashirika 65 ya kutetea haki za kibinadam na kidemokrasia. Kama unaona ni uongo tudhibitishie kwamba yote yanayosemwa na tunayoyaona, kuhusu ukandamizaji wa upinzani, wanahabari na kuminywa kwa haki za wananchi sio kweli kabisa. La sivyo, pita kimya kimya.
Haya. Wewe na wenzako mnaotetea haki za watz, basi tuone 2020, kama haki walinyimwa watamkataa huyu bwana, kama haki na maendeleo walivipata, watamchagua tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio mbaya kuendelea kujificha kwenye blanketi la walanguzi,vyeti feki nk.Pia sihitaji kubishana na maoni yako na kama unakula bata basi hongera sana.
Basi usitusemee wa Tz wote tuko na hali mbaya. Wengine wengi tunafurahia tunakula matunda ya majasho yetu, wachache wa vyeti feki na walanguzi wenginwle wa awamu ya nne lazima muwe haters.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom