Hehehe!! Sizitaki mbichi....
Halafu hivi unajua sio lazima kila mtu amiliki shamba, kunao wachakarikaji mjini ambao maisha yao yote hawajawahi kukamata jembe, na wanaingiza kipato mara mia ya wewe na hako kashamba kako kijijini. Sio lazima tulime sote, kuna wale tunachangia kwenye uchumi kwa njia zingine mbadala.
Cha msingi ni kuhakikisha malengo yako yamekaa sawa, unatimiza majukumu yako kwa familia kwa kuwapa nyumba nzuri, elimu, chakula, usafiri, mawasiliano n.k.
Teh teh teh,
Mbona povu na maneno meengi utafikiri muimba mchiriku.
😁😂🤣
Aliyekuambia maisha bila gari hayaendi ni nani?
Kuna watu kibao tu duniani hawana magari na wanafika sehemu yoyote ile, tena kwa wakati. Wanafika kazini, sokoni, Ibadan, kusalimia ndugu na jamaa, lkn hawaja wahi miliki gari hata siku moja maishani mwao. Wee unataka utuaminishe kuwa kumiliki gari ni utajiri. Wakati kwa mtu makini kama mimi, labda umiliki gari linaloingiza hela kama kirikuu au daladala au bodaboda, lkn kama umiliki gari ambalo linachukua hela mfukoni mwako, hiyo ni hasara, it's a liability not an asset. Siyo kitu cha kujisifu nacho.
Huyu jamaa aliyeuliza takwimu za mashamba, amefikiria mbali sana. Anaulizia wangapi wanamiliki Mali ambazo zinapanda thamani kadiri muda unavyo songa? Mfano mashamba *au real estate kwa ujumla), ambayo ni Mali hai. Magari ni mali mfu, kwa maana huzidi kupoteza thamani yake kadiri muda unavyoyoyoma.
Kwa upande mwingine ulaya na marekani wanaanza kutafuta namna ya kupunguza uhitaji wa magari binafsi kwa kuboresha zaidi usafiri wa umma, yaani uwe unapatikana kwa muda mfupi zaidi na kuchukua watu wengi zaidi kwa mkupuo. Pia wanajitahidi kuongeza baiskeli za umma, pay n ride. Ili kupunguza magari binafsi na hatimaye kupunguza uchafuzi wa anga hewa.
Hivyo magari si kitu cha kukionea fahari katika miji au nchi. Ni janga hilo, linalohitaji kudhibitiwa.